Moshi, Kilimanjaro: Watu waliojitambulisha kama maafisa wa TRA wavamia Rau Pub Usiku huu

bloggerboy

JF-Expert Member
Nov 13, 2017
568
1,211
Habari wanajukwaa,

TRA moshi wamevamia club maarufu ijulikanayo kama Rau pub usiku na kuifunga wakidai club hiyo inadaiwa hivyo wanatakiwa kufunga na kulipa kwanza, hali iliyopelekea tafrani ,maana wateja bado walikuwa wamejaa sana!

Umetokea mvutano mkubwa kati ya meneja wa pub hiyo na TRA akidai inakuwaje waje usiku? Wakamjibu wameagizwa na boss Mkoa

More updates and pictures to come!
 
Kama Wiki moja nyuma Hawahawa TRA walivamia 40 40 Bar pale Tabata Bima na kuwatoza faini ya Million 6,

Ilikua hivi,
Afisa wa TRA alienda mpaka Kaunta na kuagiza maji ya 1000 Kilimanjaro, akahudumiwa bila risiti ndipo akatoa kitambulisho na kutaka kukagua mauzo ya Siku hiyo ndipo walipofikia kuwatoza Faini ya 6 Million
 
Vipi kuhusu agizo la Waziri Mpango juu ya kufunga biashara za watu?

Alipiga marufuku TRA kufunga biashara za wafanyabiashara kwa kushindwa kulipa kodi badala yake watumie njia ya kukaa nao na kujadiliana namna ya kulipa kodi hizo na kwamba uamuzi wa kufunga biashara uwe wa mwisho baada ya njia zote kushindikana na mwenye mamlaka ya mwisho ya kufanya hivyo ni Kamishna Mkuu wa TRA.

“Ukifunga biashara ya mtu leo kwa madai ya kodi ambazo anadaiwa za huko nyuma maana yake unapoteza kodi nyingi ambazo ungezipata kama biashara ingeendelea. Kufunga Biashara yawe ni maamuzi ya mwisho kabisa pale inapotokea hakuna mbadala kabisa wa kupata ufumbuzi na nilikwishatoa maelekezo siku za nyuma kuwa uamuzi huo utolewe na Kamishna Mkuu wa TRA in person. Hata matumizi ya Agency Notice busara itumike kumlazimisha mlipa kodi alipe deni - Kimsingi iwe ni njia ya mwisho (last resort) baada ya majadiliano kushindikana kabisa.” Aliongeza Dkt. Mpango
 
Kama Kuna evidence ya mtu kutenda kosa Kuna ubaya gani Kama ukimwita ofisini asubuhi? He usiku huo analipaje hiyo fine au Kodi yako? Je walevi wakiungana na kuwashambulia mtamlaumu Nani?
 
Kama Wiki moja nyuma Hawahawa TRA walivamia 40 40 Bar pale Tabata Bima na kuwatoza faini ya Million 6,

Ilikua hivi,
Afisa wa TRA alienda mpaka Kaunta na kuagiza maji ya 1000 Kilimanjaro, akahudumiwa bila risiti ndipo akatoa kitambulisho na kutaka kukagua mauzo ya Siku hiyo ndipo walipofikia kuwatoza Faini ya 6 Million
Mi nakumwaga roho
 
Ila baa nying hazitoi risiti na EFD wanazo sijajua utaratibu upoje na kodi zao wanalipaje sijawah enda baa nipewe risiti...

Kuna siku nilikua na jamaa angu wa TRA mpenda sifa hv akawakazia wampe risiti ikaonekana hawajatoa risiti kama mwezi hv kwny kile kimashine....

Sema nilimkanya jamaa aache udwanzi wa kudai risiti off duty atakuja pigwa afe
 
Kama Kuna evidence ya mtu kutenda kosa Kuna ubaya gani Kama ukimwita ofisini asubuhi? He usiku huo analipaje hiyo fine au Kodi yako? Je walevi wakiungana na kuwashambulia mtamlaumu Nani?
Vipi kama umemuita hakuitika!
Kwani hiyo pub ndo ilikuwa inazinduliwa usiku huo, si ipo siku nyingi?

Walevi washambulie kwa maslah gan, kwani ikifungwa bar ndo wamefungiwa kulewa!
Tuwaache wataalam wakati mwingine wafanye kazi,
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom