Morogoro: Vifo vitokanavyo na ajali za barabarani vyapungua kwa asilimia 25

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,406
2,000
Vifo ajali barabarani vyapungua 25%

Vifo vinavyotokana na ajali za barabarani mkoani Morogoro vimepungua kutoka 90 mwaka 2019 hadi 57 mwaka jana, sawa na asilimia 25.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilimu, alisema jana kuwa vifo hivyo vimepungua kutokana na elimu inayoendelea kutolewa kila wakati kwa madereva wa malori, mabasi, teksi, wanafunzi na magari binafsi.

Alisema mwaka 2019, ajali 75 zilitokea na kati ya hizo, 67 zilisababisha vifo 90 na majeruhi wakati mwaka jana, ajali 54 zilitokea na kusababisha vifo 57 vilivyotokana na ajali 37 kati ya ajali zilizotokea.

Kamanda Musilimu katika kuhakikisha ajali hizo zinapungua, Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa, lilitoa elimu kwa abiria wa mabasi 3,600, madereva 2,000 wa pikipiki, wanafunzi 4,000 kwa kila mwezi mkoa mzima kutokana na kuweka vipindi maalum vya elimu ya usalama barabarani shuleni na kwa madereva wa magari binafsi na daladala wapatao 3,600 kila mwezi.
 
brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
6,902

Muslim bado anaota mambo ya usalama barabarani.

Bado hajaamini kuwa si kamanda mkuu wa usalama barabarani tena.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom