Morogoro: Wabunge Peter Lijualikali & Suzan Kiwanga wa CHADEMA wanatafutwa na Polisi kwa udi na uvumba

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Polisi Mkoa Morogoro wanawashikilia wanachama 7 katika ya 13 wa CHADEMA walioachiwa na Mahakama Januari 2019, baada ya Polisi kushindwa kuwasilisha ushahidi. Wabunge Peter Lijualikali & Suzan Kiwanga bado wanatafutwa, na polisi wamesema sasa hivi wana ushahidi na vielelezo vyote.


======

Morogoro. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema jeshi hilo linawasaka wabunge wawili wa Chadema, Peter Lijualikali (Kilombero) na Suzan Kiwanga wa Mlimba.

Wabunge hao walikuwa miongoni mwa wanachama 13 wa Chadema walioachiwa huru na mahakama mkoani humo Januari 2019.

Waliachiwa huru kupitia kifungu cha Sheria namba 225 cha mwenendo wa makosa ya jinai baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yanawakabili, ikiwa ni pamoja na kuchoma moto ofisi ya Sekondari ya kijiji cha Sofi Wilaya ya Malinyi.

Siku chache baada ya kuachiwa huru, polisi leo Jumatano Februari 20, 2019 imeeleza kuwa imewakamata wanachama saba kati ya 13.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Mutafungwa amesema miongoni mwa wanachama wanaowatafuta ni wabunge wa chama hicho.

Amesema hivi sasa wamejipanga kwa kuwa na ushahidi na vielelezo vya kutosha vya kuwatia hatiani.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Kiwanga amesema mahakama ilishindwa kuwatia hatiani kwa sababu polisi waliandaa ushahidi wa kupika na walishindwa kupeleka mashahidi wote mahakamani kama walivyokuwa wameahidi.

"Mimi nipo mbali lakini nimemtuma kiongozi mmoja wa chama kufuatilia. Polisi wamewakamata wenzangu kwa kuwavamia na kuwavizia majumbani jambo ambalo sio la kistaarabu wakati wangeweza kuwapelekea hati ya wito na wakaenda wenyewe" amesema Kiwanga.
 
Lijualikali yupo kimya sana yaani hata bungeni hasikiki amepatwa na nn huyu jamaa?
 
Mamaa! wanarudisha korosho Mtwara, Morogoro wapo bize na Chadema! Tutaponea wapi?
 
polisi waliandaa ushahidi wa kupika na walishindwa kupeleka mashahidi wote mahakamani kama walivyokuwa wameahidi.

Tunaposema polisi wetu wanatumiwa na wanasiasa hatueleweki

Sasa tutaamini vipi kama ushahidi walionao sasa ni wa kweli
 
Siku mzee Nelson Mandela alipokuwa akiapa kuwa rais wa Africa ya Kusini polisi wengi sana wa kikaburu walijiuuzulu. Maana walichanganyikiwa, watu waliokuwa wakiwakandamiza leo ndio wanawatuma..

Polisi wetu nanyi mjifunze, Hawa mnaojaribu kuwakandamiza watakuja kuwa maboss wenu baadae. Mtakimbilia wapi?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi za Kiafrika ukiwa mpinzani tu unachukuliwa kama mhalifu wa kiwango cha juu kbs na unaweza kufanyiwa chochote wewe na familia yako ilihali huna sheria uliokiuka au kuvunja kipengele chochote cha katiba. Tukiitwa "anasi" tunalalamika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom