Moshi: Diwani wa CHADEMA akwepa risasi sita akipambana na majambazi

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Diwani wa kata ya Kiborlon (Chadema) katika Manispaa ya moshi, Frank Kagoma ameonyesha ujasiri wa hali ya juu alipopambana na majambazi waliokuwa na silaha za moto.

Alinusurika Kuuawa baada ya majambazi hao waliokuwa na bunduki na bastola kumfyatulia risasi sita alipokuwa akiwafukuza ambazo hata hivyo hazikumpata.

Tukio hilo ambalo lilionekana kama sinema, lilitokea mwishoni mwa wiki baada ya majambazi hao kuvunja duka la jumla la kuuza mitumba linalomilikiwa na Menti Mbowe na kupora sh10 milioni.

Katika tukio hilo lililotokea saa tano asubuhi eneo la kiborlon, majambazi hao walimjeruhi kichwani mfanyabiashara huyo anayemiliki pia mabasi ya Machame Safaris.

Akisimulia tukio hilo, diwani huyo alisema siku ya tukio akiwa maeneo ya kiborlon alipigiwa simu kuwa mfanyabiashara huyo amevamiwa na majambazi ndipo alipoendesha gari lake hadi eneo la tukio.

"Nilipofika pale wale majambazi watatu ndio walikuwa wanatoka kwenye duka, nikampelekea gari yule aliyekuwa ameshika bunduki, kuona hivyo akafyatua risasi hewani "alisema Kagoma.

" Yule mwenye bunduki akaingia uchochoroni kuelekea barabara ya ya stendi ya Kidia, mwenzake aliyekuwa na bastola naye akawasha risasi nyingine hewani kunitisha "alisema.

Baada ya hali hiyo diwani huyo alilazimika kujificha kwenye gari na majambazi hao walidandia pikipiki na kuanza kukimbia kuelekea barabara ya Msaranga, naye akawafuata kuelekea huko.

" Wakati huo vijana wangu wa boda boda wakawa nao wamesikia hilo tukio tukaanza kusaidiana kuwafukuza lakini mbele kidogo pale Msaranga wale majambazi wakasimamisha pikipiki yao umbali wa mita 30 kutoka nilipokuwa na mmoja wao akafyatua risasi mbili na mwenye bastola naye risasi mbili kuelekea uelekeo wangu.

Nililazimika kujificha kwenye kiti, wale majambazi wakajua wameniua,wakapanda tena pikipiki ili watoroke, nikawasha tena gari huku vijana wangu nao wakinisaidia tukaanza kuwafukuza," alisema.

Kagoma alisema majambazi hao walipita maeneo ambayo gari haliwezi kupita, wakaelekea eneo la Mabogini Moshi Vijijini hadi lango la TPC na baadaye wakaelekea Rundugai wilayani Hai.

Kuna eneo vijana wangu wanasema kulikuwa na vumbi sana ndipo walipowapotezana na majambazi wakatoroka kupitia njia ya reli ili kukwepa polisi waliokuwa wakiwasubiri mbele.

Hatukuwa na silaha lakini tulijitahidi kupambana nao kwa ujasiri,tatizo tulikosea kidogo tulitakiwa wakati tukiwafukuza tuwe na mawasiliano na polisi tuwape uelekeo wa majambazi.

Chanzo - Mwananchi.
 
Hao vijana waliowakimbiza hao majambazi wenye silaha nzito nao walikuwa na silaha au mliamua kuwatoa sadaka
Mkuu si umesikia hawakuwa na silaha yoyote ilikuwa kujitoa nafsi
 
Hata askari aliyefuzu mafunzo ya kijeshi haruhusiwi kufanya kitu alichofanya huyo diwani....kupamabana na majambazi wenye silaha za moto bila silaha ya moto ni sawa na kuonja sumu!
Hila Mungu kamlinda sana na ashukuriwe!
 
Uyu Kagoma namjua ni mpenda kick..hana lolote uyo...uanze kukimbiza majambaz huna hata panga unajipenda kweli? uyo alieibiwa hana walinzi? kazi yao nini..anakaa na 10m+ ndani hana silaha? uyu mchaga vipi bwana....usikae urudie tena huo upuuz wako bwana Kagoma kama ni kweli maana tutakuzika apo mnazi uache mayatima..haya nenda kwa tajiri akulipe
 
Akisimulia tukio hilo, diwani huyo alisema siku ya tukio akiwa maeneo ya kiborlon alipigiwa simu kuwa mfanyabiashara huyo amevamiwa na majambazi ndipo alipoendesha gari lake hadi eneo la tukio.

Kuna kitu sijaelewa kuhusu huyo diwani alipopata taarifa ya huyo mfanyabiashara kuvamiwa alikimbilia eneo la tukio!! Nilifikiri alitakiwa akimbilie kituo cha polisi kilicho karibu aondoke na askari kuelekea eneo la tukio!!

Halafu sijaelewa kuwa alikuwa akikimbiza majambazi akiwa hana silaha yoyote !! Alikuwa akiwakimbiza au akiwasindikiza majambazi kutokomea kusikojulikana? Alipokuwa akiwakimbiza je alikuwa akiwajulisha polisi kinachoendelea kila hatua kwa simu? ili wawafukuze nyuma na mbele na kila kona wanakoelekea?

Kuna vitu sivielewi
 
hahaha!!! umesoma kwa stress gamba! hujaona kwamba kuna mahali polisi waliweka road block ila majambazi wakasepa?? ina maana polisi walipewa taarifa.
 
Kuna kitu sijaelewa kuhusu huyo diwani alipopata taarifa ya huyo mfanyabiashara kuvamiwa alikimbilia eneo la tukio!! Nilifikiri alitakiwa akimbilie kituo cha polisi kilicho karibu aondoke na askari kuelekea eneo la tukio!!

Halafu sijaelewa kuwa alikuwa akikimbiza majambazi akiwa hana silaha yoyote !! Alikuwa akiwakimbiza au akiwasindikiza majambazi kutokomea kusikojulikana? Alipokuwa akiwakimbiza je alikuwa akiwajulisha polisi kinachoendelea kila hatua kwa simu? ili wawafukuze nyuma na mbele na kila kona wanakoelekea?

Kuna vitu sivielewi
Ndo kitu ambacho hata yeye mwenyewe amejilaumu kuwa walikosea.. Ilitakiwa wawe na mawasiliano na polisi

Ukisoma thread hapo mwisho
 
Back
Top Bottom