Moshi: Mwanamke aliyemfumania mwanamke mwenzake na kumpiga azungumza mazito

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,191
4,103


Joyce Kilia amezungumza na familia ya Vicent (Mwanamme anaedaiwa kufumaniwa na mke wake)

Akizungumza Agnes Vicent Malya( Mfumaniaji) anasema yeye ni mke wa ndoa wa Vicent Malya na wamefanikiwa kupata watoto wawili na mme wake.

Anasema ilikuwa tarehe 18/5/2020 aliondoka asubuhi na mme wake, mme wake alikuwa anaenda mahakani kutoa ushahidi wa kaka kesi ya kaka yake. Anadai waliachana na mme wake vizuri eneo la magereza.

Anadai akiwa sokoni aliambiwa na mmewe kuwa alishafika na mme wake akamwahidi kumtumia 12000 kwa ajili ya mafuta ambayo mkewe alikuwa ameomba na wala haikutumwa hela hiyo wala hawakuwasiliana tena.

Anadai ilipofika saa 12 jioni ndipo alipompigia na kumuuliza kama bado yupo mahakamani na akamjibu kuwa yupo mjini, naye akamwambia mmewe kuwa yeye bado yupo msibani maana alikuwa kaenda msibani, mmewe alimjibu kuwa atakwenda amsubiri arudi ili waondoke wote.

Anadai alimsubiri mmewe bila mafanikio na ndipo alipoamua kuchukua bodaboda na kurudi nyumbani, na ilipofika saa tano usiku alimpigia simu mmewe lakini haikupokelewa mpaka yeye alipoamua kulala bila kumuona mmewe akirudi nyumbani.

Siku ya tarehe 19/05/2020 aliamka na kuendelea na majukumu ya kifamilia na alimpigia mmewe na akapokea kisha kumjibu kuwa ameamka salama.

Baadae alielekea shambani kuchukua mahindi na alifika nyumbani kwa mama mkwe wake na kwenda kuchukua funguo mahali wanapowekaga na hakukuta funguo bali sadolini ya maji ambayo kwa kawaida haikai hapo alipoikuta.

Alimtumia meseji mme wake kumuuliza funguo ipo wapi? Akajibu kuwa ipo kwa dada yake na mlio wa meseji ulisikika ndani ya chumba ambacho yeye mke kasimama dirishani.

Ndipo alipogundua kuwa mme wake yupo ndani ya nyumba hiyo ndipo alipomwambia kuwa kama yupo Boma apokee simu na ndipo alipiga na simu ikaitia humo ndani.

Na baadae alimuuliza wifi yake kama funguo ipo kwake ndipo wifi yake huyo alikwenda eneo la tukio na dada mtu alikana kuwa na funguo hiyo.

Na baada ya hapo waliamua yeye na wifi yake wakaanza kupiga ukunga na ndipo walipochungulia kwenye vitundu vidogo vya dirisha na kumuona aliwa kitandani na mme wake.

Anadai kuwa baada ya wao kupiga ukunga ndipo mmewe alipotoka ndani mbio na kumpush kisha akakimbia, baada ya hapo alimuona mwanamke yule ambae ndie mwizi wa mmewe na kuanza kumpiga.

Anasema kitendo kile sio kizuri alifanya hivyo kwa kuwa alishindwa kuvumilia maumivu ya kuchukuliwa mme na mwanamke ambae kashamuonya mara nyingi kwa swala la kutembea na mmewe.

Mwanaume nae azungumza

Amekiri kuwa mfumaniaji ni mke wake wa ndoa pia mfumaniaji ni mtu ambae walifahamiana sehemu ya kuuzia vinywaji na walikuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Anadai wana uhusiano uliodumu kwa miaka mitano na anadai kuwa alikuwa anatumia gharama kubwa kumhudumia dada yule hata anashindwa kukidhi mahitaji ya familia yake na mpaka biashara za mwanaume huyu ziliyumba kwa sababu ya mwanamke huyu.

Anadai kuwa mwanamke huyu alihamia Mwanza na hivyo Vero alikuwa kaenda kwa Boma muda huo kuoka Mwanza. Na anadai kuwa mwanamke huyo alimkataza kurudi nyumbani na kulazimisha walale wote, na akatoa ushauri wasiende gesti maana ni gharama na akadai hela ya gesti ampe na akashauri waende pale kwenye nyumba ya mama yake.

Anadai ni kweli walifumaniwa na tuhuma za kuwa Vero aliibiwa sh. laki tisa na elfu saba ni uongo kwa kuwa huwezi tembea na hela hiyo ikaibwa na usitoe taarifa polisi.

Anasema anashukuru kwa tukio hilo kutokea kwake ni fundisho ili alirudi kwa familia yake maana dada huyo amechangia kumfilisi na miradi yake yote imekufa na hata hela ya kupanga nyumba hana anaishi kwa shemeji yake.

Amesema anaomba wanaume wenzake wenye tabia kama yake waache Maana sio jambo zuri.

Pia soma
Aliyepigwa kwa kudaiwa kufumaniwa amliza Mkuu wa Mkoa

VIDEO: Fumanizi na kipigo kikali sana
 
Bado anabaki kuwa muhalifu tu. Kujichukulia sheria mikononi!??
 
Kwahiyo show alifanyia kwao mwanaume na mama kakubali mwanaye apigie show hapo
 
Huyo jamaa nimemkubali sana. Amemtetea mke wake wa ndoa na amekubali yaishe. Michepuko ielewe kua mke wa ndoa ana nguvu sana. Ukitaka kujua michepuko haina nguvu, mke akimfumania mume. Mara nyingi tunawaomba msamaha wake zetu.
 
Huyo jamaa nimemkubali sana. Amemtetea mke wake wa ndoa na amekubali yaishe. Michepuko ielewe kua mke wa ndoa ana nguvu sana. Ukitaka kujua michepuko haina nguvu, mke akimfumania mume. Mara nyingi tunawaomba msamaha wake zetu.
Ni kweli, lkn huyo mwanaume hawezi acha umalaya kamwe, kuleteana maradhi ndo kubaya
 
Aisee! Hilo tukio lao litabakia daima kuwa funzo kwetu na kwa mamlaka pia.
 
Wanaendelea Kusimulia Kupenda Vipande Vipande, Sawa Sawa 😁😀😀
Kuacha Ndiyo Mtihani Kwa Wanaume 🙄😏
 
Joyce aibu yake ameacha kufanya shughuli zake kaenda kumtetea malaya !

Mwisho wa siku anaomba hela ya mafuta watu wamchangie!
 
Back
Top Bottom