Morogoro: Wanawake wawili mbaroni kwa kukutwa na mikia ya tembo na silaha

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,498
3,465
Wanawake wawili wakazi wa kijiji cha Ikuti Tarafa ya Mwaya wilayani Ulanga wametiwa mbaroni na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro wakikabiliwa na tuhuma za kupatikana na mikia mitatu ya tembo yenye thamani ya shilingi milioni 74.2 na silaha aina ya Rifle 458 ikiwa na risasi moja kinyume cha sheria.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Leonard Paul amewataja wanawake hao kuwa ni Mariam Mata(27) na Maria Mgosanya (35) ambao bado wanaendelea kuhojiwa na Polisi wakitarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kujibu mashtaka yanayowakabili, pindi upelelezi wa shauri hilo ukikamilika.

Katika tukio jingine Polisi wanamshikilia Mkazi wa Mkono wa mara,kata ya Kingoluwira katika Manispaa ya Morogoro Abel Ngaya(49) akituhumiwa kupatikana na noti 4 za bandia kila moja ambayo kama ingekuwa halali, ingekuwa na thamani ya shilingi 10,000.
Kamanda Paul amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa na askari waliokuwa doria,katika maeneo ya Nunge na tukio hilo lilifanikishwa kutokana na taarifa kutoka kwa wasamaria wema.

Chanzo:ITV
 
...........shilingi milioni 74.2 na silaha aina ya Rifle 458 ikiwa na risasi moja kinyume cha sheria.......

Naomba ufafanuzi inakuwaje bunduki kuwa na risasi moja ni kinyume na sheria, mnaomiliki bunduki nisaidieni kiwango cha chini kabisa cha risasi kinayotakiwa kuwa kwenye bunduki, je ni kutokana na kuwa risasi moja siyo kinga tosha dhidi ya adui kwa maana kuwa lazima kuwa na risasi zaidi ya moja kiusalama zaidi?!
 
watu wa kazi wanagawana nao hao hohehahe ndio wanawakamata kusafisha nyota kama kova waqti alipokuwa rpc mbeya kila siku anaonyesha kakamata gobore mpaka akaletwa dar, hili jeshi 97%sio waaminifu ni pesa mbele.
 
Katibu wetu mkuu wa ccm njoo uwatoe ndugu zako huku zana zako za kazi zimekamatwa!
 
Back
Top Bottom