MOSHI : Aliyebadili dini afariki baada ya kubatizwa

Status
Not open for further replies.

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
f43d1213da75b03969f01ef8c03c5df6.jpg
Mkazi wa Mailisita wilayani Hai, Paulo (35) amekufa maji baada ya kuzama katika Mto Kikafu, dakika chache baada ya kubadili dini na kubatizwa na maji ya mto huo kwa imani ya dini ya Kikristo

Paulo ambaye jina la awali lilikuwa Issa Juma kabla hajabadili dini, alifariki Jumapili iliyopita katika mto huo, wakati wa shamrashamra za kubatizwa kwake zikiendelea pembeni ya mto

Hata hivyo, Jeshi la Polisi lililazimika kuwakamata wachungaji wawili wa kanisa la Efatha waliombatiza lakini waliachiliwa baada ya Polisi kujiridhisha kuwa Paulo alikufa maji baada ya kubatizwa

Habari zilizothibitishwa na Polisi, zimeeleza baada ya kubatizwa saa 8.30 mchana na wakati waumini wakiimba kwa ajili ya kurudi kanisani, ndipo Paulo na mwenzake waliamua kurudi kuogelea.

Chanzo :Mwananchi
 
f43d1213da75b03969f01ef8c03c5df6.jpg
Mkazi wa Mailisita wilayani Hai, Paulo (35) amekufa maji baada ya kuzama katika mto Kikafu, dakika chache baada ya kubadili dini na kubatizwa na maji ya mto huo kwa imani ya dini ya kikristo

Paulo ambaye jina la awali lilikuwa Issa Juma kabla hajabadili dini, alifariki Jumapili iliyopita katika mto huo, wakati wa shamrashamra za kubatizwa kwake zikiendelea pembeni ya mto

Hata hivyo, Jeshi la polisi lililazimika kuwakamata wachungaji wawili wa kanisa la Efatha waliombatiza lakini waliachiliwa baada ya polisi kujiridhisha kuwa Paulo alikufa maji baada ya kubatizwa

Habari zilizothibitishwa na polisi, zimeeleza baada ya kubatizwa saa 8.30 mchana na wakati waumini wakiimba kwa ajili ya kurudi kanisani, ndipo Paulo na mwenzake waliamua kurudi kuogelea.

Chanzo :Mwananchi
Jamaa ana bahati sana amekufa wakati kishabatizwa!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom