Morogoro: Madiwani wamsimamisha kazi Mganga Mkuu kwa tuhuma za wizi wa mafuta

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,266
5,361
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro imemsimamisha kazi Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dustan Mshana kwa tuhuma ya wizi wa mafuta lita 100, kununua kumpyuta chakavu pamoja na kutosimamia vizuri idara yake hiyo.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Rachael Nyangasi, alisema hayo juzi kuwa mbali na huhuma hizo, pia Dk. Mshana anatuhumiwa kusimamia mapato lindwa ikiwa na matumizi mabaya ya ofisi kushindwa ni pamoja yake.

"Dk. Mshana anatuhumiwa kufoji saini za madereva na kuchukua mafuta lita 100 za magari ya halmashauri hii, lakini ameshindwa kutii maagizo ya mwajiri wake yaliyomtaka kuwasilisha kumpyuta mpya na sio chakavu," alisema Nyangasi.

Nyangasi alisema mwajiri alimtaka Dk. Mshana kununua kompyuta 19 mpya kwa ajili ya kukusanya mapato lindwa, lakini katika ukaguzi uliofanywa na mkaguzi wa ndani umebainika kuwa ni kumpyuta tatu pekee ndiyo mpya na nyingine ni chakavu.

Alisema Baraza la Madiwani limeona itoe uamuzi huo wa kumsimamisha Mganga Mkuu huyo ili iwe fundis aiokwa waadilifu huyo ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wa wilaya hiyo ya Gairo wasiokuwa waadilifu na amewataka watumishi kuwa na waledi.

Mwenyekiti huyo alisema katika ununuzi wa kompyuta hizo kuna watumishi wengine kadhaa nao wanatuhumiwa kuhusika na baraza limemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri kuchukua hatua stahiki kwa wahusika wote.

"Serikali imeongeza mishahara kwa wa tumishi wake, lakini bado kuna baadhi ya watumishi wasio waadilifu na kusababisha kutumia fedha zinatotolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo ya wana Gairo kwa matumizi yao binafsi, hili halikubariki," alisema.

Aidha, aliwataka madiwani wa halmashauri hiyo kusimamia vizuri ukusanyaji wa mapato kwenye kata zao na pia aliwahimiza kuhakikisha waziba mianya yote ya upotevu wa mapato kwa maslahi mapana ya maendeleo ya Gairo na taifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Jabiri Makame, alisema wote waliohusika na hoja za Mkaguzi wa Fedha za Serikali (CAG), wachukuliwe hatua kali ili kitendo hicho kisiweze kujirudia tena upya katika wilaya yake hiyo.

Source: Nipashe
 
Madaktari wengi ni wezi na wala rushwa.

Serikali ibadilishe sera idara ya afya inarudishwa nyuma sana na hawa mds.

#MaendeleoHayanaChama
 
Taaluma za watu zipo chini ya Madiwani ambao ni darasa la saba.
Wewe mwenyewe unazungumzia kiti usichokijua.

Anyway, Leo unabweka kuhusu Madiwani kuwa na nguvu hiyo, lakini kesho utakuja tena hapa kupigania demokrasia bila kujua hayo ndio matokeo.

Sheria ya serikali za Mitaa inaweka mamlaka ya nidhamu ya Mtumishi kiwa baraza la madiwani.

Lakini kuhusu huyo DMO ( Mkuu wa Idara ) huteuliwa na Katibu Mkuu Utumishi na hawalipwi TGS.

Kwahiyo, Sina hakika Kama mamlaka yake ya nidhamu bado Ni Madiwani.

Maana ninachohisi, In charge wake ambaye Ni DED ndio alitakiwa kuwasilisha shitaka lake kwa Katibu Mkuu.
 
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro imemsimamisha kazi Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dustan Mshana kwa tuhuma ya wizi wa mafuta lita 100, kununua kumpyuta chakavu pamoja na kutosimamia vizuri idara yake hiyo
Wa hivi ndio mafisadi wengi sana
 
DMO ananunuaje computer na wakati siyo Afisa Manunuzi? Computer zinapokelewa na Afisa Manunuzi kwa ukaguzi wa IT wa Halmashauri, hapo atashinda mapema sn
Kama aliyezipokea alikubali kwamba no mpyaa! imekula kwake! Manunuzi wanamruka kimanga maili kumi! (Anyway! mambo hayo huwa ni coordinated issue, mnunuzi na mpokeaji)
 
Wewe mwenyewe unazungumzia kiti usichokijua.

Anyway, Leo unabweka kuhusu Madiwani kuwa na nguvu hiyo, lakini kesho utakuja tena hapa kupigania demokrasia bila kujua hayo ndio matokeo.

Sheria ya serikali za Mitaa inaweka mamlaka ya nidhamu ya Mtumishi kiwa baraza la madiwani.

Lakini kuhusu huyo DMO ( Mkuu wa Idara ) huteuliwa na Katibu Mkuu Utumishi na hawalipwi TGS.

Kwahiyo, Sina hakika Kama mamlaka yake ya nidhamu bado Ni Madiwani.

Maana ninachohisi, In charge wake ambaye Ni DED ndio alitakiwa kuwasilisha shitaka lake kwa Katibu Mkuu.
Ukiondoa Mkurugenzi, watumishi wengine wote mamlaka Yao ya nidhamu na Baraza la Madiwani.
 
Taaluma za watu zipo chini ya Madiwani ambao ni darasa la saba.
Mkaguzi wandani sindokammaliza huyu sasa madiwani kosalao likowapi kusimamia hill

Unajua athari ambazo wagonjwa (safe government) wangeipata kupitia computer hizo kwenye mchakato wamatibabu kuazia mwanzo hadi kumwona Dr wake
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom