Moshi: Fedha zilizotengwa kununua Bastola ya Mkurugenzi kurejeshwa

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
8,986
14,713
Meya wa manispaa ya Moshi Mh.Juma Raibu ameagiza uongozi wa manispaa hiyo kurejesha Fedha kiasi cha Tsh.3.2 milioni zilizotengwa kwaajili ya kununua Bastola ya Mkurugenzi wa manispaa.

=======

meyapic 2.jpg

Moshi. Meya wa manispaa ya Moshi, Juma Raibu ameagiza Sh3.2 milioni zilizotengwa na halmashauri ya manispaa hiyo kwa ajili ya kununua bastola ya mkurugenzi kurejeshwa.

Raibu ametoa tamko hilo leo Ijumaa Mei 28, 2021 katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ofisi za mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk Stephen Kagaigai ambaye pia alishiriki kikao hicho.

Amesema fedha hizo zilipitishwa na halmashauri hiyo mwaka 2015 na kubainisha kuwa ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

"Kuna fedha zilipitishwa mwaka 2015 kiasi cha Sh3.2 milioni kwenye akaunti ya halmashauri kununua bastola ya mkurugenzi, haya ni matumizi mabaya ya fedha za umma, nimeagiza fedha hizi zirudishwe mara moja," amesema Raibu.

Chanzo: Mwananchi
 
Huko moshi kuna wizi mkubwa. Mkurugenzi ananunuliwa bastola ya kumlinda Nani? Huyo mkurugenzi alistaafu na alihujumu hiyo manispaa mabilioni ya fedha. Huko huko anayekaimu walikuwa mtandao mmoja.

Uteuzi wa Wakurugenzi uendane na uteuzi wa wakuu wa idara ndani ya manispaa nchini. Wakuu wa idara nao wamekuwa kama mchwa kwenye fedha za umma.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom