Moshi: Akamatwa na polisi kwa kosa la kufyatua risasi ovyo

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Moshi.Mfanyakazi mmoja wa Kampuni ya Marenga Investment ya mjini Moshi amekamatwa na polisi kwa kosa la kufyatua risasi ovyo baada ya gari lililokuwa mbele yake kutomruhusu kupita kwa wakati.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amesema jana ameagiza mfanyabiashara huyo anyang’anywe silaha na kufunguliwa mashtaka ya matumizi mabaya.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki eneo la Rongai wilayani Rombo na ofisa huyo alilifyatulia gari hilo risasi mbili ambazo hazikuleta madhara.

Amedai kuwa siku hiyo saa 11:30 jioni, mtuhumiwa huyo akiwa na watu wengine watatu katika gari aina ya Suzuki Escudo, alilifyatulia risasi gari aina ya Mitsubish Canter.

Chanzo: Mwananchi
 
Hizi silaha zinawapa watu kichaa sasa.. Mtu akimiliki kidubwana chake hicho basi anajiona yeye ndo mume, yeye ndo kila kitu... Wamsweke tu kunakostahili
 
Upumbavu tu hizi silaa wanapewa kama njugu wakati kuna watu hawakustahili kuwa nazo , ila wakati wa mchakato wa silaha si ali qualify mkampa wenyewe ,

Tatizo lipo kwa watoa silaha ama wananchi ??
 
Mfanyakazi mmoja wa Kampuni ya Marenga Investment ya mjini moshi, amekamatwa na jeshi la polisi kwa kosa la kufyatua risasi ovyo baada ya gari lililokuwa mbele yake kutomruhusu kupita kwa wakati.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amesema jana ameagiza mfanyakazi huyo anyang'anywe silaha na kufunguliwa mashtaka ya matumizi mabaya ya silaha.

Chanzo :Mwananchi
Mpuuzi kabisa huyu bwana.
Anastahili kichapo.
Watu wengine hawastahili kabisa kumiliki silaha.
 
Hizi silaha zinawapa watu kichaa sasa.. Mtu akimiliki kidubwana chake hicho basi anajiona yeye ndo mume, yeye ndo kila kitu... Wamsweke tu kunakostahili
Kupotezewa muda tu hivyo.. je angeibiwa siangefyeka watu bila kuangalia
 
Back
Top Bottom