Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Paulo ambaye jina la awali lilikuwa Issa Juma kabla hajabadili dini, alifariki Jumapili iliyopita katika mto huo, wakati wa shamrashamra za kubatizwa kwake zikiendelea pembeni ya mto
Hata hivyo, Jeshi la Polisi lililazimika kuwakamata wachungaji wawili wa kanisa la Efatha waliombatiza lakini waliachiliwa baada ya Polisi kujiridhisha kuwa Paulo alikufa maji baada ya kubatizwa
Habari zilizothibitishwa na Polisi, zimeeleza baada ya kubatizwa saa 8.30 mchana na wakati waumini wakiimba kwa ajili ya kurudi kanisani, ndipo Paulo na mwenzake waliamua kurudi kuogelea.
Chanzo :Mwananchi