Moshi: Mjane mwenye watoto wanne atupwa jela maisha kwa kosa la kusafirisha mirungi

mchwa mpaka

Member
Nov 18, 2009
35
70
NEWS UPDATES
Mwanamke mwingine mkazi wa Kiboriloni katika Manispaa ya Moshi,Sophia Kimaro (28) amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kusafirisha kilo 12:5 za Mirungi, kosa alilolitenda tarehe 4.12.2014. Alikamatwa eneo la Njoro ya Dobi Moshi akisafirisha mirungi kwenda kuiuza. Hukumu imetolewa na Jaji Amour Khamis akisema ushahidi wa mashahidi 11 unethibitisha shitaka hilo. Hukumu hiyo imekuja siku chache tu baada ya mjane mwenye watoto wanne naye kufungwa maisha kwa kosa kama hilo Jumanne ya wiki iliyopita.

REFERENCE (SOMA HII HAPA CHINI)

Mwanamke mmoja mkazi wa mtaa wa Bondeni katika Manispaa ya Moshi,Fatuma Mushi mwenye watoto wanne wanaomtegemea, amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kusafirisha Mirungi.

Pamoja na mwanamke huyo, wamo vijana wawili Rashid Rajabu (23) na Hemed Bakari (25) ambao wamefungwa kifungo hicho cha maisha katika hukumu iliyosomwa na Jaji Amour Khamisi juzi mjini Moshi.
 
Dada Fatuma ni wa Arusha mtaa wa Bondeni sema kesi ilikua Moshi nilisikia yupo jela ishu hiyo aisee hatari sana kwa kweli...
 
Nakumbuka nilishawahi kupigwa laki kwa kesi ya kukutwa na picha tu za hio mirungi, nilikuwa na wana wanachanja wakapiga picha tukiwa geto flani.

The next day nikakumbana na wazee wa ngwasuma wakanityt wakaanza kupekua simu yangu na kukuta zile picha nikiwemo. Walikomaa niseme ile mirax nani ame supply nikawakataa maana ilikuwa msala af kipindi hiko napiga 3rd year wakaniambia tunakupeleka central na ushahidi upo so kwa huu msala huchomoki. Wakanirushia kwenye Cruiser lao.

Tukazozana we mwisho wakataka 200, walikuwa kama mtu 9 hivi wako full gwamba wana mikwasa kama yote nikaona nikifurukuta naweza nikapamba magazeti ya kesho. Nkawamegea 100 wakanitema ila nilipiga nao doria toka saa 5 mpaka saa 11 hivi jioni. Hio kitu siwezi sahau ilinitia stress sana.
 
Aisee, pole sana.
 
Asilie lie hapa eti kwakuwa ni mjane,
Je hakujua kuwa ni kosa kisheria?
Kwanini asingefanya kazi yoyote halali?
 
Back
Top Bottom