Moshi: Juma Raibu ang'olewa aunganishwa na Ole Sabaya kesi ya uhujumu uchumi

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,773
21,327
Ole Sabaya = Juma Raibu Juma
760A847C-4B9B-4C84-AC4A-09914D1302A3.jpeg
 
Ni jambo jema. Ahadi ya Mungu haichelewi wala kukawia bali huja kwa wakati wake.

Walitenda uovu wa ajabu, wakiamini wana kinga milele.

Waovu wote wa awamu ya 5, kwa wakati ufaao, tunamwomba Mungu aendelee kuonesha ukuu wake kwa kuwapa nafasi ya kulipia uovu wao.

Sabaya, anatajwa kukata watu masikio, kuwapiga watu misumari, na kuwapora watu fedha, alipatwa na upofu akiamini kuwa uovu wake hautakuja kuhojiwa popote, lakini sasa anatambua kuwa alikuwa zaidi ya mjinga.
 
Kama mchakato utakamilika hadi mwisho na haki ikatendeka hapo nitaamini. Ila kwa hii sisiem ya mwaka 77 kwa maigizo hawajambo. Hivi ina maana kati ya 2015 hadi 2020 CCM nzima ilikua imelala? Usalama walilala? Jeshi la polisi walilala? Mambo ya hawa watu kama walifanya wenyewe bila baraka za chama na wakubwa wao hayakujulikana? Naendelea kuwa Tomaso hadi nipapase kwa mikono yangu mwenyewe.
 
Mbona taarifa zipo wazi. Uovu wa Sabaya ulifikishwa mpaka kwa PM. PM alifikisha taarifa mpaka kwa jiwe, lakini jiwe, kwa vile alikuwa na roho ya uovu, iliyofurahia uovu anaoutenda Sabaya, hasa dhidi ya Mbowe, aliendelea kubariki ushetani ule.

Katika uovu wa Sabaya, umwone jiwe.
 
Mwandishi wa ITV Kilimanjaro Bi . Fadhila Omary siku Juma Raibu anakamatwa Alihongwa fedha Ili asirushe Wala kutoa taarifa Za kukamatwa kwake kwenye vyao vya habari. Jf imefuatilia hadi kuliibua hili.
 
Mbona taarifa zipo wazi. Uovu wa Sabaya ulifikishwa mpaka kwa PM. PM alifikisha taarifa mpaka kwa jiwe, lakini jiwe, kwa vile alikuwa na roho ya uovu, iliyofurahia uovu anaoutenda Sabaya, hasa dhidi ya Mbowe, aliendelea kubariki ushetani ule.

Katika uovu wa Sabaya, umwone jiwe.
Sabaya matendo yake hayakuwa ya kificho,
Viongozi wake walifahamu, ila kwa vile walioumizwa wengi ni Chadema, wakadhani anapigania chama ccm, kumbe nyuma ya pazia anafanya ujambazi wa kutisha, aendelee kupambana mahakamani, hata akitoka atakuwa amejifunza kitu,
 
Wazalendo wangapi wa enzi ya mwendazake walikuwa wasafi ?

Kwa mwendo huu huku kulikuwepo tetesi / uvumi juu ya waovu kujificha ktk kichaka cha uzalendo, tunaimani kuwa rushwa na ufisadi wa kutisha pia maovu ya kuogofya dhidi ya utu wa binadamu ulitokea ndani ya miaka ya 2015- 2021
 
Mbona kuna makosa makubwa ya kiuandishi kwenye hiyo Hati ya Mashtaka? Tafadhalini Mawakili wenzangu wa Serikali, umakini unatakiwa wakati wa kuandaa nyaraka kama hizi. Wakati mwingine makosa haya huyumbisha hata shauri zima. Masahihisho yafanyike mapema!
Aisee....
 
Mbona Mnyeti, Makonda, Mrisho Gambo, Ally Hapi, Jerry Muro bado wapo uraiani?
Ally Hapi, Mnyeti, Jerry Muro hawakufanya ujambazi, wao ni siasa tu. Ukifatilia Kwa undani Hawa mabwana walikuwa wanasaidia wananchi Sana, wakitatu CHANGAMOTO za wananchi BILA kujali itikadi na Imani zao na bila kiathiri utu wao.

KAZI IPO KWA GAMBO, GAMBO TUBU, TUBU NA UJIREKEBISHE. KUHUSU MAKONDA NYOTE MWAFAHAMU
 
Back
Top Bottom