Morogoro: Stand ya Daladala kuhamishiwa kilomita 2+ kutoka katikati ya mji ni kero kwa Wananchi

Hii ni kero na si maendeleo. Kwa mfano mtu unatoka Kihonda kuelekea Hospitali kubwa kuna ulazima gani wa kwenda kupelekwa huko stand pembezoni ya mji?

Nashauri stand ya Bajaji ingeachwa iendelee pale mjini, au kuwe na vituo vya Hice karibu na Hospitali kubwa ya Mkoa na pale masika kile kituo cha Hice kiendelee kuwepo.
 
Wanapeleka kalibu na viwanja vyao, huu ni ujinga kabisa na ni kama serikali pia haina mipango ya mda mrefu, yani kimji kama Lamadi ya Mwanza pia wanaamisha wakati stendi ndo imechangamsha mji
ukweli ni kwamba ile stendi ya pale mjini Morogoro... ilikuwa ni kero kwa watumiaji wa barabara za Boma pamoja na hii ya madaraka, ile iendayo halmashauri na ile iendayo masika... na tukumbuke pia daladala zinazidi ongezeka... fujo zitapungua kwa kuihamisha hiyo stendi
 
Hii ni kero na si maendeleo. Kwa mfano mtu unatoka Kihonda kuelekea Hospitali kubwa kuna ulazim gani wa kwenda kupelekwa huko stand pembezoni ya mji?.

Nashauri stand ya Bajaji ingeachwa iendelee pale mjini, au kuwe na vituo vya Hice karibu na Hospitali kubwa ya Mkoa na pale masika kile kituo cha Hice kiendelee kuwepo.
Stendi ya hice ukaiweke karibu na hospitali? Mpango upo vizuri na umesimama. Palikuwa na fujo sana pale
 
Hii ni kero na si maendeleo. Kwa mfano mtu unatoka Kihonda kuelekea Hospitali kubwa kuna ulazim gani wa kwenda kupelekwa huko stand pembezoni ya mji?.

Nashauri stand ya Bajaji ingeachwa iendelee pale mjini, au kuwe na vituo vya Hice karibu na Hospitali kubwa ya Mkoa na pale masika kile kituo cha Hice kiendelee kuwepo.
Kituo cha Masika opposite na NMb kimefungwa? Ila kwa kile cha mjini kilikuwa kimebanana sana. Lakini kukipeleka Mafiga nako ni mbali sana
 
Kituo cha Masika opposite na NMb kimefungwa? Ila kwa kile cha mjini kilikuwa kimebanana sana. Lakini kukipeleka Mafiga nako ni mbali sana
automatically... kuna root zinaweza kuongezeka ama kuna vituo vinaweza vinaongezeka... mfano root ya kihonda mjini... inaweza ikawa Via kihonda magorofani kuja ipoipo, ama kupitia yale mataa ya msamvu shule kuja tumbaku, ama kupitia masika kuja sabasaba,
mwanzo zitasumbua... lakini watu wakizoea kila kitu kitakuwa sawa
 
Lakini pia kuna watu wa bajaji nadhani hili la kuhama stendi pia limewaletea fursa.
 
Kuhamisha stand haiepukiki, ni moja ya matokeo ya maendeleo na ukuaji wa miji.

Ya Dar es salaam ilikua kisutu, ikahamia ubungo zilikua km9 toka mjini. Sasa imetoka ubungo imepelekwa mbezi Luis km26 toka mjini na bado watu wanadunda tuu

Usiogope mabadiliko

Mama wewe unazungumzia stendi za mabasi tena ya kwenda mikoani. Hapa watu wanazungumzia stendi ya daladala!
 
Kituo cha Masika opposite na NMb kimefungwa? Ila kwa kile cha mjini kilikuwa kimebanana sana. Lakini kukipeleka Mafiga nako ni mbali sana
Kituo kilichoachwa ni kile cha Hice za kwenda Mikese tu. Hice zote na Bajaji zimeelekezwa kwenda kituo cha Mafiga hivyo kumeongeza kero kwa watu wanaoenda maeneo ya mjini kati.
 
Hata ubungo Tanesco pale chini palikua na Stendi ya Daladala sahivi iko mbezi Luis kitambo sana pale pamebaki gofu tuu

Na mwendokas itafik kibaha
Niliandika hivi

"Ni jambo jema kuboresha huduma kwa jamii kutokana na kukua kwa mji, lakini viongozi wa jambo husika hawakaushirikisha mawazo ya wananchi katika kufikia maamuzi ya jambo walilofanya."

Hapajawepo utaratibu wa kuwarahisishia wananchi kushuka katikati ya mji hasa wale watokao Bigwa, Kihonda, na Tungi
 
Huu mtindo wa hovyo mno , ina maana kila stend ikibanana mnahamisha , ikibanana tena mnahamisha mwisho watafika Dodoma au Iringa Kwa kuhamisha hamisha , Kwa nn wasijenge nyingine karbu wakatenganisha Tu route , huku zikabaki za kwenda kule na stemd mpya zikabaki za route nyingine kuliko kupeleka watu pori
Sio tu Morogoro hata Dar-es-Salaam vituo vya mabasi yakwenda Mikoani na nchi jiani.

Kujenga kituo kikuu cha mabasi kwenda mikoani Mbezi,wasiondoe vituo vingine katika maeneo mengine. Kwa mtu anaenda Lindi au Mtwara wajengewe maeneo ya kuelekea Kilwa Road.

Sana sana ikibidi kupitia Morogoro road kuelekea mikoani ndipo basi ipitie tu kama kituo kikuu tu.

Sisi wasafiri msitugeuze watumwa ,au mradi.Nimegundua vituo vingi vikubwa vilivyojengwa na serikali licha ya kuwa na maeneo makubwa na majengo yanayovutia lakini hawatilii maanani huduma kama Vyoo.

Vyoo mara nyingi having usafi wa kuridhisha,ni kero. Kama tungekuwa wakali kwa hilo karibu vituo vingi vingefungiwa.
 
Daladala zilikuwa zinaleta kero pale kwa watumiaji wengine wa barabara

Ni kweli lakini isiwe hukumu kwa wananchi wengine kwasababu tu madereva wa daladala walikuwa wankiuka sheria, iafutwe namna ya kuwashusha abiria katikati ya mji kabla daladala hazijaendelea na safari kwenda stand mpya.
 
ukweli ni kwamba ile stendi ya pale mjini Morogoro... ilikuwa ni kero kwa watumiaji wa barabara za Boma pamoja na hii ya madaraka, ile iendayo halmashauri na ile iendayo masika... na tukumbuke pia daladala zinazidi ongezeka... fujo zitapungua kwa kuihamisha hiyo stendi
Tatizo la Mprogoro barabara ni finyu mno. Kama ile barabara ya Masika kuja hapo stendi na ile ya kutoka Manispaa hadi roundabout ya Sua zingeongezwa ili zikidhi mahitaji. Hii idea ya kuhamisha stendi kupeleka kijijini haina mantiki kabisa.
 
Nashauri magari yaruhusiwe kushusha na kupakia abiria katikati ya mji bila kufanya maegesho ya zaidi ya dakika
Hili ndio la muhimu,stand waipeleke hata mzumbe,ila abiria akifika ilipokua stand ya mwanzo akiomba kushushwa

ashushwe,na hao wengine wanaoendelea na gari hadi mwisho stand wataendelea ila muhimu ni ruhusa itolewe ya

abiria kushushwa/kuteremka mahali alipopazoea mwanzo,stand kuhamishwa ni halali stand nyingine ziliibuka tu lakini

haukua mpango kwamba stand iwe eneo hilo,kwahiyo muda huu ambao ndio nchi inapangwa watu wawe tu wavumilivu.
 
Tatizo la Mprogoro barabara ni finyu mno. Kama ile barabara ya Masika kuja hapo stendi na ile ya kutoka Manispaa hadi roundabout ya Sua zingeongezwa ili zikidhi mahitaji. Hii idea ya kuhamisha stendi kupeleka kijijini haina mantiki kabisa.

Wangetoa miongozo kuwa daladala zipite njia gani kuelekea kwenye hiyo stand, ilivyo kwa sasa nyingi ya daladala za Tungi na Kihonda zinashushia abiria Masika ambako ni mbali katika kupata connection na route zingine kama Bigwa nk
 
Basi kama vp wahamishe stendi lakini wasiue kabisa route ya kwenda mjini kati. Sasa kama mtu anatoka Lukobe anafanya kazi AgaKhan inakuwaje?
 
Basi kama vp wahamishe stendi lakini wasiue kabisa route ya kwenda mjini kati. Sasa kama mtu anatoka Lukobe anafanya kazi AgaKhan inakuwaje?

Au anaishi Lukobe anafanya kazi Kilakala, maana yake ashushwe Masika kisha atembee kwa miguu hadi mjini kati mwendo wa dakika 10++
 
Back
Top Bottom