Moshi: Madiwani wa CCM wakataa 'mpango wa Madiwani wa CHADEMA' kutaka kununulia Madiwani wote Ipad

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameiomba serikali kuingilia kati na kuzuia matumizi ya zaidi ya Sh milioni 104 zinazotarajiwa kununua Ipad za madiwani.

Wameomba fedha hizo zisinunue Ipad kama ilivyopangwa na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na badala yake zitumike kukarabati miundombinu ya barabara kwenye vijiji na kata za halmashauri hiyo.

Diwani wa Kata ya Okaoni, Moris Makoyi (CCM), alisema fedha hizo zilipangwa zitumike kukarabati barabara baada ya kipindi cha mvua za masika kumalizika, lakini madiwani wa Chadema na Mwenyekiti wa Halmashauri, Michael Kilawila, wameamua zitumike kununua Ipad za madiwani na baadhi ya wataalam.

“Hii ni rushwa kwa sababu wanakaribia kumaliza muda wao, vyoo vya wanafunzi mashuleni vimeanguka, zahanati hazina umeme, wakinamama wanashindwa kwenda kujifungua na wagonjwa wanafariki njiani kwa sababu barabara ni mbovu halafu wanataka kununua Ipad,” alisema.

Alisema kipaumbele ni wananchi kupata maendeleo badala ya viongozi kujinufaisha wenyewe kwa vitu ambavyo havina msingi na kudai kuwa, mwenyekiti wa halmashauri hiyo amekuwa akipeleka miradi mingi ya maendeleo kwenye kata za Chadema.

Diwani wa Kata ya Kahe Mashariki, Kamili Mmbando (CCM), aliomba serikali izuie matumizi ya fedha hizo akisema ni ufisadi ndani ya halmashauri kwani zikinunuliwa Ipad zitatumika zaidi kwa matumizi binafsi.

Diwani wa Kilema Kaskazini, Anna Lyimo (CCM), aliwataka madiwani wakumbuke kuwa wamechaguliwa kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi hivyo hawatakiwi kutumia vibaya fedha za umma bali zitumike kuleta maendeleo kwenye kata.

Akijibu hoja za madiwani hao wa CCM, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi, Kilawila alisema halmashauri hiyo inaendeshwa bila kuangalia itikadi za vyama na kwamba waliamua kununua Ipad kwa ajili ya kupunguza matumizi ya kutoa nakala kivuli na usafiri wa kusambaza nyaraka za madiwani kwenye kata 32.

“Tuliamua kuingia kwenye mfumo wa dijitali kwa sababu madiwani na wataalam wakiwa na Ipad itapunguza gharama za kutumia makaratasi na kutoa nakala kivuli na hatuna sababu za kupinga kwa sababu halmashauri nyingine zimefanya hivyo,” alisema.
 
Milioni mia haziwezi kumaliza matatizo yote katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro! Kama kujenga kilometa moja ya lami ni around Bilioni 1.6,hizo pesa hata zikipelewa huko 'hazitofanya chochote'... Nako wajanja watazipiga kwenye kununulia Diesel ya kuendeshea 'vijiko' vya halmashauri.

Kama pesa zipo na kuna uhitaji wa madiwani kununuliwa Ipad, sioni kwa nini wasinunuliwe. Nao ni watumishi wa umma, wanafanya kazi kwa kujitolea bila kulipwa mshahara. Ipad ya milioni moja, gawanya kwa miezi 60 watakayofanya kazi ya udiwani ni sawa na Tsh 16,000 kwa mwezi provided hiyo IPAD moja inagharimu Tsh milioni moja.

Je kumlipa mtu 'mshahara' wa Tsh 16,000 kwa mwezi is too much to ask? I dont think so...
Kama tunaona uchungu kuwalipa madiwani hizo milioni mia, basi yatupasa tuone uchungu zaidi kugharamia zaidi ya Bilioni mia tano kwa mwezi kuwalipa watumishi wengine wa umma walioko kwenye payroll.
 
Milioni mia haziwezi kumaliza matatizo yote katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro! Kama kujenga kilometa moja ya lami ni around Bilioni 1.6,hizo pesa hata zikipelewa huko 'hazitofanya chochote'... Nako wajanja watazipiga kwenye kununulia Diesel ya kuendeshea 'vijiko' vya halmashauri.
Kama pesa zipo na kuna uhitaji wa madiwani kununuliwa Ipad, sioni kwa nini wasinunuliwe. Nao ni watumishi wa umma, wanafanya kazi kwa kujitolea bila kulipwa mshahara. Ipad ya milioni moja, gawanya kwa miezi 60 watakayofanya kazi ya udiwani ni sawa na Tsh 16,000 kwa mwezi provided hiyo IPAD moja inagharimu Tsh milioni moja.
Je kumlipa mtu 'mshahara' wa Tsh 16,000 kwa mwezi is too much to ask? I dont think so...

Hapo madiwani wa CCM wameshaona huo ni mtaji wa kisiasa kwao.. Bila kuangalia hiyo hela hata wakisema iende kwenye hiyo miradi ya maendeleo waliyosema je itatosha?

Nahisi wanataka kutengeneza daraja kama lile alilozindua Mh.Mavunde la 70ml Kule Dom.
 
Milioni mia haziwezi kumaliza matatizo yote katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro! Kama kujenga kilometa moja ya lami ni around Bilioni 1.6,hizo pesa hata zikipelewa huko 'hazitofanya chochote'... Nako wajanja watazipiga kwenye kununulia Diesel ya kuendeshea 'vijiko' vya halmashauri.
Kama pesa zipo na kuna uhitaji wa madiwani kununuliwa Ipad, sioni kwa nini wasinunuliwe. Nao ni watumishi wa umma, wanafanya kazi kwa kujitolea bila kulipwa mshahara. Ipad ya milioni moja, gawanya kwa miezi 60 watakayofanya kazi ya udiwani ni sawa na Tsh 16,000 kwa mwezi provided hiyo IPAD moja inagharimu Tsh milioni moja.
Je kumlipa mtu 'mshahara' wa Tsh 16,000 is too much to ask? I dont think so...

Hahaha jaribu kuigeuza hiyo habari halafu uone ungeandikaje, tuseme ingekuwa ,,Madiwani wa CCM kutumia milioni 100 kununua ipad“ ,...
 
Hapo madiwani wa CCM wameshaona huo ni mtaji wa kisiasa kwao.. Bila kuangalia hiyo hela hata wakisema iende kwenye hiyo miradi ya maendeleo waliyosema je itatosha?

Nahisi wanataka kutengeneza daraja kama lile alilozindua Mh.Mavunde la 70ml Kule Dom.
Ndo hapo. Kama miradi ya maendeleo ingekuwa kipaumbele sana, nisingekuta hata gari moja kwenye halimashauri ya manispaa. Magari yaliyopo pale ni mazito mazito ambayo kila moja limegharimu si chini ya milioni mia moja. Je wakati wananunua hayo magari mbona hawakufikiria kuwa kuna shule hazina vyoo? Tuache unafiki...
 
MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameiomba serikali kuingilia kati na kuzuia matumizi ya zaidi ya Sh milioni 104 zinazotarajiwa kununua Ipad za madiwani.

Wameomba fedha hizo zisinunue Ipad kama ilivyopangwa na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na badala yake zitumike kukarabati miundombinu ya barabara kwenye vijiji na kata za halmashauri hiyo.

Diwani wa Kata ya Okaoni, Moris Makoyi (CCM), alisema fedha hizo zilipangwa zitumike kukarabati barabara baada ya kipindi cha mvua za masika kumalizika, lakini madiwani wa Chadema na Mwenyekiti wa Halmashauri, Michael Kilawila, wameamua zitumike kununua Ipad za madiwani na baadhi ya wataalam.

“Hii ni rushwa kwa sababu wanakaribia kumaliza muda wao, vyoo vya wanafunzi mashuleni vimeanguka, zahanati hazina umeme, wakinamama wanashindwa kwenda kujifungua na wagonjwa wanafariki njiani kwa sababu barabara ni mbovu halafu wanataka kununua Ipad,” alisema.

Alisema kipaumbele ni wananchi kupata maendeleo badala ya viongozi kujinufaisha wenyewe kwa vitu ambavyo havina msingi na kudai kuwa, mwenyekiti wa halmashauri hiyo amekuwa akipeleka miradi mingi ya maendeleo kwenye kata za Chadema.

Diwani wa Kata ya Kahe Mashariki, Kamili Mmbando (CCM), aliomba serikali izuie matumizi ya fedha hizo akisema ni ufisadi ndani ya halmashauri kwani zikinunuliwa Ipad zitatumika zaidi kwa matumizi binafsi.

Diwani wa Kilema Kaskazini, Anna Lyimo (CCM), aliwataka madiwani wakumbuke kuwa wamechaguliwa kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi hivyo hawatakiwi kutumia vibaya fedha za umma bali zitumike kuleta maendeleo kwenye kata.

Akijibu hoja za madiwani hao wa CCM, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi, Kilawila alisema halmashauri hiyo inaendeshwa bila kuangalia itikadi za vyama na kwamba waliamua kununua Ipad kwa ajili ya kupunguza matumizi ya kutoa nakala kivuli na usafiri wa kusambaza nyaraka za madiwani kwenye kata 32.

“Tuliamua kuingia kwenye mfumo wa dijitali kwa sababu madiwani na wataalam wakiwa na Ipad itapunguza gharama za kutumia makaratasi na kutoa nakala kivuli na hatuna sababu za kupinga kwa sababu halmashauri nyingine zimefanya hivyo,” alisema.
Kwa zama tulizopo hatuwezi kukwepa kwenda na kasi ya mabadiliko ya technologia. Ipad zingepunguza matumizi ya kuandaa makabrasha ya vikao na watumiwe kwenye IPad zao; nachoona hapa ni kuogopa matumizi ya hizo Ipad wala siyo gharama kama inavyotaka kuaminishwa; gharama ya TZS 104 million ni kilometa ngapi? na gharama za kuchapisha makabrasha kwa mwaka ni shilling ngapi?
 
MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameiomba serikali kuingilia kati na kuzuia matumizi ya zaidi ya Sh milioni 104 zinazotarajiwa kununua Ipad za madiwani.

Wameomba fedha hizo zisinunue Ipad kama ilivyopangwa na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na badala yake zitumike kukarabati miundombinu ya barabara kwenye vijiji na kata za halmashauri hiyo.

Diwani wa Kata ya Okaoni, Moris Makoyi (CCM), alisema fedha hizo zilipangwa zitumike kukarabati barabara baada ya kipindi cha mvua za masika kumalizika, lakini madiwani wa Chadema na Mwenyekiti wa Halmashauri, Michael Kilawila, wameamua zitumike kununua Ipad za madiwani na baadhi ya wataalam.

“Hii ni rushwa kwa sababu wanakaribia kumaliza muda wao, vyoo vya wanafunzi mashuleni vimeanguka, zahanati hazina umeme, wakinamama wanashindwa kwenda kujifungua na wagonjwa wanafariki njiani kwa sababu barabara ni mbovu halafu wanataka kununua Ipad,” alisema.

Alisema kipaumbele ni wananchi kupata maendeleo badala ya viongozi kujinufaisha wenyewe kwa vitu ambavyo havina msingi na kudai kuwa, mwenyekiti wa halmashauri hiyo amekuwa akipeleka miradi mingi ya maendeleo kwenye kata za Chadema.

Diwani wa Kata ya Kahe Mashariki, Kamili Mmbando (CCM), aliomba serikali izuie matumizi ya fedha hizo akisema ni ufisadi ndani ya halmashauri kwani zikinunuliwa Ipad zitatumika zaidi kwa matumizi binafsi.

Diwani wa Kilema Kaskazini, Anna Lyimo (CCM), aliwataka madiwani wakumbuke kuwa wamechaguliwa kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi hivyo hawatakiwi kutumia vibaya fedha za umma bali zitumike kuleta maendeleo kwenye kata.

Akijibu hoja za madiwani hao wa CCM, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi, Kilawila alisema halmashauri hiyo inaendeshwa bila kuangalia itikadi za vyama na kwamba waliamua kununua Ipad kwa ajili ya kupunguza matumizi ya kutoa nakala kivuli na usafiri wa kusambaza nyaraka za madiwani kwenye kata 32.

“Tuliamua kuingia kwenye mfumo wa dijitali kwa sababu madiwani na wataalam wakiwa na Ipad itapunguza gharama za kutumia makaratasi na kutoa nakala kivuli na hatuna sababu za kupinga kwa sababu halmashauri nyingine zimefanya hivyo,” alisema.
Weka Audio Clip Mkuu.
 
Napendekeza iPad zinunuliwe na badala Yake ili tupate maendeleo ya kweli magari yote aina ya V8 na mengine yanayo fanana na hayo yauzwe,viongozi watumue Rav4 au Toyota wish
 
Naomben sample ya barabara ya milioni mia

IMG_5432.JPG
IMG_5433.JPG

Izo hapo mkuu
 
Wewe Morris Makoi yule mkandarasi aliyejenga Kituo cha Polisi Okaoni mbona mpaka sasa hamtaki kumlipa pesa zake na wewe ulikuwa Mwenyekiti wa Halmshauri ya wilaya ya Moshi wakati huo?,huo wema uonyeshe na kwa huyo Mkandarasi kama mnataka maendeleo
 
MADIWANI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameiomba serikali kuingilia kati na kuzuia matumizi ya zaidi ya Sh milioni 104 zinazotarajiwa kununua Ipad za madiwani.

Wameomba fedha hizo zisinunue Ipad kama ilivyopangwa na madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na badala yake zitumike kukarabati miundombinu ya barabara kwenye vijiji na kata za halmashauri hiyo.

Diwani wa Kata ya Okaoni, Moris Makoyi (CCM), alisema fedha hizo zilipangwa zitumike kukarabati barabara baada ya kipindi cha mvua za masika kumalizika, lakini madiwani wa Chadema na Mwenyekiti wa Halmashauri, Michael Kilawila, wameamua zitumike kununua Ipad za madiwani na baadhi ya wataalam.

“Hii ni rushwa kwa sababu wanakaribia kumaliza muda wao, vyoo vya wanafunzi mashuleni vimeanguka, zahanati hazina umeme, wakinamama wanashindwa kwenda kujifungua na wagonjwa wanafariki njiani kwa sababu barabara ni mbovu halafu wanataka kununua Ipad,” alisema.

Alisema kipaumbele ni wananchi kupata maendeleo badala ya viongozi kujinufaisha wenyewe kwa vitu ambavyo havina msingi na kudai kuwa, mwenyekiti wa halmashauri hiyo amekuwa akipeleka miradi mingi ya maendeleo kwenye kata za Chadema.

Diwani wa Kata ya Kahe Mashariki, Kamili Mmbando (CCM), aliomba serikali izuie matumizi ya fedha hizo akisema ni ufisadi ndani ya halmashauri kwani zikinunuliwa Ipad zitatumika zaidi kwa matumizi binafsi.

Diwani wa Kilema Kaskazini, Anna Lyimo (CCM), aliwataka madiwani wakumbuke kuwa wamechaguliwa kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi hivyo hawatakiwi kutumia vibaya fedha za umma bali zitumike kuleta maendeleo kwenye kata.

Akijibu hoja za madiwani hao wa CCM, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi, Kilawila alisema halmashauri hiyo inaendeshwa bila kuangalia itikadi za vyama na kwamba waliamua kununua Ipad kwa ajili ya kupunguza matumizi ya kutoa nakala kivuli na usafiri wa kusambaza nyaraka za madiwani kwenye kata 32.

“Tuliamua kuingia kwenye mfumo wa dijitali kwa sababu madiwani na wataalam wakiwa na Ipad itapunguza gharama za kutumia makaratasi na kutoa nakala kivuli na hatuna sababu za kupinga kwa sababu halmashauri nyingine zimefanya hivyo,” alisema.
"vyoo vya wanafunzi mashuleni vimeanguka, zahanati hazina umeme, wakinamama wanashindwa kwenda kujifungua na wagonjwa wanafariki njiani kwa sababu barabara ni mbovu"

Shikamoo CCM
 
Ccm na vitu vya maendeleo ni vitu mbalimbali... ingekuwa mchango wa mwenge na "mafiesta" wangeunga mkono chapchap
 
Back
Top Bottom