Morogoro - Matukio na Matokeo ya Uchaguzi Mkuu 2015 kama yanavyotujia

uungwana vitendo

JF-Expert Member
Nov 20, 2013
1,313
2,000
i thought ingekuwepo thread moja yenye matokeo ya nchi nzima. Hii ya mikoa yenyewe iko mingi si itasumbua sana?

uko sahihi

upo sahihi,au wangefungua kikanda

iwe ni kutoka nchi zima yani majimbo ya mikoa yote. Hii ya mkoa mmoja itachanganya sana.
naungana na huyu wa chini
hii ndiyo nzuri, unajua hali ilivyo kila mkoa tofauti.
Angalia hapo chini mada zinazofanana.ukitaka kujua mkoa wa mara hali ipoje unagonga tu.
 

mwambunnyara

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
520
250
Hakika Tanzania hatupo serious na mambo,mpaka dakika hii,katika kituo cha maelewano B na A nusu saa imepita watu bado hatujaanza kupiga kura,hii sio sawa kwanimuda wa kufunga ukifika hata hatuongezewi muda,huku nikutupunja muda wetu!!
 

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
14,985
2,000
toka Moro hapa, sitaki mchezoo nachinjaaaa kama sina hurumaaa, yano leo nawapa uhondo wote hapaa
 

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
14,985
2,000
hiyo ni sua, watu hawataki mchezooo, abood mwisho wake leo
 

Attachments

  • 1445752048195.jpg
    File size
    67.8 KB
    Views
    526

Pendael24

JF-Expert Member
Feb 13, 2014
3,682
2,000
Kwa hapa morogoto mjini kata ya sabasaba hali ni nzuri watu wamejitokeza kwa wingi kwenye vituo. Soko la sabasaba linalokuwepo kila jumapili limefungwa, shughuli nyingi nyingi zimesimama, mjini watu na magari ni wakuhesabu sana.
 

PNC

JF-Expert Member
Feb 3, 2015
7,988
2,000
Kama kawaida nishaliza kaz yangu ya kuchinja MKOLON MWEUSI hapa Dumila KILOSA kifup hali ya utulivu na kila mtu LOWASAAA
 

Eddyka

Member
Jul 11, 2015
42
95
Nimesha chagua maji barabara elimu bora na bure pamoja na afya njema bila kusahau uhakika wa umeme hapa kigurunyembe zahanati na nimewaona international observers kutoka Ireland wakikagua mchakato kifupi ni kwamba nimeshachinja maana hamna namna tena ni kuwachinja
Asanteni
 

p emy

Member
Sep 12, 2015
57
95
kilosa watu wamehamasika, tagu saa 11 alfajir foleni zimeanza, shughuli nyingi za kiuchumi na kijamii zimesimama au zimezorota, utulivu umetawala japo tafsir ya ujumla inawapa nafasi wagombea wa ccm haitakuwa rahisi kama wengi mnavyo dhani vijana wamehamasika.
 

jrutta

Member
Apr 7, 2012
46
95
Mi niko Tuliani kata ya madizini na tayari nimeisha fanya yangu tatizo ambalo linanitatiza ni kutaka ufafanuzi kuhusu hili:
Mwenye haki ya kukunja kiratasi baada ya kupiga kura ni nani? Je ni Mimi mwenyewe au nakunjiwa na karani alienipa karatasi hizo??
 

Danny greeny

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
3,858
2,000
Mtandao Hatari wa JF waanza kupingana na Matamko ya serikali na kuacha members wake wakipost Matokeo ya uongo na Baadhi kutangaza washindi katika baadhi ya matokeo kinyume cha sheria.

MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inapenda kutoa taarifa kwa umma kuhusu utangazaji wa matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa vyombo vya utangazaji kwa mujibu wa Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015. Kanuni hizi zipo kwa mujibu wa Sheria kama ilivyotolewa na Gazeti la Serikali la Tarehe 26 Juni, 2015. Kanuni hizi zinalenga kuweka utaratibu mzuri wa kutangaza shughuli za kampeni na uchaguzi mkuu kuwa wa amani na utulivu.

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania inapenda kuwakumbusha kuwa ni marufuku kwa vituo vyote vya utangazaji kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu bila kupata taarifa sahihi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa utaratibu waliojiwekea.

Vilevile, vituo vyote vya utangazaji vinapaswa kuzigatia Sheria na Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015.

Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015, Na. 16 (1) na 16(2) inaelekeza kama ifuatavyo:-

16(1) kwamba kila mtoa huduma za maudhui atakuwa na wajibu wa kuuarifu umma juu ya matokeo ya uchaguzi, kadiri yanavyopatikana. uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha usahihi wa matokeo yote yanayotangazwa.

16(2) Mtoa huduma za maudhui hatatangaza maoni ambayo yanaweza kuchochea vurugu au kuhamasisha chuki kwa misingi ya mbari, kabila, jinsia, dini au Imani za kisiasa na ambayo yanajenga uchochezi wa kusababisha madhara.

Hivyo basi, vituo vya utangazaji vinatakiwa kufuata kikamilifu Kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) (Utangazaji wa Uchaguzi wa Vyama vya Siasa), 2015 na kwamba vituo vya utangazaji vitawajibika na matokeo ya maudhui ya matangazo ambayo hayatozingatia Kanuni.

Mamlaka inatoa wito kwa vituo vya utangazaji kutumia weledi katika maamuzi ya kihariri kuchanganua kipi kinafaa kutangazwa na uangalizi maalumu ufanyike kuhakikisha kuna usahihi katika kutangaza matokeo yote yatakayotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAREHE 25/10/2015

Source: MICHUZI BLOG: KUTANGAZA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU

Mkurugenzi wa Uchaguzi Bw. Ramadhani sasa hivi akiongea live na ITV amesema kwamba Matokeo rasmi ya uchaguzi wa leo hayajatolewa kabisa infact hakuna hata kituo kimoja ambacho kimeshatoa matokeo, anasema kwamba ni Tume yake tu yenye mamlaka kisheria kutoa matokeo ya uchgauzi na wao hawajafanya hivyo bado, kwa hiyo matokeo yote yanayorushwa kwenye mitandao sasa hivi ni ya uongo na ni kinyume kabisa na Sheria.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom