Morogoro: Atiwa mbaroni kwa kutumia namba ya NMB kuiba Mtandaoni

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,807
11,969
POLISI mkoani Morogoro imefanikiwa kuwatia mbaroni watu watatu akiwemo Filbert Katabazi (35) dalali wa magari mkazi wa Makongo Dar es Salaam, aliyekuwa akisakwa kwa muda mrefu na Polisi kwa tuhuma za wizi wa mitandao na utapeli.

Mtuhumiwa huyo anadaiwa kufunguliwa kesi mbalimbali za tuhuma za wizi wa mitandao na utapeli na kujipatia fedha Sh milioni 4.9 zilizohamishwa kutoka akaunti ya Amos Mniko iliyopo Benki ya NMB. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa alisema jana kuwa tukio hilo lilifanyika Oktoba 25, mwaka huu, majira ya saa mbili usiku ambapo mlalamikaji Mniko alifika kituo cha Polisi Morogoro na kutoa taarifa za kuibiwa fedha Sh milioni 4.9 kutoka katika akaunti yake ya NMB na kuhamishiwa akaunti nyingine ya NMB.

Alisema Oktoba 23, mwaka huu, mlalamikaji alihamisha fedha Sh 710,000 kutoka akaunti yake ya NMB na kumtumia mke wake kwa M-Pesa lakini hakupata mrejesho wa muamala kutoka NMB. Alieleza kuwa aliamua kupiga simu kwenda NMB huduma kwa wateja NMB 0786800008 ambayo aliikuta katika kadi yake na kupokewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mfanyakazi wa NMB ambaye ni Filbert Katabazi mkazi wa Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi huyo mlalamikaji alimjulisha kuwa anahitaji apate taarifa ya fedha aliyotuma, ndipo alipopewa maelekezo kadhaa ya kufanya hatimaye akashtuka kuona Sh milioni 4.9 zimehamishwa kutoka katika akaunti yake. Kamanda Polisi mkoa alisema, upelelezi wa kina ulifanyika na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili ambao ni Hans Bakari na Hamis Msangi waliohamishiwa fedha na Katabazi ambaye anatumia namba ya NMB huduma kwa wateja kuwaibia wateja wa NMB.

“Mtuhumiwa huwadanyanga vijana kuwa anawatafutia ajira kisha kuwafungulia akaunti NMB chapchap na kuchukua kadi zao akidai kwenda kuwafanyia uhakiki wa daftari la mishahara, akaunti ambazo hutumika kufanyia uhalifu huo wa kimtandao,” alisema Kamanda Mtafungwa. Kamanda alisema juhudi za kuwakamata watuhumiwa wengine anaoshirikiana nao ambao majina yao yamehifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi zinaendelea.
 
Huyo anatakiwa akae jela hadi ujuzi wa kielektroniki ufutike kwenye ubongo wake
 
Atatuliwe marinda ili dushe lisiwe na nguvu milele yote!
Anaibia watu ili akahonge huyo mbwiga!!
 
Back
Top Bottom