Morogoro: Kijana mwenye umri wa miaka 17 amuua baba yake kwa kumpiga ngumi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
Jeshi la polisi mkoani Morogoro linamshikilia Yohana Lameck (17) kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Issaya Lameck (47) kwa kumpiga ngumi na kumkanyaga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, amesema tukio hilo limetokea Mei 31, 2020 majira saa 12 asubuhi katika kitongoji cha Manyani kata ya Mkalama, Tarafa na Wilaya ya Gairo.

Mutafungwa amesema kulikuwa na ugomvi baina ya mtoto na baba.

Kamanda amesema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kutokana na makosa aliyoyafanya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo yote yanatokea kwa sababu mzazi alishindwa kuweka mazingira ya kuheshimiwa na watoto.

Kunamalezi mengine yanafanya mtoto akuchukulie poa tu na ndio hatma ya haya mambo
Unaweza kuta alikuwa anamtuma fegi....mara karud nyumbani amelewa na kujua michepuko ya baba ake waziwazi.
 
Mkuu usiseme hivyo,kuna watoto wamevurugwa..mtoto miaka 18 ashaanza kuvuta bange,anakaba watu mtaani mzazi ukijaribu kumsogelea mbona unatafuta mauti
Hata avute bangi ya jamaika sijafikia hatua ya kupigwa na mtoto. Km hyo bangi tumeivuta sn enzi hizo na mdingi unamkwepa hata asijue coz displini ilkua mbele. Dingi anakunywa lakini hawezi rudi nyumbani anapepesuka na yuko ontime saa mbili kashafika home olewako uje baada yake ndio utajua dunia inazunguka jua.
 
Back
Top Bottom