Morogoro: Lori la Mafuta lapata ajali na kulipuka, watu 104 Wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa...(Picha zinaogofya)

Lile tukio ni baya na si vema kufurahia kifo cha binadamu mwenzio.

Lakini kwa upande wa pili pale wamepunguzwa wezi wengi wanao waibia watu wanapo pata ajali za gari.

Wakati fulani huibia hadi marehemu.

R.I.P wachota mafuta ya ajali.

Marehemu haibiwi anapunguziwa mizigo,unaona mtu amekufa mfukoni anapesa utaacha aendenzao mochwari?
Na ukiacha usitegemee kama ndugu/familia yake itapata hizo mali
 
baada ya gari la mafuta kupata ajali polisi walijulishwa mapema, polisi wangeenda mapema ile ingebidi wawatawanye watu waliokuwa wakigema mafuta kwa kutumia nguvu kama vile mabomu ya machozi na njia zingine kama kuwapiga watu hii ingeleta taharuki na ingepelekea idadi ya watu wengi kusogea eneo la tukio hivyo kungekuwa na uwezekano mkubwa ya idadi ya vifo kuwa maradufu kifupi polisi wamecheza offside trick bila hivyo sasa hivi tungekuwa tunaomboleza vya polisi na idadi ya magari yaliyounguwa na watu ingekuwa maradufu poleni wote
Mmh hapana kabisa... Ni ngumu mno kukubaliana na hii dhana...
 
Kuna Lori Moja la mafuta lilipinduka mbele ya mto ruvu nikakuta watu na madumu nikaandika humu jamii forums kuwa polisi nendeni mkawapige virungu na mabomu nikatukanwa Sana humu jamii forums kuwa Nina roho ya shetani nk kwa tamko langu lile ona sasa maafa hayo
Una mdomo mbaya sana wewe
 
Uko sahii..ajali imetokeaa sehem ya mjin sn..ingekuaa kijiji ni sawaa..bt pale kituo kipo karibu
Mkuu na hapa ndo inakuja hoja yang ya msingi 'UMASIKINI' wafanyakaz idara za dharura wanalipwa mishahara kwa kazi gan idara hazipo active. Polisi ajali imetokea kuja kudhibit eneo la ajali wati wasijazane hapo ata kwa kuzungushia utepe hata wazo hilo hawakua nalo zimamoto na imewachukua zaid ya saa nzima toka moto ulipolipuka kufika eneo la tukio. Hawa watu wanalipwa mishahara kwa kaz gan wanayofanya. Sijawah kusikia ajali ya kijinga kma hii huko kwa wenzetu.
 
Sawa chief, umeamua kula vya haramu lakini tambua kuwa utaulizwa mali yako umeipata kwa njia gani. Allah akuongoze!
Hayo mengine tutajuana mbele ya safari.watu wameenda kuhiji na hela ya unga sembuse mie.
 
Picha za video zipo.Wanaochota mafuta wanaonekana wazi.Polisi iwakamate iwashitaki kwa makosa yafuatayo la kwanza la wizi wa mafuta la pili.kosa la mauaji kwa kuwasha Moto ulioua watu na la kusababisha uharibifu wa Mali kwa kuteketeza Lori na Mali zingine.Wakidakwa na kufunguliwa mashtaka tabia ya kupora gari zinazopata ajali zitapungua
 
IMG_3617.JPG
 
Tatizo sio spillage ila watu walitoboa tank kuvujisha fuel. SS wabongo huwa tunapuuzia mambo ya msingi ikiwemo kuibia wahanga wa ajali nk. Sasahili liwefundisho
Kweli liwe fundisho, kitendo kile always huwa hatari sana, picha kama hizo niliziona ktk kitendo cha namna iyo kilichotokea uko Kongo DRC na hatukujifunza lolote.
 
Back
Top Bottom