Uchaguzi 2020 Moshi mjini: Mkutano wa Kampeni wa mgombea Urais kupitia CCM, Dkt. Magufuli. Asema atafufua viwanda vilivyolala

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,909
51,904
MAGUFULI: Nawashukuru viongozi wa dini kwa Dua na Sala zao. Ninajua wagombe wenzangu wa ubunge wameeleza yote na mikakati mbalimbali ya chama cha mapinduzi kama ilivyofafanuliwa kwenye Ilani.

54700F52-D1C6-4B4F-BE14-441975E004A4.jpeg


Nchi yetu imebarikiwa kwa mambo mengi sana, binadamu wa kwanza, mti mrefu, mlima mrefu kuliko yote Afrika, madini ya Tanzanite, Tanzania ni nchi ya pili kuwa na mifugo wengi. ya tatu kwa kuvumbua kiwango kikubwa cha gesi asili na nne kwa kuzalisha dhahabu barani Afrika.

186FA85C-EB52-432A-B9B4-4E0B62BF73A2.jpeg


Zaidi ya kilomita 1422 tunapakana na bahari, ina maziwa, mito, misitu, ina vitu mbalimbali. Nchi hii imebarikiwa sana na Mungu. Nchi yetu ni tajiri, miaka mitano iliyopita tumedhihirisha sisi sio masikini, sisi ni matajiri. Tumefanya mambo mengi makubwa tena kwa nguvu zetu wenyewe, najua mengi mnayafahamu.

Katika kipindi cha miaka mitano tuliweza kuanza kukusanya kodi kwa mwezi kutoka bilioni 850 mpaka trilioni 1.5 na kuna baadhi ya miezi tumefika trilioni 1.6. Tumeweza kujenga vituo vya afya, zahanati, kupeleka umeme kwenye vijiji. Kwa kudhihirisha Tanzania ni tajiri tumeanzisha miradi mikubwa. Tumejenga barabara za lami zaidi ya kilomita 3,500 na tunaendelea kujenga kilomita 2,500. Ndege 11, kununua na kujenga radar katika viwanja viwanja vyetu vikubwa kwa kutumia fedha zetu. Tumeanzisha mradi wa kujenga reli ya umeme, treni ambazo zinatumika Ulaya. Ninaweza kutaja miradi mingi langi lengo ni kuwathibitishia wanamoshi tuko pazuri na tunaenda vizuri.

Tumebarikiwa kuwa na nchi tajiri, kinachohitajika ni kupata kiongozi atakaeweza kuutumia utajiri huu kwa manufaa ya watanzania wote. Na mimi naamini hiyo kazi inanifa kwa sababu nimeonesha katika miaka mitano iliyopita. Mimi naamini kazi hiyo inawafaa wabunge wa CCM, madiwani wa CCM kwa sababu tumeiandaa vizuri katika ilani ya uchaguzi.

Lengo kubwa la kushusha bei ya umeme, tunataka tuwe na viwanda vingi. Tunataka viwanda vilivyolala tuvifufue vyote na kwa hapa Kilimanjaro, Moshi tumeanza, palikuwa na kiwanda cha ngozi nafikiri Karanga kilichokuwa chini ya Magereza.

Leo ukienda kwenye kiwanda hicho utafikiri umefika Ulaya, kitakuwa kinatengeneza pea ya viatu kwa mwaka milioni 1.2, bado hujaweka mikufu, mtaitaje ile? Mikoba, unajua sijamnunulia mke wangu mkoba tangu nimuoe kwa hiyo msishangae nikisahau, kwa hiyo mikoba, mikanda na vitu vingine vitaanza kutengenezwa hapa.

Palitokea ugonjwa wa korona dunia nzima, watu wamekufa maelfu tukaambiwa Afrika maiti zitakuwa zinaokotwa barabarani. Katika mtihani mkubwa nilioupata ulikuwa ni huo katika uongozi wangu.

===============

 
Kampuni za mabasi za Mtei, Machame, Lim safari na Costline zimekesha zinasomba watu kutoka Simanjiro, Mwanga, Hai, Siha, Rombo, Same na Arusha.
Wapongeze kwa kupiga pesa wewe kweli mpinzani hutaki wapate pesa? upinzani ,mna roho mbaya.Wafanyabiashara wa mabasi msiwape kura kabisa upinzani mnawaona mkipiga pesa kwao nongwa!!!
 
Kuanzia himo ni shughuli tupu ni kijani tu na uwanaja umefulika, sisi hatubabaishi.
Najua utanuna ila hakuna namna.

Sawa ila tunawakumbusha baada ya kumaliza msisahau kuwarudisha kwenye malori raia mlipowatoa ,pia mfidie muda mliowapotezea wanafunzi na walimu kwenda kumsikiliza meko inabidi jmos wanafunzi wasome kufidia muda mliowapotezea kwenda kujaza watu uwanjani.
 
Sawa ila tunawakumbusha baada ya kumaliza msisahau kuwarudisha kwenye malori raia mlipowatoa ,pia mfidie muda mliowapotezea wanafunzi na walimu kwenda kumsikiliza meko inabidi jmos wanafunzi wasome kufidia muda mliowapotezea kwenda kujaza watu uwanjani.
Jibu lako wiki ijayo tu wala sio mbali
mpungue jamii forums ibakie watu wachache baada ya tarehe hiyo tunajua mtatokomea gizani
 
Kampuni za mabasi za Mtei, Machame, Lim safari na Costline zimekesha zinasomba watu kutoka Simanjiro, Mwanga, Hai, Siha, Rombo, Same na Arusha.
Lakini ni juzi tu ulipokuwa ukisema, kanda hiyo haidanganyiki!!

Vipi Leo, kunabakora zilipita majumbani kwenu kulazimisha watu wapande hayo mabasi?

October 28 is only next week, after which JPM will be sworn in again at Mkapa Stadium
 
Back
Top Bottom