Morogoro: Muuguzi afariki baada ya kuchomwa kisu na Mgonjwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,482
9,242
Mtawa wa Kituo cha kuhudumia wagonjwa wa ukoma cha Nazareth kilichopo Ifakara, wilayani Kilombero mkoani Morogoro, Agatha Mbalalila (50) ameuawa kwa kuchomwa kisu.

Kifo cha Mtawa Agatha ambaye alikuwa muuguzi katika kituo hicho kilitokea juzi Machi 05, 2021 baada ya mmoja ya wagonjwa waliokuwa wakipatiwa matibabu katika kituo hicho (jina limehifadhiwa) kudaiwa kumchoma kisu wakati akielekea kuwahudumia wagonjwa wengine katika eneo la kituo.

Akizungumzia kifo hicho Katibu wa Kituo cha Nazareth, Ladislaus Mloti amesema marehemu alimpokea mtuhumiwa huyo wa mauaji Februari 27, 2021 baada ya kufika katika kituo na kujieleza kuwa ametoka katika matibabu ya ugonjwa wa ukoma katika Wilaya ya Bagamoyo.

Katibu huyo amesema mtuhumiwa baada ya kujieleza alionyesha kadi yake na kuonesha kuwa ni kweli alikuwa na matatizo ya ukoma na waliamua kumchukua na kumpima tena na kugundulika kuwa na ukoma na kuanzishiwa matibabu mapya.

Amesema mtuhumiwa hakuwa na matatizo ya akili wakati anapokelewa na waliamua kumlaza ili kumpatia matibabu ya vidonda alivyokuwa navyo mguuni na wakaona busara waanze kwanza kumtibia vidonda hivyo na baada ya kupona wangemruhusu arudi nyumbani ili kuendelea na matibabu ya ugonjwa wa ukoma.

Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mt. Francis, Dk Winfrid Gingo, amesema marehemu alifia hospitali wakati akipatiwa matibabu na uchunguzi wake umefanywa na daktari wa halmashauri ambaye bado hajawasilisha majibu ila walioshuhudia tukio na hata marehemu Agatha alipofika alilalamika kuwa alichomwa kisu.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fotunatus Musilmu akizungumza kwa njia simu akiwa wilayani Malinyi kikazi amesema hajapata taarifa rasmi juu ya tukio hilo na anawasiliana na Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Kilombero ili kupata taarifa zaidi.

Ippmedia
 
Mchongo utakuwa ulisukwa huu haiwezekani jina la aliechomwa liwekwe wazi halafu muuaji lifichwe
 
Atajuaje bila kupata taarifa? Au inabidi aoteshwe usiku?
Ukisoma vizuri utagundua kuwa baada ya kuambiwa hakutake any initiatives kutafuta ukweli wa taarifa hiyo. Nilidhani baada ya kupata hiyo tip angepiga simu kujua ukweli na angejibu mwandishi kuwa ameelezwa kwa kifupi, na kweli kwamba kuna hicho kifo lakini atatolea taarifa kamili baadae. Hiyo ndio namna nzuri ya ku deal na media boss wangu.
 
Visu mbona vingi hospitali labda ungeuliza huyo mkoma aliwezaje kushika kisu wakati tujuavyo ukoma huanza na vidole
Sio wote ambao ukoma uanzia mikononi boss,

Wengine ukoma uanza kula vidole vya miguuni, Mimi kuna askari Fulani namfahamu anatokea Dodoma alikuwa havai buti wala viatu maana ukoma ulikuwa umemla vidole vyote vya miguuni na baadhi ya sehemu za miguuni.
 
Halafu nasikia you ugonjwa huwa unamfanya muathirika awe na hasira za ghafla sana
Inawezekana mkuu, niliwahi kulisikia hili pia, navyofahamu mgonjwa akiugua kwa Muda mrefu anapata tatizo la kisaikolojia. Magonjwa kama TB, Cancer, HIV. etc.

Na kwa ugonjwa kama huu pia inawezekana maana kama sijakosea maelezo yanasema huyo jamaa alitokea kutibiwa kwanza Bagamoyo kisha ndio akahamia huko ifakara, Morogoro hivyo inaonyesha huenda alishaanza kutibiwa muda.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom