Morogoro: Selemani Msindi (Afande Sele) adakwa na kulazwa Korokoroni, mdomo wake wamponza

Kuna watu wanaamini Mungu hayupo, kuna watu wanaamini Mungu yupo. Nani ana mkashifu mwingine? Suruhisho: kila mtu ashikilie imani yake, serikali ishughulike na yule amnyoosheae kidole mwenzake.
Uko sahihi mkuu. Haijawa kashfa as long as unachokiamini unakiweka moyoni mwako. Ukipayuka hadharani ndipo serikali inapoingilia kati kumuingilia mtu/watu wengine katika imani yao/zao.
 
Msanii mkongwe wa muziki, Selemani Msindi maarufu Afande Sele, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mjini Morogoro kwa mahojiano baada ya video yake iliyokuwa na maudhui ya kumlaumu Mwenyezi Mungu kwa kile alichodai hakutenda haki kuruhusu kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli.

Hivi karibuni Afande Sele alisikika akimlaumu Mungu kuruhusu Magufuli afe.

Mkuu wa Polisi Morogoro kasema kesho ataongea kinagaubaka sababu za kumkamata na kumlaza Korokoroni.

Zaidi soma: Afande Sele (Seleman Msindi), asomewa dua ya kufa kabla ya Ramadhan ya 2021 kufika, atuhumiwa kumkufuru Mungu

View attachment 1732037
Hapo Selemani Msindi alias afande Sele amekamatwa kwa kosa lipi na atashitakiwa kwa kosa gani na mlalamikaji ni nani?

Je, aliyelalamikiwa atajitokeza kuthibitisha kwamba ametendewa kosa?

Je, Jamhuri ya Tanzania inaweza kuchukua jukumu la kumshitaki mtu aliyetenda DHAMBI?

Je, kuna rejea yoyote ya hukumu ambayo serikali iliwahi kumwakilisha Mungu wakilalamikia kutendewa DHAMBI na nani alishinda?

Mahakama inakiri uwepo wa uwepo wa Mungu kwa nadharia ya kwamba kuna baadhi ya matukio pamoja na utalaamu wa binadamu hawezi kuzuia kama kifo (nani alishawahi kukata ryfaa dhidi ya kifo?)

Msanii afande Sele amefanya kosa la kimaadili ambalo msingi wake umetokana na kukashifu uwepo na uwezo wa Mungu baada ya kuacha kuzuia tukio fulani lisitokee;

Je, wafahamu kuwa ni kwanini waliokufa hawarudi, na hata waliowahi kupoteza fahamu kwa imani wakapelekwa mahali ambapo baada kuonesha kilichoko huko walikataa kurudi lakini walishurutishwa kurejea ambayo huitwa ufufuo wa mfu (muujiza)?

Kesi inayomhusisha Mungu ni ngumu kwa mahakama kuitolea uamuzi kwa kuwa Mungu hawezi kuhudhuria mahakamani kati umbo la binadamu kutoa ushahidi dhidi ya tuhuma.

Huko Marekani kuna mzungu mmoja (State Senate Ernie Chambers) aliwahi kumshitaki Mungu mahakamani na akadai fidia kutokana na imani aliyohubiriwa kutomsaidia.

Uamuzi wa mahakama ulitupilia mbali kesi hiyo kwa sababu baada ya mlalamikaji aliyepewa hati ya kumkamata alishindwa kumpata ili amkabidhi wito wa mahakama.

[Huyo aachiwe ila aonywe na kupewa nasaha za kisaikolojia kutokana na mfumo wake wa maisha umeathiri fikra, huenda akwa ndiye imamu au mhubiri mzuri kusaidia wengine]
Reference attached.
 
Attachments

  • Ernie Chambers Sued God in USA.pdf
    1.2 MB · Views: 5
Tatizo sio kuamini. Mungu.
BALI KUMTUKANA.
Swali kwanini UMTUKANE?
unajua mbingu na ardhi ni MALI YA NANI?
Ndiyo nakumbaaje. Kama wewe na mimi tunamwamini Mungu lakini kuna wengi wanaona Mungu ni kitu cha kufikirika. Yaani hayupo kabisa. Hili ni suala la mtu binafsi na Mungu wake. Siyo suala lako wala langu wala la serikali. Kama ni adhabu ataipata yeye na siyo wewe wala mimi. Huu ndiyo uhuru wa kuabudu. Huyu siyo binadamu wa kwanza kufanya hili. Kwenye vitabu vitakatifu kuna mifano kede ya watu waliokuwa wanamhujumu Mungu. Mungu anajua namna ya ku-deal nao. Siyo kazi ya serikali. Jamaa hajakashfu dini yoyote bali amesema haamini kama Mungu yupo.
 
Uko sahihi mkuu. Haijawa kashfa as long as unachokiamini unakiweka moyoni mwako. Ukipayuka hadharani ndipo serikali inapoingilia kati kumuingilia mtu/watu wengine katika imani yao/zao.
Kupayuka hadharani namna gani? Mbona wanaoamini kuna Mungu kila siku wanapayuka hadharani kwa mahubiri na kila aina ya mawasiliano? Huoni hata wao wanaingilia uhuru wa wanaoamini hakuna Mungu? Kwa nini yeye asiwe na uhuru wa kupayuka anachoamini?
 
Hapo Selemani Msindi alias afande Sele amekamatwa kwa kosa lipi na atashitakiwa kwa kosa gani na mlalamikaji ni nani?

Je, aliyelalamikiwa atajitokeza kuthibitisha kwamba ametendewa kosa?

Je, Jamhuri ya Tanzania inaweza kuchukua jukumu la kumshitaki mtu aliyetenda DHAMBI?

Je, kuna rejea yoyote ya hukumu ambayo serikali iliwahi kumwakilisha Mungu wakilalamikia kutendewa DHAMBI na nani alishinda?

Mahakama inakiri uwepo wa uwepo wa Mungu kwa nadharia ya kwamba kuna baadhi ya matukio pamoja na utalaamu wa binadamu hawezi kuzuia kama kifo (nani alishawahi kukata ryfaa dhidi ya kifo?)

Msanii afande Sele amefanya kosa la kimaadili ambalo msingi wake umetokana na kukashifu uwepo na uwezo wa Mungu baada ya kuacha kuzuia tukio fulani lisitokee;

Je, wafahamu kuwa ni kwanini waliokufa hawarudi, na hata waliowahi kupoteza fahamu kwa imani wakapelekwa mahali ambapo baada kuonesha kilichoko huko walikataa kurudi lakini walishurutishwa kurejea ambayo huitwa ufufuo wa mfu (muujiza)?

Kesi inayomhusisha Mungu ni ngumu kwa mahakama kuitolea uamuzi kwa kuwa Mungu hawezi kuhudhuria mahakamani kati umbo la binadamu kutoa ushahidi dhidi ya tuhuma.

Huko Marekani kuna mzungu mmoja (State Senate Ernie Chambers) aliwahi kumshitaki Mungu mahakamani na akadai fidia kutokana na imani aliyohubiriwa kutomsaidia.

Uamuzi wa mahakama ulitupilia mbali kesi hiyo kwa sababu baada ya mlalamikaji aliyepewa hati ya kumkamata alishindwa kumpata ili amkabidhi wito wa mahakama.

[Huyo aachiwe ila aonywe na kupewa nasaha za kisaikolojia kutokana na mfumo wake wa maisha umeathiri fikra, huenda akwa ndiye imamu au mhubiri mzuri kusaidia wengine]
Reference attached.
Umeelezea vizuri sana. Jamaa hana kosa lolote. Ni unafiki wa sisi binadamu tu. Sana sana polisi watakachofanya ni ku-harrass na kumuadhibu bila kosa lolote. Hakuna mahakama itakayoweza kuhukumu kesi hii kwani hana kosa lolote.
 
Kwa hyo tumuache tu ATUKANE?
Ndiyo nakumbaaje. Kama wewe na mimi tunamwamini Mungu lakini kuna wengi wanaona Mungu ni kitu cha kufikirika. Yaani hayupo kabisa. Hili ni suala la mtu binafsi na Mungu wake. Siyo suala lako wala langu wala la serikali. Kama ni adhabu ataipata yeye na siyo wewe wala mimi. Huu ndiyo uhuru wa kuabudu. Huyu siyo binadamu wa kwanza kufanya hili. Kwenye vitabu vitakatifu kuna mifano kede ya watu waliokuwa wanamhujumu Mungu. Mungu anajua namna ya ku-deal nao. Siyo kazi ya serikali. Jamaa hajakashfu dini yoyote bali amesema haamini kama Mungu yupo.
 
Kwa hyo tumuache tu ATUKANE?
Huyo aonywe tu na aambiwe kuwa 'Karma' humwadhibu hata aliyeshika mpini!!

Mungu ni zaidi ya fikra zenye ukomo za kiumbe chochote akiwemo binadamu bila kujali rangi, kabila, itikadi, dini, elimu, uchumi au jinsia wote wanatambua bayana kwamba yupo mwasisi wa uhai na ufu kwa sababu na wakati maalum.

Huyo msanii hatakiwi kusomewa dua wala kulaaniwa maana 'alaaniye naye hulaaniwa' dhamira yake inamsuta kama ana akili timamu maana anapolala na ufahamu kujitenga kwa muda na mwili lakini baada ya muda huzinduka au kuamka huthibitisha uwepo wa NGUVU inayozidi sayansi ya mwanadamu ni suala rahisi.

Mpuuzeni tu ataadhibiwa na nadhiri yake, maana huwa kuna mapepo huwa yanatafuta mahali pa kupumzika yakibaini uchafu wa roho yake yanamwingia kisha anaweza kuanza kutembea barabarani akiwa mtupu.
 
Sawa.ila muache kwanza wana kazi nae maalum.
Huyo aonywe tu na aambiwe kuwa 'Karma' humwadhibu hata aliyeshika mpini!!

Mungu ni zaidi ya fikra zenye ukomo za kiumbe chochote akiwemo binadamu bila kujali rangi, kabila, itikadi, dini, elimu, uchumi au jinsia wote wanatambua bayana kwamba yupo mwasisi wa uhai na ufu kwa sababu na wakati maalum.

Huyo msanii hatakiwi kusomewa dua wala kulaaniwa maana 'alaaniye naye hulaaniwa' dhamira yake inamsuta kama ana akili timamu maana anapolala na ufahamu kujitenga kwa muda na mwili lakini baada ya muda huzinduka au kuamka huthibitisha uwepo wa NGUVU inayozidi sayansi ya mwanadamu ni suala rahisi.

Mpuuzeni tu ataadhibiwa na nadhiri yake, maana huwa kuna mapepo huwa yanatafuta mahali pa kupumzika yakibaini uchafu wa roho yake yanamwingia kisha anaweza kuanza kutembea barabarani akiwa mtupu.
 
Umeelezea vizuri sana. Jamaa hana kosa lolote. Ni unafiki wa sisi binadamu tu. Sana sana polisi watakachofanya ni ku-harrass na kumuadhibu bila kosa lolote. Hakuna mahakama itakayoweza kuhukumu kesi hii kwani hana kosa lolote.
Kurusha video ya matusi mitandaoni,wakitaka kumkalisha anakaa.
 
Kakashifu imani ya nani? Mimi nilisikiliza ile clip. Haamini uwepo wa Mungu. Hili ni jambo la mtu binafsi. Alisema ataabudu hata jua. Huwezi kumlazimisha mtu kuamini na polisi wamefanya kosa kubwa sana. Acha Mungu ajitetee mwenyewe. Kwanza hili kwa Mungu siyo issue kubwa kama binadamu mnafiki anavyotaka ionekana. Mbona wapo watu kama kina Paulo walimhujumu Mungu lakini baada wakaja badalika?
Hata Yesu mwenyewe pale msalabani, kama kweli, alisema 'Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha', na dola na dini za wakati huo hazikufanya kitu.
 
Sheria hazihusiani na imani ya mtu. Sele hamwamini mungu. Kuna watu wanamwabudu shetani. Na shetani anatukanwa kila siku mbona hawakamatwi hawa. Nibasoma bibilia ya shetani nipo naendelea ili nijifunze pia ukuu wa huyu gangwe. Mwenye kutaka kopi njoo pm
 
Msanii mkongwe wa muziki, Selemani Msindi maarufu Afande Sele, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mjini Morogoro kwa mahojiano baada ya video yake iliyokuwa na maudhui ya kumlaumu Mwenyezi Mungu kwa kile alichodai hakutenda haki kuruhusu kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli.

Mkuu wa Polisi Morogoro kasema kesho ataongea kinagaubaka sababu za kumkamata na kumlaza Korokoroni.

Zaidi soma: Afande Sele (Seleman Msindi), asomewa dua ya kufa kabla ya Ramadhan ya 2021 kufika, atuhumiwa kumkufuru Mungu

Wanamsumbua bure na kuonyesha wazi wazi kama aliyetukanwa ana uwezo wa kuadhibu.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom