Moshi: Yaliyojiri Mei Mosi 2017, Rais Magufuli amwaga ajira Elfu 52, madaraja kupanda....

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,789
11,930
Habari wakuu,


KAULIMBIU: UCHUMI WA VIWANDA UZINGATIE KULINDA HAKI NA HESHIMA YA WAFANYAKAZI

Leo ni siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi). Maadhimisho haya kitaifa yanafanyika mkoa wa Kilimanjaro, Wilaya ya Moshi Mjini katika viwanja vya Ushirika.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni mgeni rasmi katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) kitaifa. Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limeandaa sherehe hizi kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).. Pia wapo viongozi wengine wa kitaifa na mkoa wa Kilimajaro.

Kupitia hapa, nitatoa live updates kwa yanayojiri.

Rais TUCTA
- Umma huu unaouona mbele yako unadhihirisha imani kubwa waliyo nayo juu yako.

-Wakati tunaandaa sherehe hizi hatukujua kuwa utakuwa hivi. Umezunguka sehemu mbalimbali lakini hapa umefunika.

Utakapoanza kuongea, utakuwa unaongea na watanzania. Tunaamini TUCTA utatusikiliza.

Miaka yote Serikali haijawahi kuwa hapa mkoa wa Kilimanjaro leo viongozi wote wa serikali wapo mkoa wa Kilimanjaro. Tunaamini yote utakayoongea umma huu wa wafanyakazi utakusikiliza.

Ulituita Ikulu tukakaa na kuzungumzia changamoto na matatizo ya wafanyakazi kwa zaidi ya masaa matatu.

Yapo mengi uliyoahidi kuyazungumzia...
- Ulisema kuhusu kupandishwa madaraja kwa wafanyakazi na tunashukuru umeshashughulikia suala hili.

- Ulituahidi kushughulikia Nyongeza ya mwaka iliyosimama kwa muda mrefu wakati ukirekebisha nchi.

- Ulituahidi kuongeza ajira, Tunashukuru umetangaza ajira zaidi ya 52,000

- Kurejesha jengo letu lililoko Tanga. Tulikwama kwa muda mrefu kulipa deni lakini kwa uwezo wako ndani ya siku tatu tulirejeshewa jengo letu.

Rais wa TUCTA amemaliza na kumkaribisha Rais wa JMT, Dr. Magufuli.

Rais wa JMT, Dr. John Pombe Magufuli
Sijawahi Kuona maadhimisho ya MeiMosi Yaliyofana kama Haya,Mmevunja Record,mmenitia Moyo sana."mapokezi ya leo yamenichanganya kwelikweli ni mapokezi ya aina yake"

Kwakuwa ni mara yangu ya kwanza kufika Kilimanjaro nawashukuru kwa kunipokea na kunipa kura nyingi na kunifanya.

Mei Mosi si kwa ajili ya Tanzania bali duniani kote. Ni siku ya kukumbushana na kutafakari mambo yanayohusu wafanyakazi pamoja na kutatua matatizo yanayowakabili.

Nawapongeza sana wafanyakazi kwa kuadhimisha siku hii muhimu. Pia kuendeleza maendeleo ya Taifa letu. Serikali inawashukuru sana.

Nimesikiliza risala ya katibu Mkuu wa TUCTA. Kama kuna tatizo la kubadilisha sheria za kazi, Spika na Naibu spika wapo hapa.

Nawahakikishia kuwa tunaanza ukurasa mpya. Ndio maana mnaona hii siku ni ya tofauti. Serikali tumeamua kuimarisha maslahi ya wafanyakazi. Na nyie muwe tayari kuchapa kazi.

Wafanyakazi ndio injini ya maendeleo katika taifa lolote kubwa duniani'

Katibu Mkuu wa Tucta kaongea mengi. Mengine ni ya kurekebisha kwa muda mrefe.

Mmeomba kuhusu fao la kazi. Serikali inalifanyia kazi na kuna mchakato unaendelea pindi mfanyakazi anapoacha ajira kabla ya kustaafu basi alipwe sehemu ya mafao.

Kuhusu suala la BIMA, Nawaarifu kuwa serikali inaendelea na utaratibu wa kuanzisha fao la Bima ya ajira na wadau wameshatoa maoni.

Usalama wa kazini (Anaomba aletewe Bango ''Mh. Rais naomba msaada.. Mirathi ya mme wangu sitapata - wasaidizi chukua jina lake).

Uhuru wa wafanyakazi kujiunga na vyama- Hili lishazungumziwa mwaka jana na lipo kwa mujibu wa sheria na hakuna mwajiri aliye juu ya sheria.

Wizara na Taasisi mbalimbali naziagiza kuu kuunda mabaraza ya wafanyakazi. Mpaka sasa kuna mabaraza 478 na bado mabaraza...

Mikataba ya ajira - Hili suala la hiari. Waajiri wote wanatakiwa kutoa mikataba ya ajira makazini. Kinyume chake ni kuvunja sheria.

Kupanda kwa gharama na mfumuko wa bei niwahakikishie kuwa serikali inalishughulikia.

Makato mikopo - Kuna watu wamenufaika na mikopo lakini hawataki kurejesha mikopo hiyo. Hatuwezi kuendelea kuwa tunakopesha na wanapomaliza wanaenda kununua magari na hawataki kurudisha mikopo. Ndio maana tumeweka sheria ili warudishe mikopo haraka.

Serikali inachukua hatua ya kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Serikali ina mapango wa kuboresha na kufufua viwanda. Tukifufua viwanda vijana wetu watapata ajira na TUCTA Itapata wafanyakazi wapya.
Natoa wito kwa wazawa wa kilimanjaro kwa waje wawekeze kwenye mkoa wao kama mzee mengi kwenye Kiwanda cha cocacola.
Hata hivyo kupitia mifuko ya hifadhi ya jamii jumla ya dola za kimarekani milioni 156 zitatumika kujenga viwanda mbalimbali nchini.

Watumishi hewa walikuwa wanatafuna mishahara, wanachukua mikopo. Nilitarajia mwenyekiti wa TUCTA angetoa kauli lakini amepotezea potea kidogo.
Zoezi hili limeenda vizuri na limefikia 98%.

Kuna watumishi wamegushi umri wao wa kustaafu, hawa nao dawa yao tunaichunguza.

Wapo wafanyakazi wenye vyeti feki. Hamna sehemu kwenye sheria za kazi inalazimisha mtu kuajiriwa kwa digrii pekee. Kila mtu anaajiri kuendana na elimu yake.

Katika wafanyakazi 400,035 waliohakikiwa, 9932 wana vyeti feki. Hawa wenye vyeti vya kugushi watupishe.

Nikitaka kupandisha mishahara nitapandisha kwa watumishi kweli, kuna wengine

Nimetoa mpaka kufika tarehe 15 mwezi huu wawe wamejiondoa wenyewe kwenye ajira.
Unapokuwa na watumishi hewa wanakuwa, hawatasita kuandika madai hewa.
Katika kufaniksha kuondoa wafanyakazi hewa na wale wenye vyeti feki.

Kumekuwepo na uhamisho wa walimu ili kupata fedha za uhamisho feki. Sasa niwaombe wafanyakazi, yeyote atakayekuhamisha; Usihame mpaka huyo anayekuhamisha akupe hela za kuhama.

Wengine wanawahamisha kwasababu ya visasi.. Akikuhamisha na cheki yako ya malipo mkononi. Nafikiri wafanyakazi mmenielewa

Tumeamua kununua ndege sita na gharama zetu. Mojawapo ya ndege amabayo inakuja mwaka kesho ina uwezo wa kutoka marekani mpaka KIA. Tunafanya haya kukuza uchumi.

Juzi tumefungua ubalozi wa Israel tumeweza kupata watalii mia nane.

Kwenye bajeti ijayo serikali itaongeza mshahara wa kawaida yaani annual increment.
Nashukuru uongozi wa TUCTA, unapopata viongozi ambao wao ni kutatua matatizo hapo umepata viongozi.

Walimu mlikuwa mnakatwa asilimia mbili ya mshahara ziko wapi?
Mimi sizungumzii, mwaka huu ambayo nitafanya ni haya yaliyoorotheshwa. ni kwenda kutoa promotion kwa wafanyakazi, kupandisha madaraja na tutatoa ajira 52,000.

Sasa ninachowaambia ndugu zangu tuvumiliane,tunazungumzia uchumi wa viwanda uendane na maslahi ya wafanyakazi.
Nawaomba pia tulinde amani na pia tupambane na madawa ya kulevya.
Tutaboresha maslahi ya wafanyakazi.

Sasa ni zamu ya Makamu wa rais, PM na Spika kuwasalimu wana Moshi

Spika: Tutahakikisha sheria zote zinazohusu wafanyakazi zinashughulikiwa kwa haraka.

PM: Wakurugenzi wote wa halmashauri wazingatie agizo la rais la kutowahamisha wafanyakazi bila kuwapa maslahi yao.


Rais Magufuli;
Napenda kuwaambia wana Moshi, Moshi mmevunja rekodi. Ninachowaambia sina cha kuwalipa, nitakachowalipa ni kuwatumikia. Tumepokelewa na Mustahiki Meya, Mbunge na wengine. Na sasa ninajua ya kwamba Moshi mnanipenda.
Najua mlikuwa mnalishwa maneno mengimengi, lakini watanzania wa Moshi na wa maeneo mengine yote wanachohitaji ni maendeleo.

Kwa wafanyakazi wote Tanzania nawaambia; Serikali hii itakuwa mtetezi namba moja ya wafanyakazi.

Tuwe kitu kimoja, kila mmoja akahubiri uzalendo, maendeleo; niwaombe wafanyakazi mkashirikiane na waajiri.
Mimi ningefurahi kwa siku ya Mei mosi tukawape wafanyakazi wote zawadi, najua inawezekana.

Tusibaguane na mimi nina uhakika Mei mosi hii, imekuwa fundisho na natoka hapa ninaenda kukutana na baraza langu la mawaziri kuboresha maslahi ya wafanyakazi.

Mungu awabariki sana.



Hitimisho kwa Ufupi, haya ndo Yaliyojiri Sherehe za Mei Mosi zilizofanyia Moshi Kilimanjaro Kitaifa

=> Mwaka huu tutapandisha madaraja ya kazi pamoja na kuweka nyongeza ya mishahara kuwa sawa na madaraja yake

=> Tunakushukuru Mhe.Rais Magufuli kwa kutekeleza kwa vitendo suala la elimu bure nchini"-Said Meck Sadik

=> Nawashukuru wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa mapokezi waliyonipa wakati nawasili"

=> "Siku ya Wafanyakazi Duniani ni siku muhimu kwa wafanyakazi kutafakari masuala yanayowahusu"

=> "Wafanyakazi ndio injini ya maendeleo katika taifa lolote duniani"-Rais Magufuli

=> "Serikali itaendelea kufanyia kazi changamoto zinazowakabili wafanyakazi"-Rais Magufuli

=> Nawahakikishia wafanyakazi kuwa tunaanza ukurasa mpya kwani serikali tumeamua kwenda mbele"-Rais Magufuli

=> Nawaarifu kuwa serikali inaendelea na utaratibu wa kuanzisha fao la Bima ya Ajira na wadau wameshatoa maoni"Rais Magufuli

=> Serikali inalishughulikia suala la ucheleweshaji wa mafao ili wafanyakazi wanapostaafu waache kuhangaika"-Rais Magufuli

=> Serikali italishughulikia swala la mfumoko wa bei ili kuondokana na ugumu wa maisha"- Rais John Magufuli

=> Vyama vya Wafanyakazi ni mahala pa kazi na sio hiari na visigeuzwe sehemu ya migogoro"-Rais Magufuli

=> "Waajiri wote wanatakiwa watoe mikataba ya ajira kwa wafanyakazi kinyume na hapo ni kuvunja sheria"-Rais Magufuli

=> "Serikali itaendelea kusaini na kuridhia mikataba ya kimataifa wafanyakazi yenye maslahi kwa wafanyakazi"-Rais Magufuli

=> "TUCTA endeleeni kuwaelimisha wafanyakazi ili fedha za bodi ya mikopo ya elimu ya juu ikusanywe kikamilifu - Rais Magufuli

=> "Tumebaini watumishi hewa 19706 waliokuwa wanaisababishia serikali Tsh Bil.230 kwa mwaka katika misharaha tu"-Rais Magufuli

=> Serikali itashughulikia suala la mfumuko wa bei ili kuondokana na ugumu wa maisha"- Rais Magufuli

=> Wapo walio na umri wa kustaafu lakini hawataki hawa nao tutaanza kuwafuatilia,hawana tofauti na watumishi hewa- Rais Magufuli

=> "Nilitaka nisafishe kwanza kabla ya kupandisha mishahara kwa wafanyakazi ili tusiwafaidishe wasiostahili"-Rais Magufuli

=> "Nawaahidi tutatoa ajira 52000 katika sekta mbalimbali baada ya kutoa watumishi hewa na walio na vyeti feki"-Rais Magufuli

=> "Yeyote atakayehamishwa hakuna kuhama mpaka ulipwe hela ya kuhamishwa"-Rais Magufuli

=> "Serikali ya Awamu ta Tano itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na TUCTA na ATE"- Waziri Jenista Mhagama

=> Nawahakikishia wafanyakazi kuwa tunaanza ukurasa mpya kwani Serikali tumeamua kwenda mbele"- Rais Magufuli

=> "Nasisitiza msiwahamishe wafanyakazi kabla hamjawalipa stahili zao"-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

=> "Serikali ya awamu ya tano ipo pamoja na wafanyakazi na haitadharau wala kupuuza maombi yenu"-Rais Magufuli

=> "baada ya kufungua ubalozi Israel tumepata watalii zaidi ya 800 wakiongozwa na Waziri Mkuu mstaafu wa israel"-Rais Magufuli

=> "Niwaahidi wafanyakazi kuanzia bajeti ijayo tutaongeza mishahara kutoka kiwango kilichokaa kwa muda mrefu"-Rais Magufuli

=> "Mwaka huu tutapandisha madaraja ya kazi pamoja na kuweka nyongeza ya mishahara kuwa sawa na madaraja yake"-Rais Magufuli

=> "Kwa sheria zote zitakazoletwa kama miswada tutafanyia kazi kwa wakati ili mambo yenu yaende vizuri"- Spika Job Ndugai

=> Serikali hii itakuwa mtetezi namba moja kwa wafanyakazi"-Rais Magufuli

======

Taarifa ya Ikulu..

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe Mosi Mei, 2017 amesema Serikali ya Awamu ya tano imepanga kufanya nyongeza ya kawaida ya kila mwaka katika mishahara yaani Annual increment, ambayo ilikuwa imesimama kwa muda mrefu ikiwa ni pamoja na promosheni.

Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo katika Sherehe za siku ya Wafanyakazi duniani zilizofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.

Amesema uamuzi wa Serikali wa kuanza kutoa promosheni unatokana na kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa Wafanyakazi hewa zaidi ya wafanyakzi kumi 19,000 walibainika kuwa wafanyakazi hewa.

''Yale mambo yote yaliyokuwa pending ikiwa ni pamoja na promosheni kwa sababu tulishindwa, unaweza kupromoti mfanyakazi hewa hayupo,kwa sababu tungetoa promosheni wakati kuna wafanyakazi 19,000 hewa,maanake tungepromoti na 19,000 na siajabu na watu waliowaandika mule ndio wangeletwa katika mapendkezo ya promosheni'' amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewaonya watumishi ambao wamekuwa wakidanganya umri wa kustaafu ili waendelee kufanya kazi kwa muda mrefu na kuwa siku zao sasa zimekwisha.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amepiga marufuku uhamisho wa Wafanyakazi bila kuwalipa stahili zao kutokana na kuwepo na tabia ya kuwahamisha wafanyakazi bila kuzingatia taratibu hasa za malipo ya uhamisho.

''Sasa niwaombe wafanyakazi yeyote akihamishwa hakuna kuhama mpaka umelipwa pesa ya uhamisho,kuanzia juu mpaka chini,yeyote atakaye kuhamisha mwambie nipe hela yangu ya uhamisho ninapoenda akishindwa usihame kaa hapohapo ufanye kazi'' Amesema Rais Magufuli.

Amesema viongozi wengine wamekuwa wakiwahamisha wafanyakazi kwa maslahi binafsi au visasi kutokana na maendeleo wanayowapata wafanyakzi

Rais Mgufuli amewahakikishia wafanyakazi kuwa Serikali ya awamu ya Tano itaendelea kuwajali na kuwa karibu nao katika kutimiza dhana ya utatu ya ushirikiano kati ya Serikali, Wafanyakazi na Waajiri kwa lengo la kuleta maendeleo.

Aidha, Rais Magufuli amewaeleza wafanyakazi mipango mbalimbali anayofanywa na Serikali katika kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege mpya ,ujenzi wa Reli ya kisasa, utoaji elimu bila malipo na uboreshaji wa miundombinu katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Sherehe za Mei Mosi zilizofanyika katika mkoa wa Kilimanjaro pia zimehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai, Mawaziri, Manaibu Mawaziri, Wabunge na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali ambapo kauli mbiu inasema,'' Uchumi wa Viwanda uzingatie kulinda Haki, Maslahi na Heshima ya Mfanyakazi''.


Jaffar Haniu

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Moshi, Kilimanjaro

1 Mei, 2017
 
Meza kuu.jpeg

C-udvxGWsAAmxR7.jpg:large.jpeg
C-ue_-ZXoAARmMY.jpg:large.jpeg
index.jpeg
umati.jpg
1.jpg
2.jpg
3.jpg
 
"Wamehamasishwa vya kutosha" !
Kwanini mpaka wahamasishwe? Mbona zamani watu walikua na hamasa bila hata kuelezwa,kualikwa,wala kuhamasishwa ? ccm imewachosha watanzania walio wengi.kama magufuli atakuepo lazima atadhihaki,atakashifu,au kutukana kabisa watu.jamani sijui mdomo au ulimi wa huyu baba una nini, anapokua katika hadhira ! Eee Mungu,ponya nchi yetu dhidi ya hili ombwe la huu utawala.Amen
 
Hali ya hewa inazuia kabisa sare za watumishi kutokana na kada zao kutokuonekana.
Makoti na masweta vinazuia
 
Maandamano yanakaribia kuanza sasa....

Watumishi na wakazi wengine wa mkoa wa Kilimanjaro wamekusanyika eneo la idara ya maji kwa ajili ya maandamano yakuelekea viwanja vya Chuo kikuu cha Ushirika
 
Ajira nje nje, waliopitiwa na panga vyeti feki kulipwa mafao,kununua hisa ya makampuni,Tanzania ya viwanda,tufanyeni kazi-hakuna mission town
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom