Morogoro: Viongozi wa CHADEMA wakamatwa na polisi, vurugu zaibuka!

AdvocateFi

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
11,492
5,040
Mida hii nikiwa hapa morogoro mjini msamvu ambapo polisi wamewatia mbaroni viongozi wa CHADEMA akiwemo na BENSON KIGAAlA.

Subirieni taarifa zaidi.

Habari kutoka Morogoro zimetufikia hivi punde kutoka chanzo cha uhakika nguvu ya umma imeshinda watu wanaendelea na maandamano baada ya Mabomu kushindwa kutawanya watu. Hali ni tete polisi wamelegea mabomu yamewaishia watu wanasonga mbele

Ni kweli. Polisi wamevuruga maandamano yaliyokuwa yafanyike kwenda eneo la mkutano, Uwanja wa Ndege, hapa Morogoro Mjini. Wamedhalilisha viongozi waliowakamata na sasa wameanza kuomba samahani, yaishe.

Kamanda wa Polisi Morogoro, Shilogile (mnaojua alihamishwa Dar es Salaam kuja hapa...) amevunja makubaliano yaliyofanyika mara mbili ya kuruhusu maandamano. Tunajua wapo wanasiasa hapa Morogoro ambao hawataki meseji ifike leo kwa wakazi wa Morogoro Mjini.

Inajulikana namna ambavyo CCM wamekuwa shaken big time na operesheni iliyokuwa na mafanikio huko vijijini, itawaumiza zaidi ikifanikiwa hapa mjini. Kwa hiyo lengo hapa si kuvuruga tu maandamano, bali ni kuvuruga mkutano, ili hatimaye watu waogope kuja mkutanoni, ujumbe usifike. Hawatafanikiwa kwa hilo, maana wananchi sasa wanazidi kujikusanya, maeneo kama ya Masika, kwenda eneo la mikutano, kwa maandamano.

Polisi wanachafua mji sasa, polisi wanawapitisha wana-Morogoro kwenye tanuru ambalo watu wa Mwanza, Mbeya, Arusha, Moshi, Musoma, Tarime, Ruaha na kwingineko kwingi, walipita/kupitishwa ili kuwa hapo walipo wakiwa na imani isiyoyumba katika mapambano haya ya kudai na kuwaandaa Watanzania kwa mabadiliko makubwa ya kimfumo na kiutawala. Chuma hakiwezi kuwa chuma mpaka kipite kwenye tanuru, lakini why doing it unnecessary?

Tutawapatia more updates on the issue?

Nguvu ya umma imeshinda mabomu ya polisi na mabavu ya polisi. Watu wameandamana na tayari wameshakusanyika eneo la mkutano, Uwanja wa Ndege. Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Hamad Mussa Yusuf naye alikamatwa, lakini wamemwamchia. Bado wanamshikilia Kigaila, hawataki kumpeleka kituoni, badala yake wanazunguka naye ndani ya gari. Pia walimkamata mwandishi mmoja wa habari, kwa kupiga picha (sijui ni kosa?????), lakini naye pia wamemwachia.

Taarifa ambazo nimeweza kuzithibitisha ni kuwa kuna watu watatu wamepigwa risasi, ni risasi za moto. Mmoja amekufa baada ya risasi kumpata kichwani, anaitwa Ally Zona; wengine wawili wamelazwa hospitali ya Mkoa wa Morogoro.

I'll keep u updated wakuu, for anything good or bad...

Habari za uhakika ni kua polisi wameua mtu maeneo ya Msamvu bila sababu ya msingi,kisa ni kua walikua tu wanajaribu kuzuia maandamano ya Cdm na kijana huyo aliyekua akiuza magazeti aliwaonyesha alama ya V ndipo walipomlipua! My take: ni wazi jeshi la police chini ya IGP Mwema limeshindwa kuwalinda raia na mali zake,na kuwachukulia hatua wezi wakubwa na wahujumu nchini,bali jeshi la polisi limegeuka kua la mauaji kwa raia wasio na hatia kwa jinsi watakavyo! Source: mimi mwenyewe nipo kwenye mkutano hapa Morogoro

=====================
MATUKIO KATIKA PICHA
=====================




Wafuasi wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema

Askari waliokuwa katika eneo la tukio kabla ya kuanza kwa maandamano hayo

Moshi wa mabomu yaliolipuliwa kutawanya maandamano ya chadema leo mjini morogoro




Gari la chadema lililokuwa likiongoza maandamano hayo

Mmoja wa kiongozi wa chadema akiwa amekamatwa akiwa ndani ya gari la polisi

Wafuasi wa chadema wakiwa na maandamao hayo mjini morogoro



============================
Marehemu Ally Zona [R.I.P Kamanda]
============================



Kijana Ally muuza magazeti aliepingwa risasi ya moto kichwani... RIP Ally....



==================
MMOJA WA MAJERUHI
==================

images
 
Hivi viongozi wa nchi hii ni wasomi kweli na ni watu wenye kuona mbali?

Hivi raisi kweli huwa anapima ushauri anaopewa na wasaidizi wake?

Hivi ushauri bora ni kuzuia maandamano kwa risasi au kuacha watu waandamane na kuwapa ulinzi?

Kuua raia kwa risasi,ccm na chadema yupi mwenye hasara hapo kama sio ccm?

Tangu lini risasi za moto zikashinda nguvu ya umma?CCM hamjifunzi kwa yanayotokea nchi za wenzetu?

Raisi Kikwete hutambui kuwa 2015 wana ccm watakulaumu wewe na wala si washauri wako?

Raisi Kikwete hutambui kuwa wanaokuunga mkono leo kesho mambo yakiharibika watakugeuka na utabeba lawama peke yako?

Tafakari waliokuwa wanakushauri juu ya katiba mpya kama mfano mmoja tu na alafu ujiulize kama kweli una washauri wazuri na unaopaswa kuendelea kuwa nao mpaka leo

Raisi Kikwete tafakari sababu zilizokupunguzia kura kutoka aslimia 80 mpaka 60 kama mpake leo hii umezifanyika kazi au ndio zinazidi kuongezeka

Hivi leo hii nani asietambua ukweli kuwa chadema kimelenga kutetea maskini na ccm kimelenga matajiri wachache?

Mwisho mjiulize nchi hii wengi ni matajiri au maskini?

Sintashangaa na ninaomba chadema wachukue nchi hii 2015 alafu muje kuwajibika kwa mauaji haya.
 
Senzi sana...wanataka nini hao?
Lete taarifa iliyosheheni na picha ikiwezekana ili tujue kwa undani wanakwamisha M4C kwa sababu zipi!
 
Huwa nalishangaa sana jeshi la polisi linapokuja swala kama hili. Wamefanya makosa gani?
 
Kuna picha tatu zinazua maswali:

1. Picha moja inaonesha wakina mama wanakimbia na hawaonekani kama wana silaha yoyote. Mama/binti mmoja anakimbia huku akiwa amembeba mtoto mdogo!

2. Picha nyingine inaonesha gari jeupe likiwa na bendera za CHADEMA na nyuma yake kuna gari la polisi. Ukitazama vizuri utaona (very clearly) askari wawili wakiwa wamelekeza mitutu yao upande wa abiria aliyeko kwenye gari lililo na bendera ya CHADEMA! Abiria anaonekana kunyoosha vidole na hana silaha, askari on the other hand wana silaha - na sasa tunajua ni za moto maana kuna fatality.

3. Picha ya marehemu inaonesha kama amepigwa risasi kichwani kwa nyuma, that means askari alikuwa nyuma yake. huyu kijana alikuwa threat kwa vipi wakati alikuwa hatazamani na aliyekuwa ameshika silaha iliyomuua?

Jambo ambalo sijaelewa ni busara inayotumiwa na viongozi wa nchi hii hasa polisi. Kwa muda sasa raia wamekuwa wanapambana na jeshi la polisi na licha ya mauaji yanayofanywa na jeshi la polisi bado raia hawaonekani kutishika. Raia wanajua fika kuwa askari wa Tanzania wanatumia silaha za moto na muda wowote wanaweza kuua lakini hili halijabadilisha msimamo wao (wananchi). Arusha, Songea, Mbeya na sasa Morogoro, infact leo wameuwa lakini raia hao hao walionusuruka wamehudhuria mkutano.

Kwa akili ya wastani tu viongozi wanatakiwa kukubali ukweli. Maji ya washawasha, mabomu na hata risasi za moto hazitabadilisha msimamo wa raia. Na tukiendelea na mtindo huu mioyo ya wananchi itazidi kuwa migumu - watajihami!!!
 
Wakati tunasubiri taarifa kamili bora tuanze kuwapa pole polisi wetu wana maisha magumu hawathaminiwi ila wanatumiwa kama vile wao wanavyowatumia wale mbwa wao kwenye vurugu kuwalazimisha wamng'ate mtu asiyekuwa na hatia nao hulazimishwa kuwakamata hata wale wanaojua ni watetezi wao.
 
asubuhi nilisikia kwenye radio kuwa hawaruhusiwi kufanya maadamano kwenda katika mkutano C4M labda ndo sababu
lakini hii sababu ilishindikana Dar kwa sababu si lazima kwa wanachama kupanda daladala kwenda katika mikutano
 
Haya mambo ya kukaa kwenye keyboard na kuwaachia wachache watupiganie kutukomboa itachukua muda sana nchi hii kukomboka,shime makanda wa Morogoro,twendeni kituo cha police tukajue ni nini kilichojiri,nasikia msamvu nako wanapga mabomu ya machozi,always polisi uwa ndio waanzisha fujo!nidhamu ya uoga bila ujasiri na maneno matupu ya pembeni ni,nasari anasisitiza watu kwenda kituo cha polisi,naelekea huko
 
polisisiem kazini...nawashanga sana hawa jamaa,wanapelekwa tu kama mang'ombe wakati wanamatatizo kuanzia wanapolala paka wanapoamka..nilidhani wangeisapoti chadema ili iwakomboe...
 
Nipo ndani nasikia mabomu ya machozi yanapigwa maeneo ya msamvu. Sijapata kujua ni kwanini ? najaribu kufuatilia ili kujua lakini mwenye taarifa anaweza kutujuza
 
Nimelazimika kuja kwenye thread hii kwa uchungu mkubwa wa jinsi ya vyombo vya dola "The coerisive instruments" hasa hawa police wanavyotekeleza maagizo ya watawala ya kuzima demokrasia hapa nchini Tanzania. Kimsingi nguvu na mabavu ya dola huegemewa na Viongozi wa serikali zilizokosa uhalali wa kutawala kama kinga ya wao kuendelea na uovu wao.

Ni muhimu kujikumbusha Rais kikwete alisema nini mwaka 2011 baada ya mauaji ya Arusha, Kikwete akiongea na Dunia kupitia Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania pale ikulu alisema, namnukuu " The curent Arusha killings is the case in Point, I'll make sure tha it w'll not happen again" .

Kikwete alizungumza kama Amiri jeshi mkuu akimaanisha amri ya kuua au kutokuua inatolewa na yeye ; tujiulize swali, je leo Kikwete anapata wapi " moral authority '' ya kuiambia dunia na watanzania kuwa mauaji yaliyotokea leo Mkoani Morogoro ni bahati mbaya ? Achilia mbali mauaji ya Ruvuma yaliyopoteza maisha ya wananchi waliokuwa na matawi ya majani mikononi kwe maandamano.

Ni muhimu pia kujua kuwa Mizengo Pinda aliliambia bunge kuwa watanzania hawatendelea kuuwawa tena na jeshi la police , sasa basi kama Rais na Waziri mkuu wanasema HAKUNA TENA{no more} mauaji ; IGP,RPC,OCD wanaagizwa na nani? Au military phsychology na mafunzo waliyopata kupiga na kuua yanawasumbua, ? Kama hivyo ndivyo au sivyo viongozi hawa watafakari kisha Wajiuzulu kama Lowasa.
 
Bila shaka RPC wa hapo ni miongoni mwa wale wanaojipendekeza kwa watawala dhaifu,si huyo huyo alizuia uzinduzi wa M4C usifanyike hapo moro mjini badala yake ukafanyikie mikumi,sasa anataka kutumia mbinu hiyohiyo kuzuia na huo mkutano,hivi kupiga watu na mabomu ambao hawajaleta vulugu kunafaida gani zaidi ya kutumia kodi za wananchi vibaya kununulia hayo mabomu,upuuzi sana huu
 
taarifa zilizopo ni kuwa CDM walipewa eneo la 'fire' kwa ajili ya mkutano wao, sasa wakaanzisha na maandamano, jambo ambalo nafikiri limewalazimisha polisi kutumia nguvu.
 
Back
Top Bottom