Mossad ya Israel ilimuua mwanasayansi wa Iran

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Trump athibitisha kuhusika Mossad katika mauaji ya shahidi Fakhrizadeh

Nov 28, 2020 07:46 UTC

[https://media]

Hatua ya rais wa Marekani ya kuusambaza ujumbe ulioandikwa na mwandishi mmoja wa habari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel imethibitisha kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuhusika utawala huo katika mauaji ya mwanasayansi wa nyuklia wa Iran.

Magaidi wenye silaha jana jioni waliishambulia gari iliyokuwa imembeba Mohsen Fakhrizadeh, Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu la Wizara ya Ulinzi ya Iran na kumuua shahidi mwanasayansi huyo.

Kufuatia jinai hiyo ya kinyama, Rais Donald Trump wa Marekani ameamua kuutuma tena katika ukurasa wake wa Twitter ujumbe ulioandikwa na mwandishi wa habari wa Israel, ambaye amesema katika ujumbe wake huo kwamba shahidi Fakhrizadeh alikuwa akifuatiliwa kwa miaka kadhaa na shirika la ujasusi la utawala wa Kizayuni Mossad.

[https://media]Ujumbe uliosambazwa tena na Trump

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amelaani vikali hujuma hiyo ya kigaidi na kuongeza kuwa, kuna ushahidi mkubwa unaoonyesha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umehusika katika mauaji ya Fakhrizadeh, ambaye pia alikuwa profesa wa fizikia katika Chuo Kikuu cha Imam Hussein mjini Tehran.

Zarif amesisitiza kuwa Iran inaitaka jamii ya kimataifa na hasa Umoja wa Ulaya uache kutumia vigezo vya kuaibisha vya undumakuwili na kulaani kitendo hicho cha kigaidi.../

Tags

4bvfd4685819a91rvpk_800C450.jpeg
 
Hatua nzuri sana hii. Kama kweli Mossad wamehusika pongezi nyingi sana kwao maana kwa kifo cha Fakrizadeh uhai wa maelfu ya watu duniani umeokelewa. Silaha za maangamizi alizokuwa ana pioneer zingekuja kumaliza wengi.
 
Swali ni hili; je alikuwepo yeye pekee katika mpango huo???, je yeye alikuwa mwanasayansi pekee wa Nuclear aliyebaki??.
 
Kuna watu watakamatwa na kunyongwa miezi ijayo kwa haya mauaji.
 
Hatua nzuri sana hii. Kama kweli Mossad wamehusika pongezi nyingi sana kwao maana kwa kifo cha Fakrizadeh uhai wa maelfu ya watu duniani umeokelewa. Silaha za maangamizi alizokuwa ana pioneer zingekuja kumaliza wengi.

Kuna nchi hapa duniani zikiwa na nuclear ndio kutakua na amani zaidi duniani sababu kutakua hakuna mambo ya kijinga ya kuvamiana vamiana bila sababu na wataheshimiana sana mfano tu uwepo wa nuclear kule korea kaskazini japo ni nchi masikini lakini huwezi kwenda kuivamia hivi hivi tu lazima ujipange sana na nina kuhakikishia north korea isingekua na nuclear ingekua imeisha pigwa zamani sana
 
Hatua nzuri sana hii. Kama kweli Mossad wamehusika pongezi nyingi sana kwao maana kwa kifo cha Fakrizadeh uhai wa maelfu ya watu duniani umeokelewa. Silaha za maangamizi alizokuwa ana pioneer zingekuja kumaliza wengi.
Hizi akili uwa zinanifurahisha. Hivi hao wengine wanaomiliki hizo silaha uwa wamezitengeneza kwa ajili ya mapambo au? Kwanini utengeneze kitu tena una kiupgrade kila mara wakati huhitaji kukitumia?

Na toka dunia imeumbwa ni taifa moja tu liliwahi kutumia silaha za Nuclear, na ni Marekani. Hakuna taifa lingine limewahi kuzitumia dhidi ya taifa lingine.
 
Trump athibitisha kuhusika Mossad katika mauaji ya shahidi Fakhrizadeh

Nov 28, 2020 07:46 UTC

[https://media]

Hatua ya rais wa Marekani ya kuusambaza ujumbe ulioandikwa na mwandishi mmoja wa habari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel imethibitisha kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuhusika utawala huo katika mauaji ya mwanasayansi wa nyuklia wa Iran.

Magaidi wenye silaha jana jioni waliishambulia gari iliyokuwa imembeba Mohsen Fakhrizadeh, Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu la Wizara ya Ulinzi ya Iran na kumuua shahidi mwanasayansi huyo.

Kufuatia jinai hiyo ya kinyama, Rais Donald Trump wa Marekani ameamua kuutuma tena katika ukurasa wake wa Twitter ujumbe ulioandikwa na mwandishi wa habari wa Israel, ambaye amesema katika ujumbe wake huo kwamba shahidi Fakhrizadeh alikuwa akifuatiliwa kwa miaka kadhaa na shirika la ujasusi la utawala wa Kizayuni Mossad.

[https://media]Ujumbe uliosambazwa tena na Trump

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amelaani vikali hujuma hiyo ya kigaidi na kuongeza kuwa, kuna ushahidi mkubwa unaoonyesha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umehusika katika mauaji ya Fakhrizadeh, ambaye pia alikuwa profesa wa fizikia katika Chuo Kikuu cha Imam Hussein mjini Tehran.

Zarif amesisitiza kuwa Iran inaitaka jamii ya kimataifa na hasa Umoja wa Ulaya uache kutumia vigezo vya kuaibisha vya undumakuwili na kulaani kitendo hicho cha kigaidi.../

Tags

View attachment 1637594
Mossad hata rais wa hao vibaraka wako Iran wanaweza mdedisha wakiamua, ila Israel ni wastaarabu sana wapigie makofi hapo ulipo moro
 
Viongozi wa Iran akili hawana hivi wanasayansi kila Siku wanauawa halafu wanaendelea kuishi bila ulinzi HV mwanasayansi mkubwa hvyo anatembelea Nissan fuga anashindwa usafiri hata na mkuu wa wilaya huku Tanzania anatumia v8 MTU ambaye muhimu angekuwa na gari isiyopenya risasi kwa uchumi wa Iran wanauwezo kuyapata.
 
Kwanza aliyepost siyo msemaji wa jeshi au serikali, hata hivyo ujumbe huo haubainishi kuwa Mossad ndio waliohusika. Kufuatilia na kumuua mtu ni viti viwili tofauti.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Hata mimi nimejiuliza swali hili hili. Hivi hawezi kununuliwa gari bullet proof la USD500,000? Akawa na escort ya polisi? Mambo mengine wanayataka wao.
Viongozi wa Iran akili hawana hivi wanasayansi kila Siku wanauawa halafu wanaendelea kuishi bila ulinzi HV mwanasayansi mkubwa hvyo anatembelea Nissan fuga anashindwa usafiri hata na mkuu wa wilaya huku Tanzania anatumia v8 MTU ambaye muhimu angekuwa na gari isiyopenya risasi kwa uchumi wa Iran wanauwezo kuyapata.
 
Hatua nzuri sana hii. Kama kweli Mossad wamehusika pongezi nyingi sana kwao maana kwa kifo cha Fakrizadeh uhai wa maelfu ya watu duniani umeokelewa. Silaha za maangamizi alizokuwa ana pioneer zingekuja kumaliza wengi.
Mkuu achana na propaganda za wazungu wa Magharibi na Israel. Mbona Korea kaskazini, Pakistani na India wanazo hizo silaha na hakuna mauaji ya wengi.

Hawa wanachoogopa Iran wakimiliki hizo silaha hawawezi kuwatisha na kuwatawala milele. Maisha yangu mimi na wewe yatabaki salama.
 
Viongozi wa Iran akili hawana hivi wanasayansi kila Siku wanauawa halafu wanaendelea kuishi bila ulinzi HV mwanasayansi mkubwa hvyo anatembelea Nissan fuga anashindwa usafiri hata na mkuu wa wilaya huku Tanzania anatumia v8 MTU ambaye muhimu angekuwa na gari isiyopenya risasi kwa uchumi wa Iran wanauwezo kuyapata.
Labda fuatilia tena mkuu, ulinzi alikuwa nao Tena mzuri tu
 
Back
Top Bottom