Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,499
- 9,279
Moshi. Ofisi ya Taifa ya mashtaka nchini Tanzania imewafikisha mahakamani watuhumiwa watatu wakiwemo wanafunzi wawili kwa tuhuma za kuhusika katika matukio ya kuchoma moto mabweni ya shule za sekondari za Uchira na Ebeneza Sango zilizopo Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Novemba 5, 2020 mkurugenzi wa utenganishaji wa shughuli za mashtaka na upelelezi wa ofisi hiyo, Oswald Tibabyekomya amesema walifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi jana na leo.
Amesema katika tukio la uchomaji moto bweni la shule ya sekondari ya wasichana Uchira ofisi hiyo imefungua mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu yanayowahusu washtakiwa wawili ambapo mmoja ni mwanafunzi na mwingine ni mwalimu, Abdallah Ramadhani. Haya hivyo, Tibabyekomya hakutaja majina ya wanafunzi hao.
Amebainisha kuwa katika tukio jingine la kuchoma moto bweni la shule ya Ebeneza Sango, mashtaka yamefunguliwa kwa mwanafunzi wa shule hiyo.
"Kulingana na upelelezi uliofanyika mpaka sasa kichocheo kikubwa cha matukio haya ni mahusiano mabaya na ushawishi wa vikundi rika visivyofaa mashuleni.”