MORUWASA Morogoro na ufisadi wenu na wanasiasa

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,238
2,864
Kama kawadia yangu napenda kula raha kila wakti noti zikijaa mfukoni. Jana nilikuwa Morogoro kwenye hotel ya Mbunge Shabib, inaitwa MORENA, njiani kabisa pale Msamvu. Hotel Porsche sana! Kilichonishangaza, maji ni ya kumwaga ukilinganisha na maisha yetu ya Dar. Lakini pia Moro maji ni shiiida, kila kona watu wanazunguka na madumu mekundu. Nikaanza kutafuta nini na wapi Morena anapata maji.

Maji ya Morena yanatoka MORUWASA kinyume na taratibu za ugawaji maji mijini. MORENA amepewa bomba la inchi 4 peke yake wakati majirani wanahangaika na maji ya kunywa. Huu ndo ufisadi wa wafanyabiashara kama Shabib kwa kushirikiana na taasisi ya serikali, MORUWASA. MORENA anapewa bomba ambalo kawaida hutumika kuwapa maji wateja wasiopungua maelfu!

Nchi imejifia tu! Eti Shabib na wenzake ktk biashara ya hotel, wana hadhi kuliko taratibu za MORUWASA!
 
Baada ya kushambulia tembo wa mikumi sasa wanashambulia maisha yetu!
Nilijua tu! Moro wanategemea bwawa! Mtu anasimika mjengo mrefu na vyumba kibao, alitegemea apate wapi maji? Ni kuhonga tu tangu waziri na MORUWASA, wanaachia maji. Potelea mbali wapogolo na waluggulu hata wasipooga.
 
Kama kawadia yangu napenda kula raha kila wakti noti zikijaa mfukoni. Jana nilikuwa Morogoro kwenye hotel ya Mbunge Shabib, inaitwa MORENA, njiani kabisa pale Msamvu. Hotel Porsche sana! Kilichonishangaza, maji ni ya kumwaga ukilinganisha na maisha yetu ya Dar. Lakini pia Moro maji ni shiiida, kila kona watu wanazunguka na madumu mekundu. Nikaanza kutafuta nini na wapi Morena anapata maji.

Maji ya Morena yanatoka MORUWASA kinyume na taratibu za ugawaji maji mijini. MORENA amepewa bomba la inchi 4 peke yake wakati majirani wanahangaika na maji ya kunywa. Huu ndo ufisadi wa wafanyabiashara kama Shabib kwa kushirikiana na taasisi ya serikali, MORUWASA. MORENA anapewa bomba ambalo kawaida hutumika kuwapa maji wateja wasiopungua maelfu!

Nchi imejifia tu! Eti Shabib na wenzake ktk biashara ya hotel, wana hadhi kuliko taratibu za MORUWASA!
Wivu unakusumbua
 
Hiyo ni 9, 10 kuna matajiri wanaofanya biashara ya maji Kihonda wameunganishwa kwenye line inayopeleka maji kwenye tank kubwa, kinachofanyika Moruwasa wakisukuma maji kwenda kwenye matanki ya public matajiri hao wana suck maji kwa pump kuyaelekeza majumbani kwao ili asubuhi yake wayauze, hizo connections zimefanywa na wafanyakazi wa hiyohiyo mamlaka na wanapokea rushwa kila wakisukuma maji, hiyo ndiyo kazi inayoendelea, wananchi wanaambiwa maji yamepungua Mindu, lakini wauzaji wanapelekewa majumbani kwa gharama za serikali
 
Sisi wakazi wa kingolwira majengo mapya (mtaa wa bomba la mafuta).

Kuna miundo mbinu ya maji iliwekwa zamani na miradi ya Mh Mariam ditopile ambayo ilifika kwetu na maji tulikuwa tunapata vizuri tu hadi april mwaka jana 2021.(sisi tunaamini before JPM passing).

Yalitoka vizuri iwe mvua liwe jua.ila kwa sasa hatupati maji .

Toka august mita zetu hazisomi maji tunauziwa na bowser kwa sh 20000 kwa lt 1000 kwa vile huku ni mbali.(inatugharimu).

Mwanzo tuliambiwa ni ukame, mvua imenyesha tunaambiwa ni matope,

Ajabu ni taasisi za karibu tunaotumia mradi hii ya karibu karibu yaani maeneo ya chem chem ya mlima yaani magereza, jeshi na mkambarani hadi mikese wao hawakuwa na kadhia hii, Jeshi la pangawe wanauza masaa 24 mabomba 4 na utokaji ni presha nzuri sana.ajabu sisi tulio chini ya mlima wa jeshi hatupati ni IMANI pamefungwa mahali kututaabisha.

Sisi tunaambiwa ufumbuzi ni kuusubiria mradi wa mwindu, mazimbu, lukobe, yepsa , tungi na kingolwira ufike.

Tunachokiona moja SSH anahujumiwa.watu kauli zao ni kabla yalitoka ila baada ya kutenguliwa mkurugenzi wa moruwasa hatupati maji.

Pili, Diwani ni magumashi ni mbabe na watu tunamuogopa.
Tatu mkuu wa wilaya amekagua sana vyanzo vya maji lakini waliandaa mabomba na kumwambia wanabadili mradi wa zamani kwenye ule mradi aliowahi simamia Ditopile.

Sasa mvua zinanyesha hatujapata hata tone na ni wiki ya pili mvua zinanyesha.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom