Mossad: Nguzo imara nyuma ya ustawi wa taifa la ISRAEL dhidi ya hila za SYRIA.

Wanatumia jina Israel lakini wale ni wahuni toka Germany Russia France na Eastern Europe.Was Ethiopia wanadai wao wanaundugu nao lakini wanabaguliwa.Hawa jamaa ni waporaji kama Morocco kwa Saharawi
Wa Ethiopia wenye asili ya ujudaism wanabaguliwa hatari huko Israel kuanzia mashuleni, pia huko Israel wanabaguana wenyewe kwa wenyewe hata wayahudi wa nje wakienda Israel full ubaguzi.
 
Huwa nasikia raha sana nikiona mwanamke active kama wewe ambaye unapenda kuulisha ubongo wako vitu vigumu.

Hakika wanawake wote mngekuwa hivi maisha yangekuwa rahisi sana, maana tatizo la wanawake wenye hard disc ambayo imekuwa formatted na Shigongo understanding ni zero kabisa kwao.
Matola Mimi napenda kujifunza kila siku na kujisomea mambo mbali mbali tofauti, hali hii imenifanya nielewe mambo mengi muhimu.
Wanawake wengi huwa hawapendi kujishughulisha naona wameridhika na mambo simple sana hata wakikaa na wenzi wao huwa hawana wazo jipya LA ku contribute kwenye daily life. To me life is a learning process and I started when I was in primary na hicho ki tabia nimekiendeleza mno.
 
Wa Ethiopia wenye asili ya ujudaism wanabaguliwa hatari huko Israel kuanzia mashuleni, pia huko Israel wanabaguana wenyewe kwa wenyewe hata wayahudi wa nje wakienda Israel full ubaguzi.
Hiyo yako ni Topic mpya hapa Complex alikuwa anajaribu kuonyesha UMAHILI wa Mossad ktk Kazi zao,,
Wew unaleta Udini wako kwenye huu UZI mtam .

Hatuongelei Ubaguzi hapa tunadadavua Umahili wa hawa watu Taifa la Mungu YEHOVA katka Kazi za mikono yao.
 
Hiyo yako ni Topic mpya hapa Complex alikuwa anajaribu kuonyesha UMAHILI wa Mossad ktk Kazi zao,,
Wew unaleta Udini wako kwenye huu UZI mtam .

Hatuongelei Ubaguzi hapa tunadadavua Umahili wa hawa watu Taifa la Mungu YEHOVA katka Kazi za mikono yao.
Udini uko wapi? Au wewe ndio wale vipofu wanaodhani Israeli dini ya kikristo ina waumini wengi?

Kwa taarifa yako Population ya Waisrael waislamu ni wengi kuliko wakristo.

Usivamie vitu usivyo na ufahamu navyo
 
Boss, Lengo la hii habari si hilo ulilokuja nalo hapa. Hii habari ina lengo la kutoa taarifa kwa uma, na kuburudisha wale wote ambao ni wapenzi wa simulizi za kweli kijasusi ambazo zimepata kutokea katika dunia hii toka kuumbwa kwake. Kwa ulichokiandika hapa, ni vyema ukaenda kuanzisha uzi wako ambao unaelezea hayo uliyoyaandika kwa kina.


Kwani kuna si hata mimi nimeelezea pia wanachokifanya Mosad Dunia hii kwenye ujasi wao, kwamba wanawadunga sindano ya kuondoa kizazi Watu weusi kutoka wenye asili ya Ethiopia, hawataki kizazi cheusi kimee Israeli!
 
Matola Mimi napenda kujifunza kila siku na kujisomea mambo mbali mbali tofauti, hali hii imenifanya nielewe mambo mengi muhimu.
Wanawake wengi huwa hawapendi kujishughulisha naona wameridhika na mambo simple sana hata wakikaa na wenzi wao huwa hawana wazo jipya LA ku contribute kwenye daily life. To me life is a learning process and I started when I was in primary na hicho ki tabia nimekiendeleza mno.
Keep on, akupataye wewe kwa hakika atakuwa amepata mke mwema kabisa, hata muda ukiamuwa kupitia udaku wa Shigongo unakuwa na upeo wa kufilter mambo na kudigest.

This is it.
 
Unadhani level ya uelewa ingekuwa sawa shuleni wengine mngepata zero?

Sasa hapo ameandika kwa kiswahili hujaelewa kwamba Wasyria walifia North Korea kwenye mlipuko na ikatumwa ndege ya Syria kuirudisha miili nyumbani, nini hakieleweki hapo?

Kaka afadhali umueleweshe wewe, maana nimetumia muda mwingi sana kuiandika katika kiswahili kinachoeleweka kwa urahisi, lakini kumbe kuna ambao bado hawajaeelewa kiswahili kilichoandikwa.
 
Usisahau pia Mossad hata wewe watakutoa kizazi siku ukikanyaga Israeli, kama wanavyowafanyia watu weusi wote wenye asili ya Afrika waishio Israeli, na Waisraeli wanatuchukia sisi watu weusi zaidi kuliko binadamu yoyote yule, hivyo usijidaganye ukiona wanapigana na Waarabu ukafikiri wewe wanakupenda, ukiwauliza Waisraeli wachague kati ya Msyria na Muafrika kama mimi na wewe watachagua Msyria, na ndiyo maana hakuna Mwarabu aliyetolewa kizazi Israeli lkn Waafrika wote wamedungwa sindano na Mosad!

Mtu mweusi hana heshima sehemu yoyote ile duniani.
Iwe Ulaya, Amerika au Asia na kibaya zaidi haheshimki hata nyumbani kwake Afrika.
Hao wachina ndiyo hawatupendi kabisa sema tu hawana jinsi.
 
North Korea 2004, Treni ya mizigo ilikuwa ikisafiri katika moja ya miji yake iliyopatikana kaskazini mwa nchi hiyo iliyogubikwa na inayoendelea kugubikwa na usiri mkubwa juu ya mambo yake yanayoendelea nchini humo. Ghafla ukasikika mlipuko mkubwa na wa kishindo kikubwa sana kiasi kwamba kudhaniwa ni tetemeko la ardhi. Mtikisiko ule ulikaribia ukubwa wa 3.2 katika vipimo vya richter, kipimo ambacho hutumika kuelezea ukubwa wa tetemeko la ardhi. Mlipuko na tetemeko lile halikuwa tetemeko la ardhi kama ambavyo ingedhaniwa, Bali ulikuwa ni mlipuko wa hiyo treni ya mizigo iliyokuwa imelipuka na kusababisha madhara kwa takribani watu 3000 waliokuwa maeneo ya karibu na mlipuko huo ulipotokea na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 700. Taarifa toka vyombo vya habari na toka serikali ya nchi hiyo viliripoti kuwa treni ile ilikuwa imebeba Petroli na mlipuko ule ulikuwa umesababishwa na hitilafu katika treni hiyo ambayo ilipelekea mabehewa yaliyokuwa ndani yake kuna petroli kulipuka kwa kishindo.

Katika ulimwengu wa ulinzi na usalama wa mataifa yote duniani na vyombo vyake vya ulinzi na ujasusi, huwa hakuna taarifa kubwa wala ndogo. kwani wanaamini kuwa jambo lolote lile lazima lianzie katika taarifa na mawasiliano, hivyo basi huwezi kupuuza mawasiliano kwani pengine mawasiliano hayo yanaweza kupelekea kupata kile ulichokuwa ukikihitaji. Habari hii ilifuatiliwa kwa ukaribu sana na mashirika ya kijasusi duniani, na shirika lililoonesha kuvutiwa zaidi na tamko la serikali ya korea kaskazini ni shirika la kijasusi la kizayuni, nalo si jingine bali ni lile linalotambulika kwa jina la, Mossad. Mossad kwa ukaribu chini ya mkurugenzi wake wa kipindi hicho aliyejulikana kama MEIR DAGAN, wakaanza kufuatilia tukio hilo kwa ukaribu, na katika kufuatilia kwa ukaribu huko wiki moja baada ya tukio walishangazwa na taarifa za mamlaka ya anga ya nchi yao kuona ndege iliyokuwa ikitoka Syria kwenda korea kaskazini. Kitu ambacho ni nadra sana na ukizingatia hakukuwa na ukaribu huo baina ya nchi hizo mbili(Syria na Korea kaskazini) kitu ambacho kiliongeza shauku ya wao kutaka kufuatilia zaidi. Baada ya hiyo ndege kutua katika uwanja wa ndege nchini Korea kaskazini, waliendelea kushangazwa zaidi na walichokiona uwanjani hapo. Mossad walitaraji kuona ndege ikiwa na misaada ya ama vyakula ama mavazi kwa waathirika wa mlipuko ule, Ila badala yake waliona majeneza yasiyo ya kawaida 12 kwa idadi yake yakipandishwa katika ndege hiyo. Majeneza yale yalikuwa yametengenezwa kwa madini ya risasi(Lead) huku waliokuwa wameyabeba majeneza yale wakiwa wamevalia nguo maalum kama zile ambazo huwa zinavaliwa na wafanyakazi wa viwanda vya nyuklia na kemikali ama wanaanga wanapokwenda anga za mbali.

View attachment 444631

Bw. Meir Dagan, Mossad spy chief 2002–2011


Hili lilimshangaza sana Bw Dagan, Na haikuishia hapo bali wakati wakiendelea kulitafakari hilo waliloliona uwanjani hapo, Dagan alipokea taarifa kuwa ndani ya majeneza yake hakukuwa na raia wa korea kaskazini, bali kulikuwamo na raia wa Syria, taarifa zilienda mbali zaidi kwa kusema kuwa na maiti zile zilikuwa ni za wanasayansi wa kisyria toka katika taasisi ya utafiti wa masuala ya kinyuklia ya siri iliyokuwa chini ya jeshi la syria. Kichwani mwa Bw Dagan kwa maana nyingine ilimaanisha kuwa ndege ya syria ilikuwa imekuja kufuata maiti za raia wake ambao uwezekano mkubwa walikuwamo katika mlipuko ule wa treni. Na hii ikapelekea Dagan kung’amua kuwa taarifa iliyotolewa na serikali ya Korea kaskazini kuwa treni ile ilikuwa imebeba mafuta ya petroli kuwa nayo itakuwa ni ya uongo. Hii ilipelekea Dagan kujiuliza swali ambalo alikosa jibu kwa muda huo, na swali hili halikuwa jingine bali ni “ Je hii inamaanisha Korea kaskazini wanawasaidia serikali ya syria kujenga kiwanda cha kutengeneza silaha za nyuklia.?? ”. Hii ilipelekea mossad kuunda kikosi kwa ajili ya kufuatillia suala hili kwa ukaribu 24/7/365.

London 2016, Miaka miwili baadaye, wakiwa bado wanalifuatilia hili swala la ukaribu, Mossad walipata taarifa za uwepo wa nia ya kusafiri kwa mmoja wa wanasayansi wa ngazi za juu kabisa wa masuala ya nyuklia kuelekea katika jiji la London. Alikuwa amepanga kusafiri peke yake, na hivyo akiwa bado nchini syria akabook kwa jina bandia chumba cha hoteli atakayofikia ambayo ilikuwa ni hoteli iliyojulikana kwa jina la KENSINGTON inayopatikana katika mji wa London. Baada ya kupata taarifa hiyo, bila kupoteza muda Mossad waliona hii ni taarifa tyenye manufaa kwao na wanaweza kuitumia vizuri kupata kile ambacho wamekuwa wakikifuatilia tangu miaka miwili iliyopita. Hii ilipelekea Mossad kuandaa timu tatu za takribani watu kumi kwa ujumla ambao waligawanywa katika makundi matatu. Timu ya kwanza ilijumuisha timu ya wachunguzi (spotters) ambayo ilitumwa katika uwanja wa ndege wa heathrow kwa ajili ya kumtambua na kuthibitisha utuaji wa mwanasayansi huyo pindi atakapotua nchini uingereza. Timu ya pili ilipangwa kwenda kufanya booking katika hoteli ambayo mwanasayansi alikuwa amepanga kufikia, na timu ya tatu ilikuwa kwa ajili ya kuangalia wale wote watakaokuja kumtembelea na kufuatilia nyendo za mwanasayansi huyo pindi atakapokuwa anazunguka katika mitaa ya London. Na timu hizi zilikuwa zimebeba watu wa aina mbili ambao wanapatikana katika nyanja za ujasusi. Miongoni mwa watu 10 wale wa mossad, ndani yake kulikuwa na watu kutoka katika kitengo cha KIDON ( hawa wanasifika kwa uuaji wa kimyakimya na kudungua) na pia kulikuwa na watu toka kitengo cha NEVIOT ( Hawa ni watu wa kuingilia mifumo ya milango, kufuli na kupandikiza visikilizi (bugs))

Baada ya kutua tuu jijini London, Timu ya mossad iliyokuwepo uwanjani hapo ilifanikiwa kumng’amua na kuwapa taarifa timu nyenzake kuwa mwanasayansi huyo amekwishatua. Hivyo kupelekea kwa timu ya pili kuianza kazi yake ya kumfuatilia kila anapokwenda. Kwa bahati alikwenda moja kwa moja mpaka hoteli aliyokuwa amepanga kufikia na baada ya kupaki mizigo yake, aliamua kutoka na kwenda kupata kinywaji katika baa ya karibu kwa jioni ya siku hiyo. Akiwa mwenyewe katika baa hiyo, ghafla alimuona msichana mrembo akiingia peke yake katika baa hiyo huku mrembo yule akionekana mwenye bashasha na furaha alikwenda kuketi karibu na alipokuwa ameketi mwanasayansi yule. Kama wahenga (wahenga wa kisasa) walivyopata kusema kuwa hakuna mkate mgumu mbele ya supu. Mwanasayansi yule alianza kubadilishana maneno mawili matatu na mrembo yule na kujikuta wakiwa katika lindi la maongezi. Alichoshindwa kugundua mwanasayansi yule ni kuwa, mwanamke yule hakuwa pale baa kwa bahati mbaya kama alivyodhania, bali alikuwa ni mmoja wa majasusi wa mossad na alikuwa pale kwa lengo maalumu, nalo si lingine bali ni kumpumbaza mwanaayansi yule huku wenzake toka kikosi cha Neviot wakijaribu kupenya kuingia katika chumba cha mwanasayansi yule kuangalia alichokuwa amekuja nacho na watakachokutana nacho.

Muendelezo..

Wakati bar maongezi yakiwa yamekolea, mossad walishafanikiwa kuingia katika chumba cha hoteli alichokuwa amefikia mwanasayansi yule kwa njia za kufoji security system za vitasa vya hoteli ile. Baada ya kufanikiwa kuingia wakakutana na kompyuta mpakato ya mwansayansi yule ikiwa mezani bila ulinzi wowote. Bila kupoteza muda, waliifungua na kuanza kazi ya kukopi kila kitu kilichokuwamo katika harddisk ya kompyuta ile na wakati huohuo wakitumia internet hawakupoteza muda walituma mjini Tel Aviv, Israel vyote walivyovipata toka katika kompyuta ya mwanasayansi yule, Baada ya kumaliza kutuma taarifa zile, walipandikiza katika kompyuta ile kirusi ambacho kitakuwa kinatuma taarifa kwao pindi tuu watakapokuwa yule mwanasayansi atakapokuwa antumia kompyuta ile, baada ya kumaliza yote hayo, walimuarifu yule mwanadada kule bar kupitia vispika vidogo ambavyo walikuwa wamevitumbukiza ndani wa masikio kasha wakaondoka, huku bar napo yule mwanadada alimuaga yule mwanasayansi na kumuacha solemba kwani kazi waliyokuwa wametumwa kuifanya ilikuwa imekwisha.

Iliwachukua takriban nusu saa kumaliza kukopi kila kilichokuwemo katika kompyuta ile na kukituma makao makuu. Baada ya nyaraka hizo kufika mezani kwa Bw Dagan, kazi ya kuanza kizichambua ikaanza. Miongoni mwa taarifa zile, kulikuwamo na picha ya jengo moja kuukuu ambalo kwa muonekano lilikuwa kwenye ujenzi, huku kukiwa na mtiririko wa picha nyingine zinazoonesha hatuakwa hatua ujenzi wa jingo hilo. Kwa kukadiria jingo lile lilifika takribani futi 150 kwa urefu na mapana huku likiwa na wastani wa futi 70 kwenda juu. Bw Dagan kwa haraka alishindwa kuelewa lilikuwa ni jingo la nini, lakini baada ya kuangalia vyema mtiririko wa picha zile alikuja kugundua picha ile ilikuwa ina ufanano mkubwa na jengo la YONG BYON linalopatikana korea ya kaskazini. Jengo hili la Yong Byon ni jengo ambalo ndani yake tafiti na utengenezaji wa makombora ya nyuklia unafanyika kwa korea ya kaskazini, hivyo ilikuwa ni dhahiri kuwa wasyria walikuwa wanatumia ramani za jengo la YONG BYON kujenga jengo kama hilo nchini mwao. Pia katika picha zile, zilionekana picha za baadhi ya wataalamu wa masuala ya nyuklia wa korea ya kaskazini na Syria wakiwa wamepiga picha za kumbukumbu. Hii ilibu swali alilokuwa akijiuliza Dagan na ilileta picha kuwa North korea wanawasaidia Syria kutengeneza mitambo ya kuchakata na kuunda makombora ya nyuklia.

Bila kupoteza muda Dagan aliiwasilisha taarifa ile kwa waziri mkuu wa kipindi hicho wa Israel Bw EHUD OLMET juu ya tishio hilo lililopiga hodi mlangoni mwao kama taifa. Jibu na maoni toka kwa Olmet kwenda kwa Dagan lilikuwa moja tuu, Kuwa ni dhahiri hicho kiwanda kinatakiwa kikome uundwaji wake. Na namna pekee ya kukiondoa ilikuwa si nyingine bali kukilipua. Lakini kaba ya kutekeleza hilo, Olmet alihitaji kujibiwa baadhi ya maswali na kufahamu baadhi ya mambo toka kwa mossad. Mambo hayo ni:

1. Je kiwanda hicho kimeshaanza kufanya kazi
2. Kiwanda hicho kipo eneo gani la Syria

Hayo yalikuwa ni maswali magumu kujibika, kwani picha walizokuwa nazo toka kwa mwanasayansi wa kisyria zilikuwa ni za miezi 15 iliyopita hivyo ilimaanisha kuwa yawezekana tayari kiwanda kilikuwa kishamalizika kujengwa na katika muda huo ambao walikuwa wanazungumza kilikuwa tayari kimeshaanza kufanya kazi. Hii ilimaanisha kukilipua kungeweza kuleta madhara makubwa kama kingekuwa tayari kimeshaanza kufanya kazi.

Dagan ilibidi aamuru moja ya satellite yao ya mawasiliano ifanye kazi ya kuichunguza Syria toka angani ili kujua ni wapi haswa kiwanda hicho kipo. Baada ya muda waligundua katika mji wa Al-Kabar kulikuwa na mawasiliano ya simu yasiyo ya kawaida toka nchini humo kwenda North korea. Hii iliwafanya waipeleke satellite katika anga la Al Kabar, na satellite ikiwa hapo Al-Kabar ilifanikiwa kuona picha ya jengo sawa na lile waliloliona katika picha walizokuwa nazo. Hii ilitatua swali la pili aliloulizwa Bw. Dagan, kuhusu swali la kwanza Bw Dagan hakuwa na jinsi zaidi ya kutuma watu kwenda kuchunguza kama kiwanda hicho kimeshaanza kazi ama laa. Kwa hili jambo ilibidi awasiliane na kikosi maalum cha jeshi ambacho kimebobea kwa suala la kufanya ujasusi katika nchi hasimu pasipo kutambulika. Hicho kikosi si kingine bali ni SAYERET MATKAL, hiki ni kikosi cha makomamdo wabobezi sawa kabisa na SPETSNAZ wa urusi ama NAVY SEAL ya marekani. Baada ya kuteuliwa watu hao, usiku mmoja wa majira ya kiangazi mwaka 2007 Walipanda helikopta ya kijeshi yenye mlio mdogo na kwenda mpaka Al-Kabar. Walifanikiwa kutua salama na walitua umbali wa kama maili moja hivi toka kiwanda kilipokuwa kasha wakaanza kutembea kwa miguu kuelekea kiwanda kilipo. Wakiwa umbali wa mita chache walikishuhudia kiwanda, kwa macho na wakaanza kutimiza kazi waliyotumwa. Kazi yao ilikuwa ni kukusanya sampuli za udongo na maji maeneo mbalimbali na jirani kabisa na kilipokuwa kiwanda kasha kuvipeleka Tel Aviv maabara kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Walifanya kama walivyoagizwa, wakachukua sampuli hizo na kuanza kutembea sehemu waliyokuwa wametua na kuanza safari ya kurejea Israel usiku huohuo.

Baada ya kuwasilisha sampuli hizo maabara kwa ajili ya uchunguzi, majibu yalitoka kuwa kiwanda hakijaanza kazi na ripoti hii ilipelekwa kwa Bw Olmet. Ilikuwa ni majibu yenye unafuu, kwani zoezi lilokuwa linafuata ni kukilipua kiwanda hicho ili kisiendelee kuwepo na kisianze kazi yake iliyokusudiwa. Hivyo Olmet aliitisha wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama vya Israel ili kujadili ni namna gani watakamilisha zoezi la kulipua hicho kiwanda cha nyuklia. Baada ya kujadili plan kwa kina wakaona watumie ndege za mmarekani za kivita za F16 na F15, na kuamuru ndege 10 na marubani wakae tayari kwa ajili ya shambulizi ambalo hawakuambiwa ni wapi. Hakuna mtu yeyeote miongoni mwa marubani wale wala nje ya wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliofahamu ni wapi haswa zile ndege zitakwenda kushambulia kwani taarifa hiyo ilifanywa siri ya kiwango cha juu sana(top secret). Usiku wa September 6 2007, ndege zile 10 zilitoka katika kambi ya kivita Israel tayari kwa kwenda kufanya shambulio nchini Syria. Walipanga njia ya ndege zile iwe kupitia bahari ya mediterenean, kisha kuingia kuingia Syria kupitia uturuki. Waliwaomba uturuki kutumia anga yao ili kufanikisha wao kuingia Syria. Katika kituo cha kuongoza ndege hizo walikuwemo waziri mkuu na viongozi wote wa ulinzi na usalama wakifuatilia suala hilo kwa karibu moja kwa moja katika television zao. Dakika 10 baada ya kuanza safari, viongozi walijiridhisha ndege zote zilikuwa sawa na hazikuwa na hitilafu yoyote, hivyo wakaziamuru ndege tatu kati ya zile 10 zirudi nyumbani Israel huku zikiacha 7 zikiendelea na safari.

........ inaendelea

CC:
Punainen, MTOTO WA KUKU, scorpnose, Mbimbinho, Daudi Mchambuzi, Mussolin5, the-sniper, MO11, upupuwapwani, Geniveros, Raimundo
Bado?
 
Mtu mweusi hana heshima sehemu yoyote ile duniani.
Iwe Ulaya, Amerika au Asia na kibaya zaidi haheshimki hata nyumbani kwake Afrika.
Hao wachina ndiyo hawatupendi kabisa sema tu hawana jinsi.


Tutaheshika vp kama sisi wenyewe hatujiheshimu wala kujithamini? Angalia uongozi mzima wa chadema wako kwa Mzungu Ulaya kushitaki tena wanakwenda kaanchi kadogo kama Denmark hivyo kwa akili yao wanategemea Mzungu ndiyo aje kutatua matatizo yao, sasa tutaheshika vp?
 
Anzisha thread yako itakuwa vizuri sio kuchafua hali a
Kwani kuna si hata mimi nimeelezea pia wanachokifanya Mosad Dunia hii kwenye ujasi wao, kwamba wanawadunga sindano ya kuondoa kizazi Watu weusi kutoka wenye asili ya Ethiopia, hawataki kizazi cheusi kimee Israeli!
Kwani kuna si hata mimi nimeelezea pia wanachokifanya Mosad Dunia hii kwenye ujasi wao, kwamba wanawadunga sindano ya kuondoa kizazi Watu weusi kutoka wenye asili ya Ethiopia, hawataki kizazi cheusi kimee Israeli!
Anzisha thread yako itakuwa vizuri
 
Anzisha thread yako itakuwa vizuri sio kuchafua hali a
Anzisha thread yako itakuwa vizuri


Hali ya hewa gani niliyochafua? Mada inahusu ujasusi wa Mosad na mimi nimeongezea kwenye huo Ujasusi, kwamba wanawahasi watu weusi huko Israeli, sasa kwa nini unataka nianzishe nyingine wakati hii ipo?
 
Hali ya hewa gani niliyochafua? Mada inahusu ujasusi wa Mosad na mimi nimeongezea kwenye huo Ujasusi, kwamba wanawahasi watu weusi huko Israeli, sasa kwa nini unataka nianzishe nyingine wakati hii ipo?
Anzisha yako yenye uchambuzi yakinifu kaka
 
Hiyo yako ni Topic mpya hapa Complex alikuwa anajaribu kuonyesha UMAHILI wa Mossad ktk Kazi zao,,
Wew unaleta Udini wako kwenye huu UZI mtam .

Hatuongelei Ubaguzi hapa tunadadavua Umahili wa hawa watu Taifa la Mungu YEHOVA katka Kazi za mikono yao.
Uwe unafatilia vizuri comments ndugu Mimi nilimu quote kuna MTU mwingine, kwanini cha ajabu ni nini? Kwanza hata sijaelezea udini hayo ni yako mkuu. Mbona unaumia kuliko mleta mada you need to relax stop complicating some issues. Life is easy.
 
Back
Top Bottom