MOSHI: Mwanafunzi ajiua kutokana na mshtuko wa kifo cha mama yake

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,261
Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Kakoleni wilayani hapa mkoani Kilimanjaro, Khalid Shaban (14),amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali akiwa chumbani kwake

Inadaiwa Shaban amejiua kutokana na mshtuko wa kifo cha mama yake mzazi aliyefariki siku chache zilizopita

Katika tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi lilitokea Novemba 28 mwaka huu, saa 7.00 mchana katika eneo la kata ya Mabogini, Moshi.

Akizungumza na gazeti hii leo (Jumanne) Diwani wa Kata hiyo, Emmanuel Mzava, amesema baada ya mama mzazi wa Mwanafunzi kuanza kuugua mtoto huyo alikata tamaa na kusema kuwa mama yake hataweza kupona tena

Mzava amesema baada ya muda mfupi mama wa kijana huyo alifariki dunia, alipofariki afya ya Shaban ilianza kudhoofika kutokana na kifo cha mama yake

"... Alipoteza matumaini na kwamba hawezi kuendelea tena kuishi bila ya mama yake,"amesema Mzava

Chanzo: Mwananchi
 
jamen tuonyeshe upendo wa kweli kwenye familia zetu,,,tusibaguane tubebane na kusameheane kweli,,,,aliona hana msaada mwingine ila angepata upendo sidhani kama yangetokea,,,.....rajun
Bila shaka alikosa mtu wa kumfariji kwa mazito yaliyompata

Mungu amsamehe..!
 
Very sad. R.I.P
 
jamen tuonyeshe upendo wa kweli kwenye familia zetu,,,tusibaguane tubebane na kusameheane kweli,,,,aliona hana msaada mwingine ila angepata upendo sidhani kama yangetokea,,,.....rajun
Kweli kiongozi,angetokea mwenye upendo kwenye hiyo familia akamfariji kweli kweli asingejinyonga.R.I.P kijana
 
Mwanafunzi wa darasa la sita katika shule ya msingi ya Kaloleni wilayani hapa mkoani Kilimanjaro, Khalid Shaban (14), amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali akiwa chumbani kwake.

Inadaiwa Shaban amejiua kutokana na mshtuko wa kifo cha mama yake mzazi aliyefariki siku chache zilizopita.

Katika tukio hilo lililiovuta hisia za watu wengi lilitokea Novemba 28, mwaka huu, saa 7.00 mchana katika eneo la kata ya Mabogini, Moshi.

Akizungumza na gazeti hili leo (Jumanne), Diwani wa kata hiyo, Emmanuel Mzava amesema baada ya mama mzazi wa mwanafunzi kuanza kuugua mtoto huyo alikata tamaa na kusema kuwa mama yake hataweza kupona tena.

Mzava amesema baada ya muda mfupi mama wa kijana huyo alifariki dunia. Alipofariki afya ya Shaban ilianza kudhoofika kutokana na kifo cha mama yake.

“…Alipoteza matumaini na kwamba hawezi kuendelea tena kuishi bila ya mama yake,”amesema Mzava.

Kaimu Kamanda wa polisi mkoani hapa Koka Moita, amesema mwanafunzi huyo alijinyonga kwa kutumia mkanda wa suruali wa ngozi ambapo aliufunga mkanda huo kwenye dirisha la chumbani kwake na kujinyonga hadi kufa.

“Mpaka sasa hakuna anayejua chanzo cha kujinyonga kwa mwanafunzi huyo wala hakuna ujumbe wowote alioacha, hii imefanya kifo chake kiwe na utata maana hakuna mtu anayejua chochote,”amesema Kaimu Kamanda Moita.

Moita amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mawenzi kwa uchunguzi.

Chanzo: Mwananchi
 
Kumpoteza mama ni pigo kubwa sana duniani, hakuna wakuziba pengo la mama dunia hii.
*poleni sana wafiwa kwa misiba miwili
 
Daaaah very sad.......

Ila kiukweli Mama uwa anauma kuliko mzazi yeyote.......

Yawezeka amejiuliza maswali mengi kuwa ataishi vipi bila mama ukizingatia bado mtoto Mdogo?..........

R.I.P........
 
Mtutukane humu kwenye mitandao, mtupe majina ya ajabu lakini mama ni mama. Hao mnaowaona madada poa wengi wana watoto wanafanya hivyo siyo kupenda ila wameterekezwa na kazi wanazofanya za official hazilipi inabidi waongezee ili walishe watotowao na bibi wa watoto. Siku hizi wanaume hakuna anayemjali mama yake mnawajali mababy na ndugu wa wake zenu ni watoto wa kike tu na do wanatunza familia hivyo mtoto alijua kuwa mwisho wa maisha yake ndo huo.
 
wanaume wana dhambi sana waache tu .MoTO WA MILELE UNAWAHUSU
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom