Most Wanted

Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
35,999
24,163
una mtu wako wa karibu ama ndugu
anatafutwa kwa makosa kadhaa
na wewe unataarifa zake

najua kitu sahihi ni unatakiwa upeleke taarifa kwenye mamlaka husika.
Lakini, mbona inakuwa ngumu sana kumtoa kafara??

Ni nini cha kufanya kwa hali kama hii? Ushauri tafadhali.
 
Kongosho hili swala kiukweli jibu lake halipatikan kwa mara moja ama paspo kiuface situation. Kuna mambo mengine maishan huwez kuwa na majibu yake hadi unapoiface situation husika. sababu hasa ni kwamba jambo hilo litokeapo suluhu yake hupatikana hapo hapo so ukikaa kuimagine tu huwez kupata.

hapa nikitoa jibu nitatoa bila kuangalia extent ya kosa, na jinsi ambavyo mmelipokea nyie ndugu na adhabu itakayomkabili na extent ya impact ya adhabu.

ushauri wangu wa busara kwako, pima aina ya kosa, angalia na adhabu iloko mbele yake kisha extent ya impact ya adhabu husika. kisha urudi upande wa pili angalia je nikimficha nitapata faida gani na nitapata hasara gani na nitakuwa nalea ama nakemea uovu??? na je nikimficha ataelewa kwamba sipendi tabia aloifanya aa atatumia kama loope hple ya kuwa mkosa zaid??
 
Last edited by a moderator:
Makosa yapo ya aina mbali mbali kinachoshindikana nikwenda kumripoti kituo cha polisi kwakuwa maranyingi ni adha za mahabusu ila kama hapo awali nilivyosema inategemea ni kosa gani!Kama nijambazi lakutumia silaha mimi nitamtoa kafara ila kama ni makosa mengine yasiyo husu maisha ya mwanadamu mojakwamoja basi chakufanya nikwenda kusikilizia polisi nini wanataka nakama kuna aja yakuyamaliza tuna yamaliza juu kwa juu!
 
Angalia madhara yatakayojitokeza baada ya sheria kufuata mkondo wake..kama ana familia na vitu km hivyo,au kama anategemewa na wazaz..endapo majibu ya hayo ni ndio basi mchunie mpaka watakompata wenyewe. Ila kama hana anaemtegemea na keshafanya uharibifu mkubwa... Toa tu taarifa wangu,lakin usi-disclose kuwa ndo umemchoma..# mtazamo wangu
 
nimewapata wakuu
inakuwa tabu pale mtu wa aina hiyo anapohitaji assistance ya kumficha.

Si ndio mtu unajikuta umekuwa accomplice bila kutarajia?

Naogopa!
 
hapa bongo ingekuwa kila kosa linapelekwa kwenye vya dola robo tatu ya watz tungekuwa tupo magerezani
 
nimewapata wakuu
inakuwa tabu pale mtu wa aina hiyo anapohitaji assistance ya kumficha.

Si ndio mtu unajikuta umekuwa accomplice bila kutarajia?

Naogopa!

Aaaah...tena ukija kugundulika umemficha lazima muonekane wamoja. Kumficha not a good idea,muelezee consequences zake..usijejitia matatizon bila sababu ya msingi.
 
una mtu wako wa karibu ama ndugu
anatafutwa kwa makosa kadhaa
na wewe unataarifa zake

najua kitu sahihi ni unatakiwa upeleke taarifa kwenye mamlaka husika.
Lakini, mbona inakuwa ngumu sana kumtoa kafara??

Ni nini cha kufanya kwa hali kama hii? Ushauri tafadhali.

Kama ni ndugu yako ni ngumu sana kumtoa kafara, maana hata ndugu waliokuzunguka wanaweza kukushangaa na kutokukuelewa. Cha msingi ni labda wewe ukae kimya usipeleke taarifa kwenye mamlaka husika na kisha pia usijitwishe zigo la kumficha. Acha mamlaka ishughulike naye nje ya mikono yako. Jitahidi kwa namna yeyote ile huyo ndg yako asikae kwako kwa kutafuta visingizo hamsini elfu vya kwa nini asikae kwako! Kisingizio kimoja ni kuwa una marafiki wengi ambao ni askari, hivyo akikaa kwako ni rahisi kukamatwa!!!
 
nimewapata wakuu
inakuwa tabu pale mtu wa aina hiyo anapohitaji assistance ya kumficha.

Si ndio mtu unajikuta umekuwa accomplice bila kutarajia?

Naogopa!

Ishu ya pembe za ndovu imefikia hapo? We mfiche tu lakini kwa jinsi navyopenda kutizama wanyama nikimuona namchoma!
 
Pole sana binamu.
Naona suala ushalipatia jibu, wadau wamekupa angle zote.
Ila nilikuwa sijui kama we mchaga lol, maana matangazo ya "anatafutwa" niliyonayo wote ni wachaga tu.
 
inategemea na kosa alilofanya kama unaona nibora kumwambia asepe mapema nje ya hapo na wewe utaingizwa kwenye kudi la kusaidia polisi (vyombo vya dola). Nina ndugu zangu miaka zaidi ya 5 wako jera wanasota kwa kukaa na jamaa alikuwa anatuhumiwa kwa kukata mapanga wazee wenye macho mekundu polisi walipofika waliwachukua familia nzima mpaka leo hii wako selo. kifupi ukiona atakuingiza kwenye matatizo bora undugu uishe mwambie kabisa akimbie nje ya hapo toa taarifa sehemu husika
 
Napenda filosofia ya mafia kwenye maswala ya la familia. Family first n family stick together.
 
Back
Top Bottom