MOROGORO: Halmashauri Kilosa yapiga marufuku mikusanyiko yote ikiwemo sherehe, kuepuka kipindupindu


Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Messages
3,090
Likes
4,101
Points
280
Age
28
Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2014
3,090 4,101 280
Halmashauri ya wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro imepiga marufuku mikusanyiko yote ya watu ikiwemo sherehe za harusi na upikaji wa vyakula kwenye magenge na mama lishe katika kata za Msowero na Rudewa kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo hayo.

Akiongea kwenye uzinduzi wa mradi wa usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo bora unaotekelezwa chini ya ufadhili wa shirika la Norwegian Church Aid, NCA, kutoka nchini Norway, afisa afya na usafi wa mazingira wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa Aloyce Semiono amesema tatizo la kipindupindu katika kata hizo limekuwa sugu kwani wananchi wengi hawazingatii kanuni za usafi huku kaya nyingi zikiwa hazina vyoo na watu wengi wakijisaidia ovyo porini ama kwenye mito.

Kwa upande wake Afisa miradi wa shirika la NCA Lazaro Makobero na Katibu mkuu wa Kanisa la Kianglikana Dayosisi ya Morogoro Chars Pangapanga wamesema mradi huo utasaidia kuhamasisha utunzaji wa vyanzo vya maji, ujenzi wa vyoo bora na kuvitumia katika maeneo mengi ya wilaya za Kilosa na Gairo, mkazo mkubwa ukiwa ni afya bora kwa wananchi ili waweze kushiriki kikamilifu katika shughuli zao za maendeleo.

Nao baadhi ya wananchi wakiwemo akinamama katika kata ya Msowero wilayani Kilosa walioyokutwa na ITV wakichota maji mtoni wamesema wanalazimika kutumia maji ya mto ambayo siyo safi wala salama kutokana na ukosefu wa visima na maji ya mabomba kwani mpaka sasa kuna visima viwili tu ambavyo vina msongamano mkubwa wa watu wanaochota maji kwa zamu usiku na mchana.

Chanzo: ITV
 

Forum statistics

Threads 1,273,060
Members 490,262
Posts 30,469,631