Moshi: International School of UWCEA yasitisha masomo Baada ya Wanafunzi 2 kupatwa na Corona

Punguza ushamba
Astro Zeneca wamewapa kandarasi viwanda vya India kuzalisha chanjo kutokana na mahitaji makubwa kuliko uzalishaji wao
We baki Chatto ukijifukuza vitunguu na Joseph Kasheku Musukuma 😫
Huyo jamaa planet sijui anaishi dunia gani, demand ni kubwa kuliko uzalishaji kuna order zimewekwa baada ya miezi ndio watapata mpaka leo WHO wamezishutumu nchi tajiri kununua in advance nakuacha nchi maskini bila chanjo.

Kubwa zaidi nchi zetu tutanunuliwa na haohao tunaowatukana tutapewa bure tu. Kwanza pesa yenyewe hatuna ya kununua.
 
Nafikiri wangesema hali zao ikoje because Corona ni ugonjwa kama mwingine. Mafua hayo.Hivi do you think kwamba Corona vaccine itasababisha Corona isitokee kabisa?
 
Hivi ukija na Corona Tanzania ukiingia tu kwenye mpaka wa Tanzania Corona inaisha. Basi kama ni hivyo tunaomba muombee wa wagojwa wa cancer, kisukari na tuombee malaria iishe kabisa.
 
Hawa lazima wakipate Cha Moto, serikali imetoa utaratibu wa Nani anapaswa kutoa taarifa za Corona.
P, VP, PM na WA. Huyo aliyetoa taarifa Ana moja ya nyadhifa zilizotajwa?
Ni kweli kabisa. Hakuna mtu mwenye mamlaka ya kisheria wa kutoa au kusambaza taarifa ya magonjwa kama hayo isipokuwa hao wanne. Lazima wamiliki wa shule hiyo wachukuliwe hatua kali sana.

Siku nyingine watatangaza wanafunzi watano wameugua Ebola! Inaonekana shule yenyewe inamilikiwa na watu wa nje ya nchi wanaotaka kuchafua biashara ya utalii wa nchi yetu ambao unarejea kwa spidi kali.

Jf yetu wasitake kutuharibia kwa kusambaza humu taarifa kama hizi kwani ni kinyume na sheria ya magonjwa haya.
 
Hatari sana, na pole yao sana.

Ila wenye mamlaka ya kutangaza jambo kama hili, sii tulishapewa muongozo ni wakina nani wanaopaswa kutoa taarifa kama hizi.
 
Kuna wimbi la hofu juu ya Corona,watu wameanza kuchukua tahadhari wenyewe kwa kuanza kurejesha ndoo za kunawia nje ya majumba yao!

Kuna hospitali wauguzi wameanza kuvaa barakoa!

Kuna dalioi ugonjwa huu umerejea kwa kasi!

Chukua tahadhari!
Hapo ndio huwa nashindwa kuwaelewa,mnavyosema huu ugonjwa umerudi tena kwani lini uliondoka au kupungua? serikali ilipoacha kutangaza takwimu za corona ndio kipindi ambacho corona ilikuwa inaonekana imezidi,sasa leo kusema imerudi tena ni kwa vipimo gani tunavyotumia kujua iliondoka na sasa inarudi?
 
Kwasasa kuna vifo visivyoeleweka vimeanza kutokea,ni jambo la kawaida kuhusisha vifo hivyo na Corona hasa ukizingatia dalili walizokuwa nazo hao wafu!
 
Kwasasa kuna vifo visivyoeleweka vimeanza kutokea,ni jambo la kawaida kuhusisha vifo hivyo na Corona hasa ukizingatia dalili walizokuwa nazo hao wafu!
Swali langu ni lini corona iliondoka au kupungua na kwa njia gani iliyotumika kuondoa au kupunguza hiyo corona hadi sasa hivi ndio kuwe na vifo visivyoeleweka ambavyo havikuwepo nyuma?
 
Swali langu ni lini corona iliondoka au kupungua na kwa njia gani iliyotumika kuondoa au kupunguza hiyo corona hadi sasa hivi ndio kuwe na vifo visivyoeleweka ambavyo havikuwepo nyuma?
Hapo katikati kulikuwa hakuna vifo vya kutatanisha ambavyo vilihusisha matatizo ya upumuaji!
Sasa vifo vinavyohusiana na matatizo ya upumuaji vimeanza kusikika mitaani!
Wala sitaki kuingia kwenye utaalumu, just a normal observation kwasababu hakuna vipimo vilivyokuwa vinafanyika au vimefanyika!
Hatuwezi kusema for certain kama Corona ilitokomea au haikutokomea, ila tunaweza kufanya analysis kulingana na madhara!
 
Back
Top Bottom