Moshi: Basi la Kampuni ya DZD Royal Classic lagonga Kimotco wakati wakigombea kutoka Stendi

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Basi la kampuni ya DZD Royal Classic linalofanya safari zake kati ya Moshi kwenda Mwanza limeligonga la Kampuni ya Kimotco ambalo linafanya safari zake kati ya Moshi kwenda Iringa leo asubuhi Oktoba 31, 2018.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema walikuwa waking'ang'ania kugombea kutoka katika kituo cha mabasi hapo.

Hakuna madhara yaliyojitokea kwa abiria wote walikuwa ndani ya basi zaidi ya uharibifu wa hayo magari.

...Je unashauri nini kuhusu kadhia hii na hasa ukizingatia rai mbalimbali zinatolewa kwa madereva kuwa waangalifu muda wote wakiwa barabarani kuona kama wanaweza kuepusha maafa zaidi ambayo yangeweza kuepukika.

Kumbuka hali hiyo hutokea kwa muda fulani hata kwenye kupima uzito (kwenye mizani) kugombea kutaka kuwa wa mwanzo. Nini kifanyeke. Mabasi na sehemu zote za vituo yawe yanatoka kwa namba ama?
IMG_20181031_160937_580.jpeg
 
Huu ni uzembe sana. Yamkini kusoma kwao na kuleta Certificate mezani haikuwasaidia
 
Bahat mbaya sana hiyo. Ingekuwa maksudi madhara yangekuwa zaidi ya hapo. Lkn si nyinyi abiria huwa mnapenda mabas mliyopanda yawe mbele zaid hayo ndio matokeo yake
 
Wakapimwe mikojo, nakumbuka Abood toka arusha kwenda moro alitaka kutuua kwa upuuzi huo huo..nashukuru dereva ndio aliumia zaidi yetu. Wanakimbiza kuwahi abiria wa vituo vya mbele...sasa hizo spidi zake za kutoka stendi na kuwawahi abiria..ndio balaaa aisee.

Hata pale mwanza, asubuhi wanatoka kwa vurugu sana ...siku yakiumana hao polisi watakimbia....lakini hukaa kimya tu na kuacha wanabishana rudi nyuma wewe rudi nyuma wewe!

Aisee dakika 15 baada ya kutoka stendi arusha tulibamizwa kwenye mlori wa kubeba udongo wa kutengenezea barabara kwa nyuma baadae likaenda katikati ya barabara likagota hapo...wapuuzi kweli hao. dereva alibaki hospitali wala sijui km alipona, maana kiganja cha mguu kilitobolewa hadi upande wa pili.....so tulimtoa kwa jeki baada ya kunyenyua mavyuma yaliyoingia ndani
 
Hapo hakuna bahati mbaya..Yaani mnashindana huku mkijua kwamba mmebeba roho za watu halafu mtegemee ikitokea ajali iitwe bahati mbaya!

Huo uliofanyika hapo ni uzembe, kutokua makini na chombo na abiria kwa ujumla
Bahat mbaya sana hiyo. Ingekuwa maksudi madhara yangekuwa zaidi ya hapo. Lkn si nyinyi abiria huwa mnapenda mabas mliyopanda yawe mbele zaid hayo ndio matokeo yake
 
Dah..Inasikitisha
Wakapimwe mikojo, nakumbuka Abood toka arusha kwenda moro alitaka kutuua kwa upuuzi huo huo..nashukuru dereva ndio aliumia zaidi yetu. Wanakimbiza kuwahi abiria wa vituo vya mbele...sasa hizo spidi zake za kutoka stendi na kuwawahi abiria..ndio balaaa aisee.

Hata pale mwanza, asubuhi wanatoka kwa vurugu sana ...siku yakiumana hao polisi watakimbia....lakini hukaa kimya tu na kuacha wanabishana rudi nyuma wewe rudi nyuma wewe!

Aisee dakika 15 baada ya kutoka stendi arusha tulibamizwa kwenye mlori wa kubeba udongo wa kutengenezea barabara kwa nyuma baadae likaenda katikati ya barabara likagota hapo...wapuuzi kweli hao. dereva alibaki hospitali wala sijui km alipona, maana kiganja cha mguu kilitobolewa hadi upande wa pili.....so tulimtoa kwa jeki baada ya kunyenyua mavyuma yaliyoingia ndani
 
Hapo hakuna bahati mbaya..Yaani mnashindana huku mkijua kwamba mmebeba roho za watu halafu mtegemee ikitokea ajali iitwe bahati mbaya!

Huo uliofanyika hapo ni uzembe, kutokua makini na chombo na abiria kwa ujumla
Kama wewe ni dereva utaelewa nilicho maanisha ila kama siyo sawa.
 
Dah..Inasikitisha
hao watu wakichekewa watatumaliza. Yaani siku ile najua ni Mungu tu....maana nilikuwa nawaza sana na sikuwa na uhakika wa kufika moro. Jamaa alikuwa anaendesha vurugu nyingi breki za ghafla...hadi hiyo ajali anayumbisha gari takribani mara tatu abiria wote tulisimama kutafuta pa kujificha....ajari mnaiona kabisa aisee. Dah!
 
Back
Top Bottom