Morogoro: Selemani Msindi (Afande Sele) adakwa na kulazwa Korokoroni, mdomo wake wamponza

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
Msanii mkongwe wa muziki, Selemani Msindi maarufu Afande Sele, anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mjini Morogoro kwa mahojiano baada ya video yake iliyokuwa na maudhui ya kumlaumu Mwenyezi Mungu kwa kile alichodai hakutenda haki kuruhusu kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli.

Mkuu wa Polisi Morogoro kasema kesho ataongea kinagaubaka sababu za kumkamata na kumlaza Korokoroni.

Zaidi soma: Afande Sele (Seleman Msindi), asomewa dua ya kufa kabla ya Ramadhan ya 2021 kufika, atuhumiwa kumkufuru Mungu

FB_IMG_1616442950690.jpg
 
Alishaomba radhi asee,tena ameomba msamaha vizuri sana.
Amesema alipokea taarifa ya kifo cha JPM kwa mshtuko akachanganyikiwa na kuanza kuropoko.
Kama Mungu anasemehe sisi wanadamu ni wakina nani tusisamee?
Ingekua logic ni hiyo ingekua watuhumiwa wakifika mahakamani wanaomba msamaha halafu jaji anasema 'Kwakua Mungu anasamehe basi mtuhumiwa anaachiwa huru'
 
Alishaomba radhi asee,tena ameomba msamaha vizuri sana.
Amesema alipokea taarifa ya kifo cha JPM kwa mshtuko akachanganyikiwa na kuanza kuropoko.
Kama Mungu anasemehe sisi wanadamu ni wakina nani tusisamee?
Sheria za nchi hazitambui msamaha wa Mungu. La si hivyo watuhumiwa wote ambao wameokoka baada ya kushtakiwa wangekuwa nje.
 
Back
Top Bottom