Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Basi la Kampuni ya Ilasi Express linalofanya safari zake kati ya Dar es salaam kwenda Tunduma limepata ajali leo Oktoba 4, 2019 kwa kugongana na Lori maeneo ya Kasanga mkoani Morogoro.
Taarifa za awali zinasema katika ajali hiyo imesababisha kifo cha dereva wa Lori aliyefariki papo hapo huku majeruhi wapatao 30 wakikimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Morogoro, ambapo kati yao wanaume 14 na wanawake 16.
Mganga mkuu mfawidhi wa hospitali hiyo, Rita Lyamuya amethibitisha kupokea majeruhi hao ambapo amesema watatu kati yao wana hali mbaya na wawili wamepewa rufaa ya kwenda katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Chanzo cha ajali ni dereva wa basi la abiria kutaka kulipita gari lingine bila tahadhari ambapo ilipelekea kugongana uso kwa uso na Lori hilo.