Morogoro: Baba amuua mwanae kwa kumtumbukiza kwenye kisima

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
Mtoto afariki dunia kwa kutumbukizwa
katika kisima cha maji na baba yake
mzazi Morogoro.
7cfd1c62153d13cc145012b689318f1a.jpg

Katika hali isiyo ya kawaida mtoto mmoja aliye julikana
kwa majina ya Elena Mussa mwenye umri wa mwaka
mmoja na miezi mitano mkazi wa kijiji cha Mazoka
wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro amekutwa
akiwaamekufa ndani ya kisima cha maji kwa kile
kilicho daiwa kudumbukizwa na baba yake mzazi
mwenye matatizo ya akili kwa muda mrefu.

Wakizungumza na ITV mashuhuda wa tukio hilo na
ndugu wa marehemu wamesema wakati walipo enda
kuchota maji katika kisima hicho waliuona mwili wa
mtoto huyo ukielea majini kisha kutoa tarifa kwa
mwenyekiti wa kijiji.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Rozi
amesema baada ya kuona tukio hilo alitoa tarifa Polisi
ndipo taratibu za kutoa mwili huo zilianza huku babu
wa marehemu Bwana.Mwanangumi Makala akieleza
jinsi kifo cha mjukuu wake kilivyo tokea.

Kwaupande wake mganga wa Hospital ya wilaya ya
Kilosa Julius Chiduo amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo ambapo akitoa taarifa za uchunguzi wa mwili wa
marehemu amesema mtoto huyo amefariki baada ya
kukosa hewa kwa kuzibwa pua na kushindwa kupumua
jambo ambalo limepelekea kupoteza uhai wake.

Chanzo: ITV
 
Kwa kweli mungu atusaidie , mbona kumekuwa na matukio ya kutisha kila kukicha, R.I.p
 
Hivi ni lini tutajifunza tunandugu na jamaa zetu wenye matatizo ya akili na tunaishi nao majumban tukiamin kabisa hawana madhara, jaman tuwapeleke sehemu husika hii haimaanishi hatuwapendi la hasha ni kwa usalama wetu wenyewe.
Sasa siku yakipanda ndo madhara yake hayo.
 
Mungu wetu upo wapi twakuomba uwapiganie watoto wetu hawa.R.I.P mtoto
 
Aisee! Jaman so sad! inakuwaje kuish na hao watu karibu !mfano jirani napoishi kuna mtu wa namna hiyo na anaish na ndugu zake na kuna vitoto vidogo.sasa najiuliza ikitokea siku akafanya tukio hapo.nani wakulaumiwa?mmh hatari kwakweli!
 
Back
Top Bottom