Mossad, operation bayonet: Jinsi kisasi kinavyoweza kuwa njia bora ya kupata haki yako

Complex

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
4,113
4,741
Kisasi ni neno lisilo na ubinadamu kwa baadhi, lakini kwa wengine ndiyo njia pekee waliyojichagulia kupata haki katika kile wanachoamini ni haki yao. Ni mwaka 1972 katika mashindano ya Olympic yaliyopangwa kufanyika Mjini Munich, Ujerumani.

Maandalizi ya kuweka mandhari ya miundombinu katika hali ya kupokea wageni wanaotarajiwa katika mashindano hayo yakiwa yanaendelea, Upande wa pili katika nchi ya Lebanon wanachama wa kikundi cha kigaidi kilichojulikana kama BLACK SEPTEMBER ambacho ni kilikuwa ni kikundi tanzu cha PALESTINE LIBERAZATION ORGANIZATION (PLO) nao walikuwa wakichukua mazoezi kwa ajili ya mashindano hayo ya Olympic ambayo kwa mwaka huo yalipangwa kufanyika Ujerumani.

Katika mwaka huo Wapalestina kama yalivyo mataifa mengine, waliandika barua ya kuomba ushiriki wa Olympic, Lakini kwa kuwa halikuwa taifa huru na linalotambulika katika jumuiya ya kimataifa, Maombi yao hayakujibiwa. Na hii ilikuwa na maana nyingine kuwa wamekataliwa.

Kutokana na hili PLO wakaamua kupanga kushiriki mashindano hayo kinamna nyingine. Na namna hiyo si nyingine bali Kwenda kufanya tukio la kigaidi katika mashindano hayo ambalo litaishangaza na kuisimamisha dunia.

Ilikuwa ni January 1972 wakati ujerumani wakijiandaa na maandalizi, Nchini palestina Viongozi wanne wa juu wa PLO walipanga kukutana kwa siri nchini Beirut kusuka mpango kabambe wa kutimiza adhma yao ya kufanya tukio la kuisimamisha dunia.

Viongozi hao si wengine bali walikuwa ni MAHMOUD YOUSEF NAJAR ambaye alikuwa kiongozi wa tatu kwa ukubwa katika PLO, MOHAMED DAOUD UDE aka ABU DAOUD ambaye alikuwa ndiye msuka mipango wa PLO, ALI HASSAN SALAMEH aka RED PRINCE ambaye alikuwa ndiyo kiongozi ushushushu na ujasusi katika operation hiyo ya BLACK SEPTEMBER , na wa mwisho alikuwa ni ABU IYAD ambaye ndo alikuwa mkuu wa ujasusi wa PLO.

salameh.jpg

Ali Hassan Salameh

Katika kupanga na kusuka mikakati, viongozi hao waligundua kuwa hawatoweza kufanikiwa adhma yao bila kupata taarifa za sehemu ambapo mashindano hayo ya Olympic yalipangwa kufanyika. Na taarifa hizo ingewawia rahisi kuzipata kama wangekuwa na urafiki na watu ambao ni raia na wakazi wa Ujerumani. Ni katika hili wakaomba ushirikiano na kikundi cha kigaidi cha ujerumani kilichojulikana kama RAF.

Kufikia mwezi wa 8, RAF walianza kuwakusanyia taarifa BLACK SEPTEMBER kuhusu eneo ambapo Olympic ilikuwa inatarajiwa kufanyika. RAF walipiga picha za viwanja, majengo, watu na vyote vile ambavyo vilionekana vitakuwa vina umuhimu kwa BLACK SEPTEMBER. Haya yote yalikamilishwa na WILL VOLTZ ambaye alikuwa mwanachama wa RAF kwa kipindi hicho.

SIKU YA TUKIO
Ilkuwa ni september 5 1972 majira ya saa 10 alfajiri kikundi cha watu waliokuwa wamevaa mask waliingia katika kijiji cha olympic na kuanza kutafuta wanamichezo wa Israel ambao walikuwa tayari wameshawasili katika kambi. Huku wakiwa katika usingizi mzito, wanamichezo tisa wa israel walikamatwa na magaidi hayo.

Magaidi hayo walianza kuwaua kinyama kwa kumpiga risasi mwanamichezo mmojammoja huku wenzake wakiangalia na kushuhudia. Walikuwa wakitekeleza mauaji ya kinyama kwani walikuwa wakiua mateka mmojammoja katika muda uliopishana lisaa.

Magaidi wale wa BLACK SEPTEMBER waliendelea kuwashikilia mateka wanamichezo hao huku wakipaza sauti kwa serikali ya Israel na jumuiya ya kimataifa isikilize matakwa yao.

Kwa upande mwengine asubuhi hiyo ya september 5, Taarifa hizo za mauaji na mateka ya wanamichezo wakizayuni zilifika mezani kwa aliyekuwa waziri mkuu wa israel kwa kipindi hicho aliyekuwa akijulikana kwa jina la Bi GOLDE MEIR. Taarifa hizi zilimshtusha na kumfanya akumbuke unyama wa HOLLOCOUST waliofanywa waisraeli na serikali ya HITLER.

Na kwa haraka Bi MEIR aliliweka tukio hilo la Munich katika kundi la matukio ya kigaidi, na aliona kuwa suluhu ya kukabiliana na tukio hilo haikuwa nyingine bali ni kulipa kisasi kwa wote waliotekeleza unyama huo. Bila kupoteza muda, Bi MEIR alifanya mawasiliano na Bw. ZVI ZAMIR aliyekuwa mkurugenzi wa taasisi ya ujasusi (SPY CHIEF) wa nchi hiyo iliyojulikana kwa jina MOSSAD ,

Hakuishia hapo kwani pia alifanya mawasiliano General AHARON YARIV aliyekuwa mkuu wa kitengo cha ujasusi wa jeshi (Military inteligence) ili kuona kama kuna uwezekano wa kuokoa mateka.

4.2-Golda-Meir.jpg

Bi. Golde Meir

Ilipofika majira ya saa 8 mchana siku hiyo, tayari ZVI ZAMIR(Mossad spy chief) alikuwa ameshatua jijini Munich kuomba kutoa msaada kwa serikali ya ujerumani kukabiliana na tukio hili. Bila kupoteza muda akapelekwa katika eneo la tukio ambapo mateka walikuwa wameshikiliwa.

Wakati bwana ZAMIR na waandishi wa habari wakiwa wamezunguka jengo ambamo ndani yake walikuwa wameshikwa mateka, magaidi wale walitumia nafasi hiyo kupaza sauti ya kutaka waliokuwa takribani wafungwa 240 wa Kipalestina na Kijerumani(RAF) waachiwe huru. Baada ya madai hayo kufika kwa bwana ZAMIR, moja kwa moja aliandika Telegram na kuituma Tel aviv kwa Bi Meir.

Kwa hali ya ushujaa, Bi MEIR hakukubali madai hayo na alikataa kabisa kuingia katika meza ya majadiliano na magaidi hayo na badala yake alitaka wanamichezo wake waachiwe huru bila masharti yoyote.

...muendelezo ilipoishia(Part 2)
Nchini Israel habari kuu kwa siku hiyo ilikuwa ni juu ya habari ya kutekwa kwa wanamichezo wao, Wananchi walijawa hofu na kuonekana wakifuatilia kwa makini kisa hicho katika vyombo mbalimbali vya habari.

Katika hali ya kuonekana kuwa wataonekana dhaifu, Serikali ya ujerumani ilikataa msaada wa israel katika kukabiliana na tukio hilo. Badala yake waliagiza vikosi vyao vya usalama na ujasusi kwenda kufanya kazi ya kuwaokoa mateka na kuwakamata magaidi hao.

Kabla hilo halijafanyika, jioni ilikuwa imeshaingia na magaidi wakatoa madai ya kutaka wasindikizwe kwenda uwanja wa ndege wakiwa na mateka hao. Hii iliwafanya polisi kuibuka na mbinu kwamba wakubali maombi hayo na kuwategea watakapofika uwanja wa ndege basi wawashambulie na kuwakamata magaidi hao. Kwa bahati mbaya wakati magaidi wanafika uwanja wa ndege polisi waliwavamia na kuwashambulia.

Katika hali ya kupanic, majibizano ya risasi baina ya polisi na magaidi yakaibuka. Wakiwa wanaelekea kushindwa, Magaidi waliona hakuna njia nyingine zaidi ya kujitoa muhanga. Mmoja wa magaidi alichukua bomu la kutupa kwa mkono na kulilipua.

Hii ilipelekea magaidi watano pamoja na mateka wote kupoteza maisha papo hapo. Magaidi watatu walibaki hai, na polisi waliwakamata na kuwaweka korokoroni.

Ni simanzi na majonzi vilitanda jijini Munich kufuatia tukio hilo, kamati ya olympic iligoma kusitisha mashindano hayo kwani ingeonekana ni woga uliokithiri. Hivyo baada ya maombolezo, Mashindano yaliendelea bila ushiriki wa wanamichezo wa Israel. Wanamichezo wa israel waliosalimika walirejea israel na simanzi.

Wakati magaidi wakishangilia ushindi huo, nchini israel Bi MEIR aliitisha kikao cha usiri mkubwa (Top secret) cha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Waliunda kamati waliyoipatia jina "COMITEE X" kiongozi wake akiwa ni mkuu wa kitengo cha ujasusi cha jeshi la Israel (millitary inteligence) bw. AHARON YARIV.

Kamati hiyo iliibuka na ajenda ya kulipa kisasi cha unyama waliofanyiwa ama kwa lugha nyingine waweza sema "terrorizing the terrorists". Bw. YARIV ni muumini wa kulipa kisasi kwa njia ya kimya na kutojulikana (quiet and clean revenge).

Njia hii ilikuja kuridhiwa na kamati hiyo, kwani ndani ya miezi miwili toka tukio hilo la mateka wa olympic litokee, Wapalestina waliteka ndege ya shirika la Lufthansa wakidai kuachiliwa huru kwa wale magaidi watatu. Serikali ya Ujerumani ilitii sharti hilo, na kuwaachia magaidi wale.

Kitendo hicho kilifanya Israel ione haina mshirika, na hivyo kupanga kulipa kisasi yenyewe kama yenyewe kimya kimya na bila kutambulika (Quiet and Clean revenge).

COMITEE X ilichagua kikundi maalum cha mashushushu wa mossad ambao wangekamilisha kuwatafuta popote walipo wafanikishaji na washiriki wote tukio lile la september 5. Ndani ya mossad kazi ya kukusanya taarifa za wahusika ilianza huku bi MEIR akipewa taarifa ya kila hatua kwa ukaribu.

Katika taarifa hizo, Jina la ALI HASSAN SALAMEH likaibuka kama ndo mpangaji mkuu na mfanikishaji wa tukio hilo. Baada ya taarifa hizo kuibuka, Bi MEIR alimchagua jasusi mkongwe wa mossad MIKE HARARI kuongoza timu ya mashushushu wenzake waliochaguliwa ili kufanikisha lengo hilo la kulipa kisasi. Majasusi hao waliondolewa official links zote ambazo zingeweza kuwahusisha na israel pindi watakaposhtukiwa.

Hivyo walipewa passport za nchi nyingine na nyaraka mataifa mengine kwa ajili ya utambulisho. MIKE HARARI alichagua jiji la Paris kama makao makuu yake ya kuendeshea oparesheni hiyo. Alikaa Paris na kujifanya mfanyabishara kwa jina la EDWARD LATSKI. Hapo alipanga vikosi kazi vyake kwa ajili ya kutekeleza visasi.

5601146099340640360no.jpg

Bw. Michael Harari.


...muendelezo ilipoishia(Part 3)
KULIPIZA VISASI

Kufikia mwezi Oktoba, taarifa zilikuwa zimekusanywa kwa kiwango kikubwa na majasusi wa mossad na zilianza kufanyiwa kazi. October 16 timu ya assasins wa mossad walitua jijini Roma, Italia. Mtu wao wa kwanza kuuliwa katika list alikuwa ABDELWAHEL ZULETA.

ZULETA alikuwa ni mkalimani katika ubalozi wa Libya nchini Italia. Bwana ZULETA alikuwa na mahusiano ya karibu na PLO. Mossad walikuwa na taarifa kuwa ZULETA alihusika na Logistic ya tukio la Munich.

Takribani majira ya saa 4 usiku, ZULETA akiwa anarejea nyumbani kwake toka kazini alipigwa risasi 11 zilizomuingia kisawasawa mwilini. ZULETA alikufa papo hapo, na taarifa za kifo chake zikatumwa kwa Bi MEIR. Mamlaka ya polisi ya Italia walifika eneo la tukio na kukuta maganda ya risasi zilizotumika.

Maganda yale baada ya kuchunguzwa yalionekana kutoka katika bunduki aina ya BARETTA. Bunduki iliyopendelewa kutumiwa sana na Mossad. Lakini polisi hawakufanikiwa kung'amua lolote kuhusu wahusika wa mauaji ya bwana ZULETA .

DECEMBER 1972, Ufaransa. Dr. MAHMOUD HAMSHARI, msemaji wa PLO nchini Ufaransa alikuwa akiishi katika nyumba namba 175 LUDA LESSIA na familia yake. Kutokana na kazi yake, ilikuwa ni kawaida kwa Dr. HAMSHARI kukutana na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari.

Siku moja mwezi huo alipokea maombi toka kwa mtu aliyejifanya ni mwandishi wa habari akitaka kumuhoji. Masikini Dr Hamshari alishindwa kugundua kwamba mtu aliyeomba kukutana naye hakuwa mwandishi wa habari kama yeye alivyodhani. Ila mtu huyo alikuwa ni Jasusi wa Mossad.

Interview hiyo ilifanyika mahali alipokuwa akiishi, Wakati interview ikiendelea, yule shushushu alikuwa akiangalia na kuchunguza kwa makini nyumba ya Bw HAMSHARI na kukusanya taarifa muhimu ambazo zingewasaidia kutekeleza mauaji ya msemaji huyo wa PLO na baada ya mahojiano jasusi yule aliondoka.

Siku inayofuata jasusi yule aliamkia katika mgahawa mmoja uliokuwa karibu na alipokuwa akiishi Dr. HAMSHARI na kuanza kuangalia movements zote za watu wanaoingia na kutoka katika jengo alilokuwa kapanga Bw. HAMSHARI. Alipoona mke na mtoto wa Dr Hamshari wametoka kwa mizunguko, Alipiga simu katika simu ya mezani iliyokuwa katika nyumba ya Dr HAMSHARI.

Pasipo kujua Dr HAMSHARI alipokea simu ile, na hiyo ilipelekea vilipuzi vilivyokuwa vimepandikizwa katika simu ile kulipuka na kujeruhiwa vibaya hali iliyopelekea kupoteza maisha mwezi mmoja baadae.

Wiki tatu baadaye, Harari aliituma timu yake kwenda jijini Nicosia, Cyprus. Safari hii mlengwa alikuwa ni HUSSEIN ABADALHIYA. Huyu alikuwa ni kiunganishi mkubwa wa PLO na wasoviet kwani alikuwa ndiyo anayetumwa na kuweka mikakati yote ya ushirikiano baina ya Warusi na Wapalestina (PLO).

Siku ya tukio, akiwa anatoka katika kikao na maafisa wa urusi waliokuwa Cyprus, akiwa hana hili wala lile kama ilivyokuwa ada alirejea katika hoteli aliyofikia. Naye pasipo kujua, tayari majasusi wa Mossad walikuwa washaingia na kutega bomu katika kitanda chake.

Kama ilivyokuwa ada alifikia kulala, pressure bomb lililokuwa limepandikizwa kitandani lililipuka punde tuu alipolalia kitanda. Papo hapo akapoteza maisha na ndiyo ukawa mwisho wa maisha yake. Matukio haya yalidhihirisha alichokisema Bi MEIR ya kuwa wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine na tukio la Munich, watatafutwa kwa gharama yoyote na popote pale walipo.

Hili lilithibitishwa na aina ya matukio, kwani mpaka muda huo Mossad walikuwa wameshatekeleza mauaji matatu katika nchi tatu tofauti. Mpaka kufikia mwezi December 1972, Mossad walikuwa na orodha ya 98% ya waliohusika na mauaji ya Munich.

bbb.jpg

Baretta Pistol

April 1973 Paris, Ufaransa. Profesa wa sheria BAZIL AL KUBEZ alionekana akitoka katika mgahawa wa cefe de lape uliokuwa katika jiji hilo. AL KUBEZ alikuwa akielekea nyumbani kwake, akiwa mtaani akitembea ghafla alivamiwa na watu wawili wakiwa na bunduki mkononi.

Watu wale bila kukawia waliinua bunduki zao na kumpiga AL KUBEZ risasi 11 na kupelekea kufariki papo hapo kwa profesa huyo. Kama ilivyokuwa kwa polisi wa Italia, Polisi wa ufaransa pia walifika eneo la tukio na kukuta maganda ya risasi yaliyoonekana kutoka katika bunduki aina ya BARRETA, hii ilikuwa ni silaha pendwa ya shirika hilo la kijasusi la kizayuni.

Hii iliwafanya Ufaransa kuibua tuhuma za uhusika wa Israel katika tukio lile, lakini kama walivyokubaliana katika COMITEE X, Bi MEIR alikanusha vikali uhusika wa Israel katika tukio lile ingawaje ulimwengu wa kijasusi na halikadhalika kundi la kigaidi la BLACK SEPTEMBER walijua dhahiri kuwa Mossad wanahusika.

Wakati hayo yakiendelea, Bi MEIR aliweka msisitizo kuwa ni lazima kila aliyekuwa katika list yao auwawe hata wale ambao walikimbilia mafichoni katika nchi hasimu wa Israel. Safari hii ilikuwa ni zamu ya Jiji la Beirut, Lebanon. Taarifa ziliwafikia Mossad kuwa viongozi watatu wakubwa wa BLACK SEPTEMBER walikuwa wakiishi katika jengo moja katika jiji hilo.

Kutokana na umuhimu wa watu hao, safari hii kazi ilikabidhiwa kwa kikosi cha makomandoo wa Jeshi la Israel. Kazi ya Mossad ilikuwa ni kuwakusanyia taarifa makomandoo hao ikiwemo taarifa za mchoro wa jengo walilokuwa wakiishi, muda wa kuingia na kutoka nk.

Baada taarifa hizo kupatikana, zilipelekwa mezani kwa COMITEE X na makomandoo walialikwa ili kupanga mipango ya namna ya kutekeleza mauaji ya viongozi hao wakubwa wa BLACK SEPTEMBER.

Baada ya mipango kukamilika, usiku wa April 9, 1973 vikosi cha makomandoo vilivyokuwa vikiongozawa na EHUD BARAK (aliyekuja kuwa Waziri Mkuu wa Israel miaka ya 2000) vilikwea boti za kasi kuelekea pwani ya Beirut huku wakisindikizwa na boti za kivita zenye makombora ambazo zenyewe baada ya kufika pwani zilipaki.

Katika pwani hiyo kulikuwa na majasusi wa Mossad waliokuwa wakiwasubiria kuwabeba na kuwapeleka katika jumba hilo ambalo lilikuwa likilindwa na takribani wanamgambo 100. Wakiwa njiani kuelekea katika jumba hilo, BARAK alipokea simu toka kwa majasusi wa Mossad kuwa kuna Polisi watatu walikuwa wakilizunguka wakifanya doria jengo hilo.

BARAK alifanya maamuzi ya haraka na kuamuru askari wake watatu washuke na kutembea kama wapenzi kuelekea katika jengo lile, Alihofia kupiga simu Tel Aviv kwani kupiga simu kungeweza kupelekea kusitishwa kwa misheni ili.

Makomandoo hao wa Israel watatu walipenya katika jengo bila kushtukiwa na wale polisi waliokuwa wakifanya doria mitaa ile na kufanikiwa kutega milipuko kwa lengo la kuharibu mfumo wa umeme huku EHUD BARAK akiwa na timu ya watu wengine nje kuangalia usalama na kutoa back up kama mambo yatakwenda kombo.

download.jpg

Yaseer Arafat

Milipuko ile iliyotegwa ikalipuliwa na kuibua taharuki kubwa miongoni mwa wakazi wa jengo lile. Haikuchukua muda kwa magaidi kutambua kuwa wamevamiwa na hatimaye mapigano ya risasi yaliibuka katika kiza kilichokuwa kimesababishwa na milipuko ile.

Vikosi vya BARAK kwa kushirikiana na Mossad vilifanikiwa kuua viongozi wale watatu na baadhi ya wanamgambo wao huku wao wakipoteza makomandoo wawili katika mapigano hayo.

Kwa haraka BARAK aliinua simu ya upepo na kupiga katika pwani ambapo boti zilizokuwa zikiwasubiria zilikuwa zimepaki. Simu hiyo iliwataka manahodha waliokuwa katika boti hiyo kuwasha vyombo vyao kwani wao walikuwa wamemaliza kazi iliyowapeleka.

Kwa msaada wa majasusi wa Mossad waliokuwa wanaijua mitaa ya beirut vyema, vikosi vya BARAK vilifanikiwa kutokokomea mpaka pwani na kukwea boti zile na kutokomea zao baharini kwa safari ya kurudi Israel. Bahati mbaya kwa vikosi vya BARAK vilikosa kumuua YASEER ARAFAT aliyekuwa mkuu wa PLO kwa wakati huo.

Pamoja na hilo vikosi hivyo vilijiona washindi kwa kufanikiwa kuua viongozi watatu wa juu wa mamlaka ya Kipalestina. Viongozi hao wa BLACK SEPTEMBER waliouliwa alikuwamo MAHMOUD YOUSEF NAJAR, KAMAL ADWAN pamoja na msemaji wa PLO aliyejulikana kama KAMAL NASSER. YASEER ARAFAT akiwa kama kiongozi wa PLO alipaza sauti akitaka dunia iwasikize PLO juu ya unyama huo waliofanyiwa na ISRAEL

Mjini Athens, Ugiriki. Asubuhi ya siku inayofuata MOUSA ABU ZIYAD alizisikia taarifa za kilichotokea Lebanon kupitia redio. ABU ZIYAD alikuwa ni muhusika mwengine wa mauaji ya jijini Munich ambaye alikuwa katika listi ya wanaohitajika kuuwawa na Mossad.

Katika kutaka kupata ukweli na uhakika wa habari na kujua kile kilichotokea lebanon, ABU ZIYAD aliamua kushuka chini toka katika ghorofa alilokuwa amepanga kwa lengo la kwenda kununua gazeti.

Maafisa wa Mossad waliokuwa wakimfuatilia walitumia mwanya huo kuingia ndani mwake na kupandikiza vilipukwa vya plastiki katika kitanda chake. dakika chache baada ya kurudi toka kununua gazeti, na kufika kukaa kitandani, ABU ZIYAD alikufa kwa mlipuko uliotokana na vilipuzi vilivyokuwa vimepandikizwa katika kitanda chake.

Katika hatua nyingine, kufuatia mauaji ya NAJAR na wenzake yaliyotokea nchini Lebanon, Ilipelekea ALI HASSAN SALAMEH alijikuta akipanda cheo katika uongozi wa PLO. Hii ilipelekea SALAMEH kuwa most wanted na mamlaka za kijasusi za Israel. Ilikuwa ni July ya 1973, Mossad walipata taarifa kuwa SALAMEH yupo nchini Norway.

Baada ya kupata taarifa hiyo, HARARI alisafiri mwenyewe kwenda mpaka nchini Norway kwa ajili ya kufanikisha mauaji ya SALAMEH. HARARI akusafiri peke yake, bali alisafiri na timu mbili, timu moja ikiwa ni ya wasuka mipango na vifaa na ya pili ilikuwa ni ya kutekeleza mauaji.

Kufuatia taarifa walizokuwa wamezipata, haikuwawia muda usiku mmoja walimfuatilia na kumuona SALAMEH akiwa anatoka katika ukumbi wa sinema huku akiongozana na mwanamke ambaye kutokana na data walizokuwa nazo Mossad, mwanamke huyo alifanania na mpenzi wa SALAMEH.

Majasusi wale waliwafuatilia na huku wakiwa njiani, walimvamia SALAMEH na kummiminia risasi, Kuja kushtuka lahaulaaa..! mtu waliyemuua hakuwa SALAMEH ila mtu aliyefanania naye kwa karibu sana. Mtu huyo alikuwa ni raia wa Morocco ambaye alikuwa mhudumu wa mgahawa katika moja ya migahawa nchini humo. Aliuliwa mbele ya mkewe ambaye alikuwa mjamzito kwa kipindi hicho.

download (1).jpg

Ali Hassan salameh katikati akiwa na Yaseer Arafat kulia.

HARARI na timu zake walifanikiwa kutoroka lakini mamlaka ya kipolisi ya falme za Norway ilifanikiwa kuwatia korokoroni maafisa sita wa Mossad wakishukiwa kuhusika na mauaji ya mtu ambaye alidhaniwa ni Salameh. Kwa haraka Bi MEIR alimpigia simu HARARI na kumtaka arudi haraka nchini Israel kwani tukio lile lililoshindwa liliibua malalamiko mbalimbali toka pande zote za dunia.

Hakuishia hapo, Bi MEIR aliwapigia simu maafisa wote wa Mossad waliokuwa wametawanyika duniani kote kuwataka warudi nyumbani, hii ilipelekea kukoma kwa mauaji hayo ya malipizi toka pande zote za dunia. Bi MEIR alibaki madarakani mpaka mwaka 1974 ambapo alipokelewa kijiti cha uwaziri mkuu na YITZHAK RABIN.

Kufikia mwaka 1978, Bi MEIR aliaga dunia kwa natural death. Mamia ya waisrael walishiriki mazishi yake kwa majonzi makubwa kwani walimchukulia Bi MEIR kama mama wa taifa la Israel. Pamoja na kufariki kwake, kazi yake ya kulipa kisasi kwa wote waliohusika na tukio la Munic haikukoma. Mwaka 1979 baada ya dunia kuanza kusahau tukio lililofeli la Norway, Mossad walijipanga upya kuendeleza kulipiza kisasi kwa wale waliobaki katika list chini ya uongozi wa Bw. RABIN.

Safari hii mlengwa mkubwa alikuwa ni SALAMEH ambaye alikuwa amefanikiwa kuukwepa mkono wa kisasi wa mossad kwa miaka mingi. SALAMEH tofauti raia wengi wa jamii ya kiarabu, alikuwa kiishi maisha ya kifahari na anasa sana. Huku akipenda sana wanawake, na kuwabadilisha kama nguo.

Alifanikiwa kumuoa mwanadada aliyeshinda taji miss Universe kwa mwaka 1971 ambaye alikuwa raia wa Lebanon. Wengi waliibua minong'ono jinsi maisha ya SALAMEH yalivyokuwa ya kifahari na kufikia hata kuhoji anapopata pesa za kuponda raha kwa kiasi hicho. Kwa taarifa zisizo kuwa rasmi kwa kipindi hicho, zilimuhusisha SALAMEH na Shirika la Ujasusi la Marekani(CIA).

Ilisemekana CIA ndiyo waliokuwa nyuma ya SALAMEH kwa kumfadhili pesa na mahitaji mengine huku yeye akiwafanyia kazi ya ushushushu Wamarekani katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kama malipo ya ufadhili wanachomlipa. Kutokana na maisha ya SALAMEH yalivyokuwa, Mossad waliandaa mpango kabambe wa kumnasa. Wakati huu wakitumia udhaifu wake mkubwa nao si mwengine bali udhaifu wake wa kupenda wanawake.

Mossad walimuandalia SALAMEH kile kinachojulikana kama HONEY TRAP katika ulimwengu wa kijasusi. Mossad walimuandaa mwanamke jasusi na mrembo haswa kwa ajili ya kukamilisha mpango wa kumuua SALAMEH. Pamoja na kumuoa mlimbwende huyo wa miss universe, SALAMEH aliendelea kuwa na michepuko ya nje.

Alikuwa anapendelea sana kwenda katika beach za Beirut. Ni katika beach hizo ndipo alipokutana na mwanadada aliyejulikana kama ERICA CHAMBERS, Baada ya kumtongoza na kuwa naye katika mahusiano. Bi CHAMBERS alikuwa na lengo moja tuu. Kufuatilia nyendo za SALAMEH na kuripoti Tel Aviv juu ya nyendo hizo, hii ilikuwa ni tofauti na mawazo ya SALAMEH, kwani alimchukulia Bi CHAMBERS kama kimada wake.

Baada ya muda kupita SALAMEH kuwa katika mahusiano ya ukimada na Bi CHAMBERS, siku moja Bi CHAMBERS alitoa taarifa juu ya msafara wa SALAMEH kuja kumtembelea alipokuwa akiishi. Hii ilifanya Mossad kukodi gari na kulijaza milipuko kisha kulipaki nje ya alipokuwa akiishi Bi CHAMBERS.

SALAMEH alipowasili kwa huyo kimada wake akiwa katika harakati za kupaki gari alilokuja nalo, ghafla mlipuko mkubwa ulitokea na kupelekea watu wanne kufariki dunia papo hapo. Mmoja wa watu hao alikuwa ni ALI HASSAN SALAMEH. Huo ndio ukawa mwisho wake na juhudi zake za kuukimbia mkono wa Mossad kwa takribani miaka 8 ulifika ukomo siku hiyo.

Mpaka leo haifahamiki wazi, listi ya COMITEE X ilikuwa na walengwa wangapi, Ila tuu Waisrael wanafurahia na kusherehekea mpango wa kisasi juu ya wale waliohusika na mauaji ya Munich na kufanya sera hiyo iliyoasisiwa na Bi GOLDE MEIR kuendelea kuishi.

Mwisho

 
Imenikumbusha ASSASINER mmoja kwenye BIBLIA, kitabu cha "WAAMUZI 3:12-26" anaiwa EHUDI. Dah! Mbinu aliyotumia kumuua Mfalme Egloni ni hatari ...

Hawa jamaa wana kipaji hicho tangu enzi hizo.

Hii operation ya kulipa kisasi cha Munich inajulikana kama "WRATH OF GOD."

Anyways, nisimalize uhondo; Nasubiria umalizie namna walivyolipa kisasi ...
 
Uwe hata unaiga hekima japo nusu za mkuu The Bold, yeye huwa hana haya mambo ya kijinga eti "Itaendelea" kwani umeambiwa JF ina limit ya maneno??!!

Shukrani mkuu, kwa kuiita nililofanya kuwa ni jambo la kijinga. Hapo hapo unataka niwe na hekima za the bold wakati wewe mwenyewe umekosa hekima. Nimewaahidi kuwa nipo katika majukumu mengine now, but nimewaahidi kuwa nikipata wasaa nitaendelea na simulizi. Kumbuka kuna tamthiliya (series) na movie (filamu). Usilazimishe anavyofanya the bold nami nifanye vivyo hivyo kwani kila mmoja ana majukumu yake na ratiba zake. isitoshe hata The bold kama nawe ni mfuatiliaji wa the bold, kuna visa huwa anaweka nusu na kuja kumalizia baadae. Hii yote ni kutokana na ratiba kubana.

ila tuu kama ahadi yangu inavyosema, Habari hii itaendelea jioni. kwa sasa nina majukumu mengine, na sitoweza kutulia na kuandika kisa hiki kwani uandishi wa habari kama hizi inapaswa uufanye ukiwa umetulia akili ili msomaji anayekuja kukisoma kisa apate mtiririko mzuri na kukielewa kisa vyema.

Yote kwa yote, Amani. Tukutane jioni katika muendelezo wa hiki kisa. Tupo pamoja, Amani itawale.
 
Shukrani mkuu, kwa kuiita nililofanya kuwa ni jambo la kijinga. Hapo hapo unataka niwe na hekima za the bold wakati wewe mwenyewe umekosa hekima. Nimewaahidi kuwa nipo katika majukumu mengine now, but nimewaahidi kuwa nikipata wasaa nitaendelea na simulizi. Kumbuka kuna tamthiliya (series) na movie (filamu). Usilazimishe anavyofanya the bold nami nifanye vivyo hivyo kwani kila mmoja ana majukumu yake na ratiba zake. isitoshe hata The bold kama nawe ni mfuatiliaji wa the bold, kuna visa huwa anaweka nusu na kuja kumalizia baadae. Hii yote ni kutokana na ratiba kubana.

ila tuu kama ahadi yangu inavyosema, Habari hii itaendelea jioni. kwa sasa nina majukumu mengine, na sitoweza kutulia na kuandika kisa hiki kwani uandishi wa habari kama hizi inapaswa uufanye ukiwa umetulia akili ili msomaji anayekuja kukisoma kisa apate mtiririko mzuri na kukielewa kisa vyema.

Yote kwa yote, Amani. Tukutane jioni katika muendelezo wa hiki kisa. Tupo pamoja, Amani itawale.
Sawa mkuu ila kwa ushauri, story kama hizi unaweza kuziandaa taratibu kwenye Microsoft word ukimaliza unaicopy na kupest huku yote watu tunaburidika, hizi peace meal huwa zinapunguza ladha ya story, any way kazi njema mkuu ngoja nisubiri hiyo jioni.
 
Haya mambo ya itaendelea ni ya kizamani mkuu, kama unasimulizi yako unajipanga unaileta yote imekamilika.
[HASHTAG]#Chaichungu[/HASHTAG] muaaisi wa itaendelea.
 
Haya mambo ya itaendelea ni ya kizamani mkuu, kama unasimulizi yako unajipanga unaileta yote imekamilika.
[HASHTAG]#Chaichungu[/HASHTAG] muaaisi wa itaendelea.

kama mambo ya itaendelea ni ya kizamani kama unavyosema wewe, Leo hii kusingekuwa na tamthiliya/TV series mbalimbali zinazorushwa kila leo huku ya leo ikiwa ni muendelezo wa ilipoishia jana.
 
31 Reactions
Reply
Back
Top Bottom