Faana
JF-Expert Member
- Dec 12, 2011
- 31,685
- 32,993
Ndugu wanajamvi,
Nimefika mjini Morogoro kwenye hekaheka zangu nikashangazwa na kitendo cha kuhamishia stand ya daladala kutoka katikati ya mji na kuipeleka karibu na Chuo Kikuu cha Sokoine umbali wa kama Km 2+.
Ni jambo jema kuboresha huduma kwa jamii kutokana na kukua kwa mji, lakini viongozi wa jambo husika hawakaushirikisha mawazo ya wananchi katika kufikia maamuzi ya jambo walilofanya.
Daladala zinazoingia na abiria waendao kufuata mahitaji katikati ya mji wanashushwa mbali na mji na kulazimika kukodi bajaji na pikipiki ili wafike katikati ya mji kitendo ambacho kinawaongezea gharama wananchi ambao wengi wao ni wa kipato cha chini.
Bajaji ambazo ndiyo msaada wa haraka nazo zimeondolewa katikati ya mji na kulazimu wananchi kutembea umbali mrefu kwenda kutafuta usafiri wa kuunganisha ili waende waendako, mathalani mtu atokaye Msamvu kwenda Bigwa analazimika kuchukua pikipiki kwenda mpaka mjini kati ndipo apate daladala ya kwenda Bigwa.
Changamoto ni nyingi sana, nashauri mamlaka husika zishirikishe mawazo ya wananchi ili kuondoa usumbufu unaoendelea kujitokeza mapaka sasa na kuathiri kwa kiasi kikubwa majukumu ya watu na kuwaongezea gharama za maisha wananchi wa kipato cha chini.
Ikumbukwe kuwa maamuzi yalifanywa na viongozi bila kushirikisha wananchi, lakini viongozi hao hawakuvaa viatu vya wananchi husika ili nao wapate feelings ambazo wananchi wanazipata kwa sasa kwakuwa viongozi husika hawatumii daladala, laiti wangekuwa wanatumia daladala wangeona adha hizo na huenda wasingechukua uamuzi waliochukua.
Nawasilisha