Moshi: Mzee ahukumiwa kwenda jela miaka 20 kwa kusafirisha mirungi

Wababa wasiku hizi 50 mizinga yakufa mtu sasa ukute mwanaye ndiyo anakazi yakuajiriwa ndiyo atakoma, labda huo umri awe mwajiriwa kidogo afadhali siku hizi wababa ni shida sana bora huyo alikuwa anajishughulisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah!
50 kachoka!
Hii sasa ni balaa.
Lakini waweza kuta ni roho ya kubweteka na kudekeza uomba omba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii nchi vyombo vya dola na vinavyohusika na sheria wote wako kimaigizo tu. Bado wapo miaka 40 na kitu. Hiyo biashara ni ya kawaida sana kwa arusha,huwezi kumfunga mzee kama huyo ili uonekane tu unafanya kazi. Hapo ujue ameshawaachia wenye hela wengi tu,wenye kesi kama hizo. Ili tu aonekane yupo kazini imebidi aonyesha mfano kwa huyo mzee. Hicho walichomfanyia kwa huyo mzee,itawatafuna taratibu maisha yao yote
 
Hii nchi vyombo vya dola na vinavyohusika na sheria wote wako kimaigizo tu. Bado wapo miaka 40 na kitu. Hiyo biashara ni ya kawaida sana kwa arusha,huwezi kumfunga mzee kama huyo ili uonekane tu unafanya kazi. Hapo ujue ameshawaachia wenye hela wengi tu,wenye kesi kama hizo. Ili tu aonekane yupo kazini imebidi aonyesha mfano kwa huyo mzee. Hicho walichomfanyia kwa huyo mzee,itawatafuna taratibu maisha yao yote
Mkuu, mimi kwanza nawalaumu waliotunga hii sheria. Huwezi kuweka mirungi kwenye kundi moja na cocaine na heroine! Athari zake ni tofauti. Ndio maana wakati hizo dawa za kulevya hazikuwahi kuhalalishwa, kuna wakati Tanzania mirungi ilikua ni biashara halali kabisa

Ni sawa kusema leo hii mnaharamisha ugoro kwenye sheria zenu halafu hapohapo mnaweka capital punishment! Jamani kumfunga mtu jela miaka 20 ajili ya mirungi ni sheria mbaya, ipelekwe Bungeni ifutwe

Tena kwa taarifa yenu, adhabu ya juu kwa kupatikana na kosa mahakamani la kusafirisha mirungi kilo 50 ni kifungo cha maisha jela!!!!

Sijui kama watu wanaelewa maana yake!!!!? Sheria zetu nyingi ni mbaya na za ukatili kabisa. Kwa watu wanaofanya biashara ya cocaine na heroine ni sawa maana athari zake ni mbaya sana kwa jamii. Lakini sio mirungi
 
Maisha magumu mpaka wazee wameamua liwalo na liwe,
Mzee wa miaka 71 hakua anatunzwa na wanawe? hakua na ndugu?
Tujaribu kuwatunza wazee wetu na kuwapa mahitaji yao,leo hii kama huyo mzee ana watoto wakisikia amehukumiwa kwenda jela miaka 20 bila shaka watajuta kumtelekeza but itakua too late!
Mzee hakuwa na shida huyo wewe , hujasoma hapo anamiliki Toyota Corolla
 
Mzee mwenye umri wa miaka 71, Patrick Malya amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha mirungi, akiwa ni mshtakiwa wa kwanza mwenye umri mkubwa kuhukumiwa kwa kosa la mirungi.

Adhabu hiyo imetolewa wakati Mkoa wa Kilimanjaro, hasa Wilaya za Rombo, Moshi, Hai na Mwanga zikitikiswa kwa biashara ya mirungi inayoingizwa kutoka nchi jirani ya Kenya, kupitia njia za panya zilizopo mpakani katika wilaya hizo.

Katika hukumu ya kesi hiyo, Jaji Emmaculate Banzi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi iliyoketi Moshi, alimwachia huru mke wa mzee huyo, Paulina Mallya (60) kwa kukosekana ushahidi dhidi yake.

Awali upande wa mashtaka ukiongozwa na mawakili Agatha Pima na Nitike Emmanuel kutoka Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS), waliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Machi 20, 2017 katika Kijiji cha Kiboro wilayani Rombo.

Akisoma hukumu hiyo juzi, Jaji Banzi alisema ushahidi uliotolewa na mashahidi sita wa upande wa mashtaka, ulikuwa mzito na haukuacha mashaka dhidi ya mzee Mallya na kuukataa utetezi wake kuwa alijua amebeba mchicha na siyo mirungi.

Kulingana na ushahidi huo, Machi 19, 2017, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agness Hokororo alipata taarifa kutoka kwa raia wema kwamba mzee huyo kwa kutumia gari lake aina ya Toyota Corolla T 344 CAQ amekuwa akisafirisha mirungi.

Mkuu huyo wa wilaya akamwagiza Katibu Tawala wa wilaya (DAS), Abubakar Assenga, akutane na mkuu wa kituo (OCS) cha Wilaya ya Rombo na kupanga namna watakavyoweka mtego utakaofanikisha kukamatwa kwa mtuhumiwa.

Siku iliyofuata maofisa hao wakiwa na polisi wengine wawili, walifika eneo hilo la Kiboro saa 10:30 alfajiri na gari hiyo ilifika na kusimamishwa ambapo mshtakiwa aliamriwa afungue buti ya gari yake ili ikaguliwe ambapo alidai ni mbovu.

Gari hiyo ilipelekwa kituo cha Polisi Rombo ambapo alitafutwa askari wa kikosi cha usalama barabarani ambaye aliifungua buti bila tatizo na kukuta mifuko minne ya sandarusi ikiwa na mirungi yenye uzito wa kilo 83.

Katika utetezi mkewe alikiri mumewe kupakia mizigo njiani ingawa hakufahamu ilikuwa ni mizigo gani, utetezi ambao uliishawishi Mahakama kuwa hakuwa anafahamu jambo hilo hivyo kumwachia huru.

Kwa upande wake, Mallya alijitetea kuwa mzigo huo alipewa na mtu njiani wakati anatoka Rombo kwenda Arusha na alihisi ni mchicha au miche ya miti na alilipwa Sh200,000 za usafiri.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Banzi aliukataa utetezi huo akisema alifahamu alichokuwa amebeba kwa kuwa anakiri kulipwa Sh200, 000 akisema kama ingekuwa ni mchicha fedha hizo ni nyingi kwa mwaka 2017.

Mbali na hoja hiyo, lakini Jaji alisema mshtakiwa alikuwa ametiliwa mashaka muda mrefu kuwa anajihusisha na usafirishaji wa mirungi na hata alipokamatwa na kutakiwa kufungua buti, alitoa visingizio kwa kuwa alijua alichokuwa amebeba.

Jaji Banzi aliagiza pia kutaifishwa na Serikali kwa gari lililotumika kusafirisha dawa hizo.

Hukumu hiyo ni ya kwanza kutolewa kwa mtu mwenye umri mkubwa mkoani Kilimanjaro, ambapo kama hatokata rufaa na kuachiwa huru atatoka gerezani akiwa na umri wa miaka 85 kama atakuwa na tabia njema na kupunguziwa moja ya tatu ya adhabu hiyo.
Mzee anadai mchicha pori

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Nimeishi mji mmoja huko kaskazini aisee bangi na mirungi inalika hadharani na watu hawaogopi na vijana ndio waathirika wakubwa, tena wengi huvutia pembeni ya vituo vya police
 
Mkuu haina mitaa, ina vijiji wala usikatae.

Ibukoni, Mamsera, Keni, Ikuini vyote ni vijiji kama vijiji vingine.
Ulielewa maana yake ama kwakua una uchungu wa kujifungia? Mjinga kweli... unafundisha shule gani we fala kiangalieee. Ugumu wa maisha umekupelekea mpk ukaenda pangiwa ajira vijijini makalio wewe

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Tulia we msheku kikojozi, uambiwe ukweli.

Njoo unipe hiyo mimba kama huwa unakojoa umesimama!!

Hiyo Tarakea yenyewe ni barabarani tu, ukitembea kidogo unaingia mashambani tu huko.
Sasa kama ni vijijini waumia nn? Dada zako na nduguzo wanajua ndo town. Mmezoea kuishi mabandani lazima roho ikupwite. Unafundisha wapi? Ikuini? Ama halmashauri hapo? tutajie kijijini kwako

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
 
Ulielewa maana yake ama kwakua una uchungu wa kujifungia? Mjinga kweli... unafundisha shule gani we fala kiangalieee. Ugumu wa maisha umekupelekea mpk ukaenda pangiwa ajira vijijini makalio wewe

Sent from my SM-G960U using JamiiForums mobile app
Kwahiyo tunakubaliana kuwa huku ni vijijini, chaka pori??

Ona Warombo wenzio asubuhi asubuhi na mipombe isiyoeleweka.👇👇
 

Attachments

  • VID-20211120-WA0002.mp4
    11.3 MB
Conclusion ya kwamba ametekelezwa na watoto wake umeifikia vipi?
Mzee alikuwa msafirishaji maarufu wa mirungi akawekewa mtego.
Alikuwa analipwa .Na anatumia gari lake.Tukio hilo mkuu ni la 2017 .
Alikuwa anajua anafanya nini na alikamatwa na mzigo.
Tumia akili unaposoma comment,elewa comment kabla ya kukurupuka,kuna sehemu nimesema nimefikia conclusion kua ametelekezwa?soma tena comment na uzingatie alama ya kuuliza (?)
 
Back
Top Bottom