Morrison huru kujiunga na Simba SC, kamati yasema mkataba wake na Yanga una mapungufu

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
1597243318302.png


Baada ya vikao nenda rudi kwa siku takribani 3 hatimaye TFF wamejitokeza na kusema kuwa wamefikia uamuzi baada ya vikao vizito

Mchezaji raia wa Ghana, Bernard Morrison amepewa uhuru wa kujiunga na Simba Sc baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kusema kuwa Mkataba wake na Yanga Sc una mapungufu.

Pamoja na Yanga kuwasilisha picha wakati Morrison anasaini mkataba, kamati imesema inafanyia kaza nyaraka na picha haitoshi kuthibitisha.

Kuhusu fedha, Morrison amekiri kupokea dola 25,000 kisha kupokea 5,000 nyingine ambazo amesema atazirejesha Yanga.

> Morrison alisaini kujiunga na Simba Sc akitokea Yanga


==========

Amesikika Mwenyekiti wa kamati ya hadhi na maadili ya wachezaji akisema kwamba, mkataba kati ya Morrison na Yanga ulikuwa una mapungufu na mapungufu hayo yamempa faida Morrison kushinda kesi aliyoipeleka yeye mwenyewe TFF.

1. Kwanza ikumbukwe aliyeshtaki kwa TFF ni Morrison akiamini hakuingia mkataba na Yanga, hapa naamini aligundua mapema mapungufu yaliyopo kwenye makubaliano yao ambayo Yanga waliamini mkataba, halali wakati huohuo Morrison alitumia mapungufu hayo, kuwamaliza Yanga ndani ya masaa 72.

2. Yanga hawakuwa makini kwenye mkataba husika, ambapo yoyote akiona anapata mashaka, kuanzia kwenye tarehe, saini hadi utunzaji wa karatasi yenyewe ulitia shaka hapo ilikuwa rahisi kwa hoja za Morrison kuonekana zina mashiko kuliko za Yanga.

3. Kamati ya usajili ya Yanga ijiangalie kama jambo hili lilikuwa bahati mbaya wasirudie tena...ni aibu kwa klabu kubwa Afrika kama Yanga kutokuwa makini kwenye mambo muhimu kama haya...tena inasemakana mikataba yote haikuwa na viini vya kimkataba vilivyotimia kuanzia ule wa miezi sita na huu wa miaka miwili, ambapo hukumu imejikita kimkakati bila kuidhuru timu Yanga....maana ikijulikana vizuri kuna adhabu Yanga wanaweza kuipata ikiwemo na kushuka daraja kama walivyowahi kufanyiwa Juventus ingawa mazingira ya kesi husika ni tofauti.


4. Kwa utashi wa hali ya juu.....Yanga watulie na wakubali mapungufu madogo yaliyoficha mustakabali mkubwa wa uzembe wa kamati ya usajili na kwa hili wajifunze ingawa naamini kwa ujio wa Senzo haya mambo yatakuwa safi.


Kila la kheri SOKA LA TANZANIA
 
Back
Top Bottom