MOROGORO: Wanafunzi wa kike walazimishwa kuzibua vyoo bila ya kuvaa 'gloves'

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
MOROGORO: Mwalimu awapa adhabu ya kuzibua vyoo bila kuvaa 'gloves' Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Sekondari Sua

Mwalimu huyo alichukua hatua hiyo baada ya kubaini vyoo vya shule hiyo vimeziba kutokana na Wanafunzi hao kutupa taulo za kike katika matundu ya vyoo hivyo

Wanafunzi hao wamelalamikia kitendo hicho kwakuwa si cha kiungwana, kimewaathiri kisaikolojia pia ni hatari kwa afya zao

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Manispaa ya Morogoro, amesema kuwa alifika shuleni hapo na kumuhoji Mwalimu anayetuhumiwa kutenda kitendo hicho pamoja na uongozi wa shule

Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kumwambia Mwalimu huyo aandike barua ya kuomba kuhama kwa gharama zake mwenyewe
 
Attachments

  • IMG_20180520_072239.jpg
    IMG_20180520_072239.jpg
    221.1 KB · Views: 42
Inaelekea hao wadada wanaziba sana chemba za Vyoo ......kwa kutupa takataka Acha wasomeshwe # tu hakuna namna

Ova
 
Aiseee. Adhabu zinakubalika ila hazitakiwi kuwa hatarishi kiasi hicho.
 
MOROGORO: Mwalimu awapa adhabu ya kuzibua vyoo bila kuvaa 'gloves' Wanafunzi wa Kike wa Shule ya Sekondari Sua

Mwalimu huyo alichukua hatua hiyo baada ya kubaini vyoo vya shule hiyo vimeziba kutokana na Wanafunzi hao kutupa taulo za kike katika matundu ya vyoo hivyo

Wanafunzi hao wamelalamikia kitendo hicho kwakuwa si cha kiungwana, kimewaathiri kisaikolojia pia ni hatari kwa afya zao

Kwa upande wake Afisa Elimu wa Manispaa ya Morogoro, amesema kuwa alifika shuleni hapo na kumuhoji Mwalimu anayetuhumiwa kutenda kitendo hicho pamoja na uongozi wa shule

Hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kumwambia Mwalimu huyo aandike barua ya kuomba kuhama kwa gharama zake mwenyewe
 
Gazeti la Mwananchi Jumapili: limeandika kuwa "MWALIMU WA SHULE YA SEKONDARI SUA MKOANI MOROGORO, ANADAIWA KUWAPA WANAFUNZI WA KIKE ADHABU YA KUZIBUA CHEMBA YA CHOO BILA KUVAA GLOVU, NA KUKAMUA TAULO ZA KIKE WANAZODAIWA KUZITUMBUKIZA CHOONI BAADA YA KUZITUMIA"

Kabla ya kuwalaumu walimu tuwaulize hao wasichana kuwa walitaka wanaume waziondowe pedi zao zilizoziba chemba? Hilo liwe funzo kwao watafute njia nzuri ya kuziteketeza pedi zilizotumika. Wameondolewa balaa la kukosa masomo wakati wa siku zao, badala yake iwe balaa kwa wanaume! Haiwezekani.
 
Inatakiwa wawe na sanitary bins kwenye vyoo, pia wapewa elimu kuhusu wapi kuzitupa hizi taulo.

Hii adhabu inaweza kuhatarisha maisha ya wanafunzi.
 
Dah kama anaomba kuhama si atachagua mwenyewe shule ya kwenda?
Hiyo inaweza kuwa poa zaidi kwake maana anaweza kuamua tu Mzumbe,
Ilboru n.k
 
u
Kwanini ana hamishwa? Afisa elimu wetu akiri zao hazinaga tofouti na baadhi ya waalimu wa shule za msingi
ulitaka afanye nini? nijuacho mimi ni afisa elimu anafanya kazi kwa kufuata sheria na siyo hisia zake
 
Si wanafanya wao na wanatumika wao kufanya usafi.

Watafikiri na kushauri suluhisho bora.
Ooh. Kama ni wote hapo sawa ila pia inatakiwa iangaliwe na adhabu ya kukomesha na sio kusema eti umzibulishe mtoto choo kwa kutumia mikono yake pasi kinga yeyote.

Ni kiasi cha walimu kujiongeza tu Mkuu.
 
Back
Top Bottom