Moshi: Serikali yazuia kufunguliwa kwa baa zinazouza Mbege ili kupunguza maambukizi ya upumuaji

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Halmashauri ya Wilaya ya Moshi imepiga marufuku baa zinazouza mbege kufunguliwa pamoja na kupika chakula kwenye misiba.

Katazo hilo limetolewa leo Ijumaa Machi 5, 2021 na mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Moris Makoi akibainisha kuwa lengo ni kupunguza maambukizi ya magonjwa ya mfumo wa hewa.

Amesema watu husafiri kutoka mikoa mbalimbali na kuingia Moshi kwa ajili ya kushiriki mazishi na kusababisha msongamano, hasa wakati wa kula.

"Tumeshirikiana na viongozi wa dini pamoja na halmashauri ili kudhibiti hali hiyo kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya magonjwa mbalimbali,”

Mwananchi
 
... kwamba tuna Mungu kuliko Yerusalem; kwamba tu watakatifu kuliko Vatican; kwamba Makka wana uovu kuliko sisi Mungu hawasikilizi wao ila sisi!

Iko hivi, Mungu hajakataza wala sio dhambi ku-apply science katika kupambana na maradhi.
Kwani wangapi Mungu kawapa neema nyingi tu na wala hata hawamuabudu ila kawanyima wanaomcha Mungu? Unakuta Kiranga kapewa utajiri ila Mlokole na Sheikh hata kula yao tu ya shida.
 
Labda tuliweke hili sawa, Huyu ndiye aliyezuia wajumbe wa baraza kuvaa barakoa.

Halafu kuna haja Covid-19 kukaa meza moja na serikali ya Tanzania ili kumaliza tofauti zao mapema kwani huu ubishani hauna faida.
Kwenye suala la chanjo shida kubwa ni hawa waliopiga picha hizi wakati wanapokea chanjo za Covid-19 (Wale walioonekana wanapokea chanjo na kuonesha vidole viwili) lakini naamini na watamaliza tofauti zao kama ambavyo Barakoa walikaa meza moja na kumaliza tofauti zilizokuwepo baina yao.
 
Back
Top Bottom