Morogoro: Moto wateketeza kituo kikubwa cha kupozea umeme cha TANESCO

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,200
4,673
Moto mkubwa umeunguza na kuteketeza kituo kikubwa kabisa chenye mitambo maalumu ya kupokea, kupoza na kusambaza Umeme kuelekea Mikoa ya Morogoro, Dar es salaam, Tanga na Kilimanjaro

Moto huo bado haujazimika hadi sasa na juhudi za kuuzima zinaendelea

Hadi sasa chanzo cha moto huo hakijulikani

ITV
 
Hakuna fire hapo,au ndio Yale Yale ya Kariakoo?
20210712_151618.jpg
 
Mwenye nchi kaacha kwake kunawaka moto kakimbilia kwa jirani tukisema tunaambiwa tunampinga kwa sababu ni mwanamke. Je hiyo ni halali kweli?
 
U mean kawasha moto kaondoka au? Ama angekuwepo na moto ukawaka angekuwa na jukumu la kuuzima yeye?
Ukiwa baba au mama wa familia alafu nyumbani kwako kukatokea matatizo utayaacha hayo matatizo familia iteketee na kwenda kula urabu kwa jirani?
 
HIZI NI HUJUMA AU?
mbona majanga yanazidi kila kukicha?
Enzi Za JP.
Upuuzi mwingi tulikuwa tumeusahau!

Tulibaki kulia na mambo madogo sana (Inshu za wanasiasa)
Lakini, Maisha Yalienda Vizuri pasi na Shida!

Huyu Mama Huyu???
Upuuzi upi?
 
Ili tanesco ipate baraka za Mungu waache kukandamiza raia, Washushe bei za umeme, na huduma iwe bora kwa kila mutu. Ona sasa yanayoikumba.


Waache kukandamiza
 
Hadidhi,hadidhi .Hapo zamani za kale, Kuna mama mmoja alikuwa akisafiri bila baba( mume), na baba watoto hawajui yuko wapi ,anafanya Nini au anasema nini.je familia hiyo Iko salama?
 
Back
Top Bottom