Morogoro: Mgogoro wa Wakulima na Wafugaji Itete, Malinyi

tumbili mweusi

New Member
Feb 15, 2021
3
2
Habari wana JamiiForums,

Kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu wa wakulima na wafugaji uliotokana na wafugaji kulisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima kuanzia mwezi wa sita mwaka2021, hatua mbalimbali zimechukuliwa na mpaka sasa hakuna ufumbuzi wa tatizo hili:

HATUA HIZO NI:
1. Kuwashirikisha viongozi wa wilaya wakiongozwa na mkuu wa wilayOC OCD na viongozi waandamizi bila mafanikio.

2. Kukamata mifugo na kuwafungungulia mashitaka mahakamani bila mafanikio

MATOKEO YA MGOGORO
1. Kendelea kulishiwa mazao ya wakulima na kutishia baa ya njaa

2. Uharibifu mkubwa kwenye miondombinu ya skimu ya umwagiliaji iliyogharimu pesa nyingi bilioni 6.5

3. Kuongezeka kwa chuki za wananchi dhidi ya serikali yao na kumkataa mkuu wa wilaya

4. Kubakwa na unyanyasaji wa kijinsia wanaofanyiwa wakulima hasa akina mama na Wanaume wa kisukuma

5. Kuongezeka kwa majeruhi ambapo tarehe28.12.2021 watu 6 wakulima wameshambuliwa vibaya na wafugaji na kupelekea mmoja wao kufariki dunia baada ya kupigwa na wafugaji
 
Mtu ana ngombe 1000 kuwalisha sasa
Hapo lazima awapeleke kwenye mashamba
Ya watu,na huko ndiko unapoanzaga ugomvi

Ova
 
Nomadic livestock ni mfumo wa kizamani sana wa kufuga wanyama. Nadhani ifikie wakati serikali iupige kabisa marufuku. Yatengwe maeneo husika (ranch), ili wafugaji wafuge mifugo yao kwa tija.
 
Nomadic livestock ni mfumo wa kizamani sana wa kufuga wanyama. Nadhani ifikie wakati serikali iupige kabisa marufuku. Yatengwe maeneo husika (ranch), ili wafugaji wafuge mifugo yao kwa tija.
Ranchi zi zilikuwepo

Ova
 
Yule msukuma pale Burigi alipaswa kutenga iwe ranch ya kufungua na malisho sio Mbuga ili kuweza kumaliza hizi vurugu za ndugu zake.
 
Inasikitisha kuona kuna upotoshaji mkubwa (misinformation) unaoendelea kupitia ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Na sasa DC amefikia kumdanganya hata RC morogoro juu ya mgogoro huu aliofuga mwenyewe tangu mwezi wa 6 mwaka huu!

Lakini mkutano wa Mhe. Mbunge Mgungusi uliofanyika jana uliweka bayana chanzo cha tatizo hili kuwa ni mkuu wa wilaya ya Malinyi, Masele kuegemea upande wa wafugaji na kudharau kero za wakulima!
 
Inasikitisha sana...
Toka kifo kimetokea na vurugu kufanywa na vijana, DC hajafika eneo la tukio kutoa pole kwa wafiwa, au kuangalia uharibifu mpaka leo hii?? Anaogopa nini??

Alishaonywa mara kadhaa kwenye mikutano ya wananchi lakini hakusikia, leo mauaji ya mkulima yametokea anapotosha habari, anamdanganya nani?? RC Shigella au Mhe. Waziri Ummy Mwalimu??

Wananchi hawamtaki hata kumuona huyu DC Masele, na kama RC anadanganywa basi aje naye Itete atapata majibu.
 
Mtu ana ngombe 1000 kuwalisha sasa
Hapo lazima awapeleke kwenye mashamba
Ya watu,na huko ndiko unapoanzaga ugomvi

Ova
Sasa ni kheri walishe kwa ustaarabu kuliko kulishia kwa nguvu huku mkulima akiwa amefungwa kamba mikononi, kukalishwa chini na akishuhudia live mazao yake yakilishiwa na yeye asifanye lolote!
 
Juzi tar 31.12.2021, DC Masele kaenda eneo la tukio kwa kificho huku akiwa kapanda gari ya takukuru na kukaa/kujificha siti ya nyuma.
 
Habari wana JamiiForums,

Kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu wa wakulima na wafugaji uliotokana na wafugaji kulisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima kuanzia mwezi wa sita mwaka2021, hatua mbalimbali zimechukuliwa na mpaka sasa hakuna ufumbuzi wa tatizo hili:

HATUA HIZO NI:
1. Kuwashirikisha viongozi wa wilaya wakiongozwa na mkuu wa wilayOC OCD na viongozi waandamizi bila mafanikio.

2. Kukamata mifugo na kuwafungungulia mashitaka mahakamani bila mafanikio

MATOKEO YA MGOGORO
1. Kendelea kulishiwa mazao ya wakulima na kutishia baa ya njaa

2. Uharibifu mkubwa kwenye miondombinu ya skimu ya umwagiliaji iliyogharimu pesa nyingi bilioni 6.5

3. Kuongezeka kwa chuki za wananchi dhidi ya serikali yao na kumkataa mkuu wa wilaya

4. Kubakwa na unyanyasaji wa kijinsia wanaofanyiwa wakulima hasa akina mama na Wanaume wa kisukuma

5. Kuongezeka kwa majeruhi ambapo tarehe28.12.2021 watu 6 wakulima wameshambuliwa vibaya na wafugaji na kupelekea mmoja wao kufariki dunia baada ya kupigwa na wafugaji
Mbona haya hatukuyasikia hapo kabla mwendazake hajaenda?
 
Back
Top Bottom