Morogoro: Watu 22 Wamefariki dunia kwenye ajali ya Basi la Ahmed linalofanya safari kati ya Tanga-Mbeya. Limegongana na Lori

Mkiwa safarini jitahidi Sana kufanya maombi au dua, maombi ni ulinzi tosha dhidi ya watoa kafara. Hapo hata abiria mmoja tu angefanya dua wasingepata ajali.Dua au maombi ya hata msafiri mmoja tu ulificha gari kwenye rada za Wale wapumbavu wa barabarani awalioni na litapita salama kwenye mitego yao ya barabarani.
 
Wakifutwa kazi ndiyo itasaidia nini. Vitendea kazi na mifumo iboreshwe. Huoni ajabu kwanini inashindikana kuweka tochi usiku barabarani
Tochi zinasaidia nini zaidi ya kuwapa rushwa matrafiki? Kinachotakiwa ni kuweka camera barabarani zenye uwezo wa kuchukua matukio yote ya uendeshaji mbovu wa madereva..
 
Mkuu T1 zetu na maisha yetu nadhani unafahamu hao ng'ombe watapita hata pikipiki with cc ndogo, issue ni kwamba hiyo ajali ni uzembe Kati ya bus na IT.
Mkuu ukitaka kufanikiwa ni lazima ujilinganishe na ufanye kama waliofanikiwa, kisheria highways zinatakiwa ziwekewe fence (kazi ya tanroads)na sheria za freeways lazima zifanye kazi, bodaboda zimekaa zaidi kisiasa kuliko kisheria
 
Hapa naona Boda boda ndiye chanzo cha ajali! Dereva wa Lori amekuwa muungwana kumkwepa huyo boda boda,vinginevyo angemgonga tu huyo boda boda kuliko kumkwepa na kusababisha ajali ambayo imepoteza maisha ya watu wote hao!
Anyway ajali haina kinga! BWANA alitoa na BWANA ametwaa.
Jina la BWANA libarikiwe.Amen
 
Zijengwae double roads
Hapa naona Boda boda ndiye chanzo cha ajali! Dereva wa Lori amekuwa muungwana kumkwepa huyo boda boda,vinginevyo angemgonga tu huyo boda boda kuliko kumkwepa na kusababisha ajali ambayo imepoteza maisha ya watu wote hao!
Anyway ajali haina kinga! BWANA alitoa na BWANA ametwaa.
Jina la BWANA libarikiwe.Amen
 
Ajali mbaya maeneo ya Mzumbe maiti ni nyingi.

Walioko Mzumbe tujuzeni basi la Mbeya.

UPDATE:

1). Basi la kampuni ya Ahmed Coach linalofanya safari Kati ya Tanga kuelekea Mbeya, limepata ajali maeneo ya Sangasanga Mkoani Morogoro muda si Mrefu, chanzo na Habari zingine tutatoa baada ya uchunguzi kufanyika.

UPDATES;

2). Watu 13 wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Ahmeed baada ya kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa likisafirishwa kwenda nje ya nchi lenye namba za IT 2816 katika eneo la Melela Kibaoni Barabara kuu ya Morogoro-Iringa.

Kamanda wa Polisi Mkoani Morogoro Fortunatus Muslim amethibitisha kutokea kwa ajalim hiyo.

UPDATES;

3). Morogoro. Vilio na simanzi vimesikika kila kona katika eneo la Malela Kibaoni wilayani Mvomero, Morogoro kufuatia ajali iliyohusisha basi la abiria na lori la mizigo.

Katika ajali hiyo, watu kadhaa wamejeruhiwa wakati lori lenye namba za usajili za IT 2816 lilikuwa likitokea Dar es Salaam kwenda DR Congo kugongana uso kwa uso na basi la kampuni ya Ahmeed lenye namba za usajili T732 ATH.

Akizungumza na Mwananchi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Muslim amesema ajali hiyo imetokea leo saa 10.30 jioni na kusababisha vifo vya watu 16.

Kamanda Muslim amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori hilo kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki maarufu bodaboda hivyo, kupoteza mwelekeo na kukutana na basi hilo uso kwa uso.

Kwa mujibu wa Kamanda Muslim, basi hilo lilikuwa likitokea Mbeya kwenda Dar es Salaam. Miili ya marehemu hao imehifadhiwa kwenye Hospitali ya Mkoa wa Morogoro huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu hospitalini hapo.

Hata hivyo, Kamanda Muslim ametahadharisha kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa kuwa, kazi ya uokoaji bado inaendelea kwenye eneo hilo.
---
Rais Samia Suluhu kupitia akaunti yake rasmi ya Twitter ametoa salamu za rambirambi kufuatia ajali hiyo.

Ameandika

Nimesikitishwa na vifo vya watu 22 vilivyosababishwa na ajali ya basi kugongana na lori katika eneo la Melea Kibaoni, Morogoro.

Nawapa pole wafiwa, nawaombea Marehemu wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka.

Nawasihi watumiaji wa barabara kuzingatia sheria za barabarani.
View attachment 2155817


View attachment 2155660View attachment 2155661
View attachment 2155663
View attachment 2155702
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom