Moshi: Anayetuhumiwa kumuua mama yake kwa panga afikishwa mahakamani

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
1645625418670.png

Washitakiwa watatu wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi leo Jumatano Februari 23, 2022 wakikabiliwa na mashtaka ya kumuua Patricia Ibreack Paul (66) mkazi wa Rau mjini Moshi Kisha kuuzika mwili wake kwenye shimo nje ya makazi yake.

Washitakiwa hao ni Wendy Mrema ambaye ni mtoto wa marehemu pamoja na waganga wawili wa jadi Omary Rang’ambo (32) mkazi jijini na Dar es Salaam na Waziri Ally (37) mkazi wa Mkoani Tanga.

Wendy ambaye ni mtuhumiwa wa pili katika kesi hiyo anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya mama yake kisha mwili wake kuuzika nje ya nyumba aliyokuwa akiishi marehemu, huku panga linalodaiwa kutumika katika tukio hilo likikutwa na damu ndani ya kaburi alilolozikwa.

Patricia alitoweka nyumbani kwake eneo la Rau nje kidogo ya Mji wa Moshi tangu Februari 2021 hadi mwili wake ulipofukuliwa Januari 9, 2022.

Awali washitakiwa hao walisomewa mashitaka ya kuua kwa kukusudia, upande wa mashitaka ukasema upelelezi haujakamilika, hivyo hakimu mkazi akapanga tarehe 9 Machi, 2022 shauri hilo litatajwa tena mahakamani hapo.

Washitakiwa wote wamerejeshwa rumande kwa kuwa shitaka hilo halina dhamana.

KUJUA MKASA MZIMA WA KESI HII SOMA:
- Moshi: Binti amuua Mama yake mzazi kisa Mali. Mwili wagundulika ulipozikwa baada ya mwaka mmoja
 
Back
Top Bottom