chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,968
Mzalishaji wa pombe kali bandia aina ya Kiroba Original na Konyagi, Jonathan Njamasi (30), jana, alitupwa Gereza la Karanga mjini hapa kuanza kutumikia kifungo cha miaka mitano.
Pombe hizo zilikuwa zikisambazwa katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Singida, Dodoma, Dar es Salaam na Kanda ya Ziwa.
Njamasi alihukumiwa kifungo hicho mwaka jana mbele ya Hakimu Mkazi, Sophia Masati bila kuwapo mahakamani hadi alipokamatwa mkoani Dodoma wiki iliyopita. Wakati Njamasi anayekabiliwa na tuhuma katika mikoa mbalimbali akienda jela, kifungo kingine cha miaka saba kinamsubiri mkoani Singida kwa makosa kama hayo.
Juni 30, 2015 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani humo alihukumiwa kifungo hicho kwa kukutwa na kiwanda bubu cha Kiroba na Konyagi bandia.
Kama ilivyokuwa katika Mahakama ya mjini Moshi, wakati hukumu hiyo ikitolewa hakutokea mahakamani na Mahakama iliamua kutoa hukumu.
Washirika wake watano ambao ni wafanyakazi waliokutwa katika kiwanda hicho bubu eneo la Unyankindi mjini Singida walihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kila mmoja.
Akimsomea hukumu, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa Kilimanjaro, Joachim Tiganga alikataa ombi la mshtakiwa huyo la kutaka kujitetea upya.
Mshtakiwa alitoa ombi hilo baada ya kuelezwa anatakiwa akatumikie kifungo alichohukumiwa akiwa hayupo kortini na kwamba, alishapewa nafasi ya kujitetea kabla ya kuingia mitini.
Hakimu Tiganga alimweleza kuwa kabla ya kuingia mitini, alitoa utetezi wake na ndipo Mahakama ikapanga tarehe ya hukumu, hivyo hukumu hiyo imezingatia utetezi na ushahidi wa Jamhuri.
Hakimu alisema baada ya kutoroka, Mahakama ilitoa hati ya kumkamata ili atumikie kifungo chake na kwamba, wadhamini wake walitakiwa kufika mahakamani kujieleza kwa nini wasishtakiwe.