Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya sekondari ya Aides ya Bomang'ombe, wilaya ya hai ni miongoni mwa watuhumiwa 3 wanaoshikiliwa na polisi kwa tuhuma za kusafirisha kilo 142 za mirungi.
Watuhumiwa hao walikamatwa jana majira ya saa kumi jioni katika eneo la YMCA Moshi, wakiwa na gari ndogo aina ya Nissan XTrail.
Gari lenye usajili wa namba T 512 CXS, rangi nyeusi lililokuwa likielekea Arusha, lilitiliwa shaka na askari doria na waliposimamishwa na kuwafanyia upekuzi, walikutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya.