Morogoro: Viwavi jeshi vyateketeza heka 20 za mashamba ya mahindi Mvomero

View attachment 780674
Zaidi ya hekta Elfu ishirini sawa na ekari elfu hamsini za mashamba ya mahindi ya wakulima wadogo katika vijiji vya wilaya ya Mvomero zimeteketezwa kwa kuliwa na wadudu waharibifu wa mimea aina ya Viwavi Jeshi vamizi Fall Armyworm.

Baadhi ya wakulima ambao mashamba yao yamevamiwa na Viwavi Jeshi vamizi wanasema wamepata hasara kubwa katika msimu huu wa kilimo hali iliyowakatisha tamaa ya kuendelea na shughuli ya kilimo .

Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wilaya ya Mvomero Daina Mnywanga anasema tatizo ni kubwa.

Baada ya kutembelea eneo lililoathirika na kutoa elimu kwa waafisa ugani wakulima pamoja na wakala wa pembejeo za kilimo mtafiti wa wadudu waharibifu na viutilifu kutoka TPRI anasema hadi sasa zaidi ya mikoa kumi na sita imesha athirika na wadudu hao na kwamba tpri imeshapata viuatilifu vyenye uwezo wa kuua wadudu hao na wanaendelea kutoka elimu.

Chanzo: Nipashe
Mfumo wetu wa response to disasters ni duni sana,ila nahisi hata wataalam wetu wa kilimo nao utaalam wao ni mdogo pia.Zipo scientific approaches za kuweza kujua kwamba Maize Stalk Borers watakuwepo au hawatakuwepo mapema.Now, why monitoring and also scouting was not done early in the season is difficult to tell. Hii ingewawezesha wakulima na wataalam kujua kama wadudu hao watakuwepo au hawatakuwepo mapema ili waweze kujiandaa kwa madawa na mikakati.

Jambo la ajabu ni kwamba,hata wadudu walipokuwa tayari wapo mashambani,mchango
wa viongozi wa ngazi zote,upande wa kilimo na kisiasa was almost absent
. I had expected kwamba baada ya kuliona tatizo,viongozi wote wa kisiasa na wa kilimo wangeshirikiana kulitatua.Unfortunately that was not the case. Wakulima tuliachwa to fend for ourselves.Aibu sana.

Finally niseme kwamba ni kweli damage kwa Wilaya ya Mvomero kwenye zao la mahindi ni mkubwa.Hata hivyo hii imesababishwa zaidi na uzembe wa watendaji,kwa kuwa technologies zipo ambazo zingeweza kupunguza sana crop loss.

Kwa jinsi hali ilivyo,ni vema serikali ikajiandaa mapema kutoa msaada wa chakula kwa wakulima wa Wilaya ya Mvomero.
 
Si wawapeleke wavunja matofari wawape dozi sawa sawa. Ama hawa viwavi jeshi ni imara sana?.
 
Back
Top Bottom