Morogoro: Mwalimu Mkuu ampa kichapo na kumng'oa meno mwalimu mwenzake

Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi mkuyuni Morogoro vijiji Mussa Hasira Kwa Tuhuma za kumpiga kumng’oa jino la juu Mwalimu mwezake Witnes Makoti, huku chanzo kikiwa bado hakijafahamika.

Kamanda wa polisi Mkoa Morogoro Fortunatus MUSILIMU ametbibitisha kushikiliwa Kwa mtuhumiwa huyo huku akisema Kuwa tukio Hilo limetokea octoba 15 mwaka huu shuleni kwa kutumia fimbo ngumi na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili.

Majeruhi huyo baada ya kupata shambulio Hilo amepatiwa matibabu katika kituo Cha Afya mkuyuni na sasa anaendelea vizuri.
Hawa walimu jamani wana stress sn za maisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom